Kanisa Katoliki lasema ndoa zitaendelea kufungishwa ila watahusika Wanandoa na Wasimamizi wanne tu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,251
2,000
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anaitwa Padri Dr. Charles Kitima amefafanua tamko la Kanisa Katoliki kuzuia watu kufunga ndoa nakusema hawajazuia sakramenti hiyo ila wamezuia wale wanaotaka kufanya sherehe.

“Ibada ya kupokea Sakrament ya ndoa na kipaimara hizi shughuli zisiandamane na shamrashamra, ukishafunga ndoa kusiwepo sherehe, kinachofanyika ni mkusanyiko wa Ibada, kama unataka na sherehe subirisha” Katibu Mkuu TEC.

“Ndoa zinaendelea kufungwa, mtu amekaribia kufa huwezi mnyima Ubatizo, nyie Wachumba mmepanga kufunga ndoa April njooni Kanisani mtafunga mko wawili na wasimamizi wanne, distance mita moja moja lakini hamna sherehe” Katibu Mkuu TEC Padri Kitima.

“Tafsiri iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari haikuwa sahihi, Askofu hakuwa na maana kwamba anasimamisha sakrament, hakuna anayeweza kusimamisha huduma za Yesu” Katibu Mkuu TEC Padri Kitima.
 
GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,890
2,000
Hizi tahadhari za corona ni vituko tupu!

Hao watu wanne ndio hawawezi kuambukizana?

Kama mtu mmoja anaweza kuwaambukiza watu kumi kwa siku katika mazingira tofauti tofauti, na watu kumi nao wakawaambukiza watu mia wengine katika mazingira tofauti tofauti, seuze watu wanne wenye kila chances za kuambukizana na wakaenda kuwaambukiza wengine majumbani?

I see no point with this corona bullshits! Nawa mikono sijui sanitaiza! Upuuzi mtupu!

A contagious disease, unawaambia watu nawa mkono?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,302
2,000
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anaitwa Padri Dr. Charles Kitima amefafanua tamko la Kanisa Katoliki kuzuia watu kufunga ndoa nakusema hawajazuia sakramenti hiyo ila wamezuia wale wanaotaka kufanya sherehe.

“Ibada ya kupokea Sakrament ya ndoa na kipaimara hizi shughuli zisiandamane na shamrashamra, ukishafunga ndoa kusiwepo sherehe, kinachofanyika ni mkusanyiko wa Ibada, kama unataka na sherehe subirisha” Katibu Mkuu TEC

“Ndoa zinaendelea kufungwa, mtu amekaribia kufa huwezi mnyima Ubatizo, nyie Wachumba mmepanga kufunga ndoa April njooni Kanisani mtafunga mko wawili na wasimamizi wanne, distance mita moja moja lakini hamna sherehe” Katibu Mkuu TEC Padri Kitima

“Tafsiri iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari haikuwa sahihi, Askofu hakuwa na maana kwamba anasimamisha sakrament, hakuna anayeweza kusimamisha huduma za Yesu” Katibu Mkuu TEC Padri Kitima
Hii ni habari mbaya kwa shetani na timu yake (wakashifu dini & washabikia lock down)
 
Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
4,026
2,000
Yohana mbatizaji Yule wa memba wa LB7 alileta Uzi uliopotosha taarifa iliyotolewa haya kupelekea ufafanuzi huu.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,999
2,000
Fine, unapendekeza nini? Current data suggest hygiene and social distancing are working! Contagious diseases have been with us from time immemorial and have been combated in this way
Hizi tahadhari za corona ni vituko tupu!

Hao watu wanne ndio hawawezi kuambukizana?

Kama mtu mmoja anaweza kuwaambukiza watu kumi kwa siku katika mazingira tofauti tofauti, na watu kumi nao wakawaambukiza watu mia wengine katika mazingira tofauti tofauti, seuze watu wanne wenye kila chances za kuambukizana na wakaenda kuwaambukiza wengine majumbani?

I see no point with this corona bullshits! Nawa mikono sijui sanitaiza! Upuuzi mtupu!

A contagious disease, unawaambia watu nawa mkono?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
luck

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
951
1,000
Kuna mtu alisema mtumweusi bado yupo kwenye zile hatua za uumbwaji wa mwanadamu. Hizi kauli zinadhibitisha hili. Kule kwa madiba wanalalama wameminywa kuzika watu wao wkt huu wa korona. Wanadai waongezewe idadi ya wanaoruhusiwa kushiriki mazishi kutoka 50 iliyopo sasa hadi 150. Hii ni afrika aka 'Bara la giza'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,020
2,000
Katoliki nimewakubali Leo Kwa kauli hii....
Unafunga ndoa unasepa zako home na maisha yanaendelea hiyo nimeipenda
 
Maarko

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,160
2,000
Kanisa Katoliki linajichanganya sana katika hili,Rais wa TEC alisema hakuna kufunga ndoa,wakasema agizo hilo ni jimboni kwake Mbeya,kila siku tutasikia matamko kutoka kwao.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,212
2,000
Kipindi kizuri Kweli hiki kuoa aise
Humalizi hata laki mbili
Hakuna mambo ya kamati

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha huku nilipo kuna kipindi cha channel 4 wataanza kurusha live ndoa na kuangaliwa na maelfu ya watu kinaitwa Wedding in Lockdown
Baada ya kusitisha ndoa za kanisani
Yaani weeding online hii kiboko
Kweli dunia imebadilika

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
nabali

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
280
500
Nimewapenda bure wakatoliki, naamini itasaidia kutuondoa katika utumwa wa kuwa na masherehe makubwa wakati wanooana ni wawili tu! Katika hili nawapongeza wachina kuleta hii noma... kuna msemo kuwa if you can not learn in a soft way, then yuo will learn in a hard way!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,764
2,000
Kuna jamaa anaitwa Johnbaptist humu, nilimpinga kwenye Uzi wake wa kupotosha kuwa kanisa katoliki limesitisha ubatizo na ndoa. Anajifanya yeye anajua ukatoliki kuliko warumi wenyewe.
Hajui humu wengine ni mapadre.
Watu tumezaliwa misheni, tukakulia na kubalehe kwenye maseminari. Siyo seminary hizi uchwara za siku hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,306
2,000
Hizi tahadhari za corona ni vituko tupu!

Hao watu wanne ndio hawawezi kuambukizana?

Kama mtu mmoja anaweza kuwaambukiza watu kumi kwa siku katika mazingira tofauti tofauti, na watu kumi nao wakawaambukiza watu mia wengine katika mazingira tofauti tofauti, seuze watu wanne wenye kila chances za kuambukizana na wakaenda kuwaambukiza wengine majumbani?

I see no point with this corona bullshits! Nawa mikono sijui sanitaiza! Upuuzi mtupu!

A contagious disease, unawaambia watu nawa mkono?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kila kitu lazima kuchangia, kuna mambo mengine yanawataalam wake, ni ajabu hadi leo hujui umuhimu wa kunawa mikono, kwa sabuni kuwa ni njia bora ya kukabiriana na covid-19?!!!social distancing nayo hiitambui?!!!
 
Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,026
2,000
adi rahaaaaa...msimu wa kufunga ndoa kwa gharama ndogo, kanisani ibada watu wanne tu (wazazi wanasimama kando) no wifi no kakaz....no ukumbini, mwarudi ome na kuserebukaaa 🍷
 
The Most Winner

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
736
1,000
Hizi tahadhari za corona ni vituko tupu!

Hao watu wanne ndio hawawezi kuambukizana?

Kama mtu mmoja anaweza kuwaambukiza watu kumi kwa siku katika mazingira tofauti tofauti, na watu kumi nao wakawaambukiza watu mia wengine katika mazingira tofauti tofauti, seuze watu wanne wenye kila chances za kuambukizana na wakaenda kuwaambukiza wengine majumbani?

I see no point with this corona bullshits! Nawa mikono sijui sanitaiza! Upuuzi mtupu!

A contagious disease, unawaambia watu nawa mkono?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hujui Haya mambo yalivyo ndo maana unachangia kulingana na ufahamu wako siwez kukulaumu maana hujui unachokisema ukilinganisha na Imani ya Kanisa Cathoric, Mambk matakatifu hayawezi kusitishwa kwa sababu ya korona.

Ni saws na kusema tuache kumtukuza Mungu kwa sababu ya korona hiyo haiwezekani. Kinyume cha hapo basi tutamtukuza shetani bila kutambua.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom