Kanisa Katoliki lapinga matokeo ya uchaguzi DRC

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
kanisa-696x392.jpg

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) hayaakisi taarifa zilizokusanywa na waangalizi wake.

Jana alfajiri, CENI ilitangaza matokeo ya uchaguzi ya urais ambayo yalimtangaza Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia 38.5, akiwazidi Emmanuel Shadary wa chama tawala na Martin Fayulu aliyekuwa anaungwa mkono na vyama kadhaa vya upinzani.
“Tunaona matokeo ya urais yaliyotangazwa na CENI kuwa hayaendani na takwimu zilizokusanywa na waangalizi wetu katika vituo vyote vya kupigia kura nchini,” amesema Padri Donatien Nshole ambaye ni msemaji wa Baraza la Maaskofu nchini humo.
Wiki iliyopita, Kanisa hilo lilisambaza waangalizi 40,000 kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo. Baada ya kukusanya takwimu zake, ilieleza kuwa inafahamu mshindi wa uchaguzi huo lakini ikaitaka CENI kuhakikisha inamtangaza mshindi kwa haki.

Mwanadiplomasia Mwandamizi wa Ufaransa, Nshole alieleza jana kuwa takwimu za Kanisa Katoliki zimeonesha kuwa Martin Fayulu ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na sio Tshisekedi.
Takwimu za CENI zinaonesha kuwa Tshisekedi alipata kura Milioni 7 na Fayulu akimfuatia kwa kura Milioni 6.4 huku mgombea wa chama tawala, Emmanuel Shadary akiambulia kura Milioni 4.4.
Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa Januari 25 mwaka huu kuwa Rais wa Tano wa DRC akihitimisha utawala wa miaka 18 wa Rais Joseph Kabila. Anaandika historia mpya ya kuwa rais wa kwanza aliyekabidhiwa madaraka kwa njia ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura.
 
Huna msimamo

Jana ulikuwa unapongeza ushindi pamoja na bavicha wenzio
weka hapa andiko lolote kuhusu mimi kushangilia ushindi wa Tshishekedi

Soma nyuzi zangu kwenye jukwaa ya kimataifa kuhusu uchaguzi wa DRC
 
View attachment 992134
Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) hayaakisi taarifa zilizokusanywa na waangalizi wake.

Jana alfajiri, CENI ilitangaza matokeo ya uchaguzi ya urais ambayo yalimtangaza Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia 38.5, akiwazidi Emmanuel Shadary wa chama tawala na Martin Fayulu aliyekuwa anaungwa mkono na vyama kadhaa vya upinzani.
“Tunaona matokeo ya urais yaliyotangazwa na CENI kuwa hayaendani na takwimu zilizokusanywa na waangalizi wetu katika vituo vyote vya kupigia kura nchini,” amesema Padri Donatien Nshole ambaye ni msemaji wa Baraza la Maaskofu nchini humo.
Wiki iliyopita, Kanisa hilo lilisambaza waangalizi 40,000 kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo. Baada ya kukusanya takwimu zake, ilieleza kuwa inafahamu mshindi wa uchaguzi huo lakini ikaitaka CENI kuhakikisha inamtangaza mshindi kwa haki.

Mwanadiplomasia Mwandamizi wa Ufaransa, Nshole alieleza jana kuwa takwimu za Kanisa Katoliki zimeonesha kuwa Martin Fayulu ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na sio Tshisekedi.
Takwimu za CENI zinaonesha kuwa Tshisekedi alipata kura Milioni 7 na Fayulu akimfuatia kwa kura Milioni 6.4 huku mgombea wa chama tawala, Emmanuel Shadary akiambulia kura Milioni 4.4.
Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa Januari 25 mwaka huu kuwa Rais wa Tano wa DRC akihitimisha utawala wa miaka 18 wa Rais Joseph Kabila. Anaandika historia mpya ya kuwa rais wa kwanza aliyekabidhiwa madaraka kwa njia ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura.
Hawa nao wanalao jambo,Waache mahakama itoe maamuzi, naanza kuamini ni wengi wanataka Congo waendelee kutwangana ili waweze kuifikia virgin land na kuvuna mali
 
Hongera Felix Tshisekedi...Wazungu washenzi sana, walitaka mtu wao wamweke + kanisa katoliki.
 
Back
Top Bottom