Kanisa Katoliki 'lapigilia msumari' adhabu dhidi ya waumini

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,521
2,000KANISA Katoliki katika Jimbo la Sumbawanga, mkoani Rukwa, limevunja ukimya na kunena kuhusu mambo yaliyosababisha waumini wake, kutengwa na wengine kuwekewa pingamizi kwa kukufuru utatu mtakatifu wakati wa uchaguzi mkuu, uliomalizika Oktoba 31 mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya baadhi ya vyombo vya habari, kuandika na kuchapisha habari kuhusu sakata hilo huku kanisa likiwa halizungumzi lolote.

Kitendo hicho, kiliwafanya baadhiya wananchi waliowahi kusoma habari hizo kutaka kujua ukweli kuhusu madai kuwa kanisa, limewatenga baadhi ya waumini wake kwa kukufuru utatu mtakatifu wakati wa uchaguzi mkuu.

Jana, Wakili wa Kiaskofu katika Jimbo la Sumbawanga, Padri Modest Katonto, alikiri kuhusu adhabu hiyo kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo na kwamba hakuna anayeweza kuitengua.

"Kanisa lingependa ifahamike kuwa hakuna mamlaka yoyote ya kidunia, inayoweza kuwaoondolea waumini hao adhabu hiyo, isipokuwa kwa jitihada za mtu mwenyewe binafsi kujipatanisha na kanisa kwa wale waliotengwa," alisema Padri Katonto.
Kanisa hilo pia limesema halina itikadi za kisiasa na kwamba adhabu zimetolewa kwa waumini hao, hazijali wadhifa wa mtu yeyote katika jamii.

Alisema kilichozingatiwa ni makosa ya kwenda kinyume cha imani na kushabikia mafundisho potofu.

Wakili huyo wa kiaskofu, alisema waumini waliokumbwa na adhabu hizo wako katika makundi mawili na kwamba la kwanza, ni la waliotengwa kwa kosa la kujilinganisha na utatu mtakatifu na kushabikia mafundisho potofu, huku wakijua wazi kuwa kitendo hicho ni cha uovu.

Kwa mujibu wa Padri Katonto, kundi hilo lina jumla ya waumini 27.
Alisema kwa mujibu wa sheria ya kanisa namba 1364, kosa lililofanywa na watu hao, linawatenga na umoja wa kanisa hata bila kutangaziwa au kujulishwa na kiongozi wa kanisa.

Alisema chini ya adhabu waliyopewa, waumini hao wamepoteza haki ya kushiriki katika idaba zote za hadhara za kanisa katoliki, kutoshiriki katika maadhimisho ya sakramenti, kutopokea akramenti na kutoshirki katika shughuli za uongozi wa kanisa .
Alisema "ikiwa aliyetengwa atahudhuria au atakuwepo katika mazingira ya inapofanyika ibada, lazima aondoke au au kama hatatoka, ibada itasitishwa. Na ikiwa atakufa bila kutubu, hatapewa maziko ya kanisa," alisema Padri Katonto.
Padri Kantonto alisema kundi la pili ni la waumini waliowekewa pingamizi ambao hata hivyo, hakutaja idadi yao.

Alisema chini ya pingamizi walilowekewa, waumini hao wananyimwa haki ya kupata huduma za kanisa kwa muda, wakati makosa yao yakichunguzwa na kwamba kama itabainika kuwa hawakufanya, watarudishiwa huduma zote.

Alisema hata hivyo, pingamizi hilo haliwaondowi watu wa kundi katika umoja na kanisa, kama ilivyo kwa waliotengwa.

Alisema katika kipindi cha uchaguzi mkuu, kanisa lilijitahidi kuwakumbusha waumini wake kuhusu nafasi zao na wajibu wao, lakini kinyume chake kanisa limeshuhudia, na kusikia baadhi ya waumini wakionyesha utovu wa nidhamu kwa kukufuru utatu mtakatifu.

"Walikufuru utatu mtakatifu, baadhi ya wagombea wakajifafanisha na Mungu mwenye nafsi tatu, kukufuru msalaba mtakatifu wa kanisa kwa kuuzika, kukejeli, kutukana na kudharau viongozi wa kanisa na wakristo wenzao," alisisitiza Padri Katonto.

Alisema vitendo hivyo vimesikitisha mno mama kanisa kwa sababu vimeambatana na usaliti wa imani na maadili ya kikristo.


"Lakini pia vitendo hivyo ni makwazo kwa wana kanisa na wakristo wa madhehebu mengine na watu wote wenye mapenzi mema," alisema.
Alisema wanaotenda makosa kama hayo kwa mujibu wa sheria, kanisa, lina haki ya msingi ya kuwaadhibu na kwamba adhabu hizo si ngeni ndani ya kanisa.
Kasisi huyo alifafanua kuwa shutuma dhidi ya kanisa kuwa limewatenga na kuweka pingamizi waumini wake kwa sababu za itikadi za kisiasa ikiwa ni pamoja na kuipigia kura CCM ni uwongo na uzushi wenye lengo la uchochezi.

"Kanisa Katoliki linahoji hivi uchochezi huo unafanywa kwa maslahi na manufaa ya nani," alisema.
Alisisitiza kuwa kamwe kanisa halitokaa kimya bila kukemea uovu kwa hofu ya vitisho na uzushi unaolenga katika kutetea maslahi ya kundi la watu wachache wasio na dhamira safi.
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,237
1,500
Watu waache kuingilia mambo ya imani nyingine. Habari hii ilivyokuwa ikiripotiwa kwa mara ya kwanza zilikuwa na upotoshaji mwingi na hasa kuchochea vurugu zilisizo na maana. Muumini anayejua imani yake na kuadhibiwa kadiri ya imani hiyo anapolalamika kwenye vyombo vya habari ni ulimbukeni wa hali ya juu.

Kadiri ya ufafanuzi wa Padre huyo wa Kanisa, wahusika wamenyimwa sakramenti za kanisa kwa sababu kwa matendo na maneno yao wameasi kanisa. Wataendeleaje kung'ang'ani imani ambayo wanaikejeli?
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
umeamua kuleta thread inayochanganya dini na siasa .... kama kanisa linavyotaka kutofautisha dini na siasa .... na kusisitiza umuhimu wa maadili na ubora wa viongozi... please be very careful here ..... take note .... maadili ya viongozi.... maisha ndani ya imani... na siasa kama daraja la kupata uongozi.... vitu vitatu tofauti:

discard this thread, it is potentially baffling
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,712
2,000
Huu ndio ule udini alioukemea mkuu? Maana naona kuna watu wanali underestimate kanisa
 

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
1,763
2,000
Nafikiri hawa jamaa waliotengwa waliona ccm ndio kila kitu wakasahau imani yao muhimu ya dini waliyobatizwa nayo sijui tuite ni ulimbukeni au kiburi au makusudi? Ok waende kwenye dini ya mafisadi ya freemasons. Walijua kwakuwa wao ni ccm hawataguswa
 

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
umeamua kuleta thread inayochanganya dini na siasa .... kama kanisa linavyotaka kutofautisha dini na siasa .... na kusisitiza umuhimu wa maadili na ubora wa viongozi... please be very careful here ..... take note .... maadili ya viongozi.... maisha ndani ya imani... na siasa kama daraja la kupata uongozi.... vitu vitatu tofauti:

discard this thread, it is potentially baffling

Hii thread hapa ni mahali pake kwa sababu inaelezea suala ambalo waandishi wa magazeti ya Serikali walisema limefanya kisisa.
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
bora sisi tunaoabudu kwenye mapango, t-shirt za njano na kijani hazifiki ila mbuzi na kondoo tu, aulabda kuku!
 

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Sep 15, 2008
235
500
Can. 1364(1):

An apostate from the faith, a heretic or a schismatic incurs a latae sententiae excommunication, without prejudice to the provision of Can. 194 §1, n. 2; a cleric, moreover, may be punished with the penalties mentioned in Can. 1336 §1, nn. 1, 2 and 3.
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
Serikali inatilia mkazo kila siku kutoshabikia mambo ya udini, lakini nimeshangaa sana jinsi gazeti la Serikali la Habari leo lilivyokuwa linaandika kila kukicha habari hiyo na magazeti mengine kwa busara kutochafulia wino kwenye magazeti yao kuhusu jambo hilo. Yangefanya hivyo magazeti ya kawaida mengine kinyume cha matakwa ya serikali yangetishiwa kufungiwa, lakini serikali wala haikutamka cho chote juu ya uchochezi huo wa gazeti la serikali kuhusu habari hiyo. Jamani tunaenda wapi sasa?
 

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,404
2,000
Kwa wale wanaotaka mahakama ya kadhi mnatakiwa kicopy na kupaste utaratibu huu wa wakatoliki bila kuomba ruzuku ya serikali
 

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
1,250
Tunashukuru kwa ufafanuzi huu maana serikali kupitia gazeti lake ilijaribu kupotosha ukweli ili ionekane jamaa wametengwa kwa u ccm wao kitu ambacho si cha kweli.
 

leseiyo

Senior Member
Oct 25, 2007
116
0
Kwa mara ya kwanza habari hii iliripotiwa kwa kupotoshwa na Gazeti la Serikali asorry CCM la Habari Leo na lilidai kwamba, waumini hao walitengwa kwa sababu ya kuiunga mkono CCM.Najiuliza hivi gazeti hili lililenga nini?Ni hali ya hatari kuwa na gazeti la serikali lenye kuchochea uvunjifu wa amani na mgawanyiko miongoni mwa wanajamii.
 

BURAKEYE

Member
Dec 17, 2010
22
0
Poor beleiver,opt to other religions there is no such thing as going beyond GOD but beyond CHURCH PRINCIPALS and as said beyond TRINITY, Remember no where in the bible does the world TRINITY exist because THE WHOLE IDEA IS FABRICATION. The DOGMA of which can not be explain by the bishops themselves.
 

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,383
1,500
Ama kweli ukistaajabu ya Slaa utayakuta ya Kanisa.

umeona ehe? Sasa kaka dsm,si uwaambie wenzio wawe na mahakama kama izi? Haziitaji bajeti ya serikali kama mahakama ya Kadhi inavolazimisha. Pia mwambie mwandishi wenu Petty Siame aache kuandika unafiki. Waende kwa mbunge ndo wawe na dini walioitaka sasa. "ROMA LOUCUTA" means "rome is an end/everything no one else"
 

Afrika Furaha

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
329
0
Poor beleiver,opt to other religions there is no such thing as going beyond GOD but beyond CHURCH PRINCIPALS and as said beyond TRINITY, Remember no where in the bible does the world TRINITY exist because THE WHOLE IDEA IS FABRICATION. The DOGMA of which can not be explain by the bishops themselves.

Ptuuuuuuuuuuu! Uharo mtupu!
 

BURAKEYE

Member
Dec 17, 2010
22
0
i repeat no where in the bible does the word TRINITY EXIST, It is bitter truth but u should swallow
 

Babuyao

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
1,736
1,500
umeona ehe? Sasa kaka dsm,si uwaambie wenzio wawe na mahakama kama izi? Haziitaji bajeti ya serikali kama mahakama ya Kadhi inavolazimisha. Pia mwambie mwandishi wenu Petty Siame aache kuandika unafiki. Waende kwa mbunge ndo wawe na dini walioitaka sasa. "ROMA LOUCUTA" means "rome is an end/everything no one else"

Msemo huo unasema "Roma locuta causa finita" - yaani 'Roma ikishatamka mambo yamekwisha'! Hakuna zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom