Kanisa Katoliki lagoma kumzika bilionea wa Ngurudoto

Aaahn unaona sasa Kama ishu ni kufunga ndoa haya niambie ni wangapi wamefunga ndoa halafu wanamichepuko chungu nzima? Na kufanya Zambi nyingine nyingi Kama vile Wizi, kusema uongo, wivu, fitna, ushirikina n.k? Hao wanatishi bila ndoa wapendeni, waombeeni, wafundisheni Neno wapate kufahamu ipasavyo na siyo kuwahukumu! hiyo inaonesha namna gani mko mwilini zaidi!
Ndoa ni sakramenti, wizi, uzinzi na mengineyo ni dhambi. Kanisa linamtambua muumini kwa sakramenti anazopaswa kuwa nazo, na si kwa dhambi alizonazo. Si ndoa tu, hata angekuwa ni kijana mdogo wa sekondari amekufa bila sakramenti ya ubatizo, asingezikwa kwa imani ya Kanisa Katoliki. Kwa ufupi, kanisa Katoliki linawatambua waumini wake kwa sakramenti zao (rejea mgogoro wa sensa uliohusisha idadi ya wakatoliki nchini - hawa walihesabiwa kwa kutambuliwa through status yao ya ubatizo ambayo ndio sakramenti ya awali kabisa kumtambulisha Mkatoliki). Kama makanisa mengine yanawatambua waumini wao kwa kupitia mahudhurio ya kanisani, huo ni utaratibu wao, lakini imani ya Kanisa Katoliki inamtambua Mkatoliki pale anapobatizwa, na akifikia umri wa kuishi na mwenza wake basi awe ameshapata kipaimara kisha afunge ndoa. Usichanganye dhambi na sakramenti. Mtu anaweza akawa hatendi dhambi lakini kama hajabatizwa huyo si Mkatoliki
 
Hayo mashariti wakati mimi nakua hayakuwepo, je Kijana ambaye hajaoa inakuwaje, siku hizi hata kama huudhurii kwenye jumuiya ukifa hawakuombei, wanasema hakuwa anahudhuria kwenye jumuiya, huko kwenye jumuiya michango kila leo, siku hizi dini ni biashara
Sasa wewe hutaki kutoa michango halafu unataka ukifa padre aje kuongoza ibada, mafuta ya kuweka kwenye gari ayatoe wapi? Mbona bili kwa mama choma unalipa bila manung'uniko? au utafurahi siku moja padre anakuja kuombea mgonjwa nyumbani kwako anatembea kwa mguu huku kabeba vifaa mkononi?
 
HAPA NAONA VIONGOZI WETU WA DINI WANAENDA KINYUME KABISA . MEREMA KESHAFARIKI KITAMBO AKIWA AFRIKA KUSINI . HATIMA YA ANAKOENDA NA KAMA KABLA YA KUFA ALIONGEA NINI NA MUNGU WAKE AU ALITUBU NI SIRI YAKE NA MUNGU . MREMA HAYUPO TENA KAACHA MWILI MNAGOMEA KUUZIKA . WATU WA AJABU SANA


Hawezi kutoa Pesa tena maana ni marehemu tayari; unadhania anaonekana kuwa wa faida tena kwenye dhehebu??

Dini hizi ni wanafiki sana.

Very pathetic kabisa.
 
Kwa ninavyojua mpaka kanisa kufikia kukutenga basi wewe ni tatizo maana kabla ya kukutenga viongozi mbalimbali wa jumuiya na katekista watakuwa wameenda kumsihi ajumuike na waumini wengine akakataa, sisi tulikuwa na muumini mwenzetu alikuwa haji jumuiya wala kanisani, lakini tulijitahidi kuwasiliana nae akakataa ikabidi mwenyekiti akatoe taarifa kanisani na tulimfata na yeye kama jumuiya na kumuambia uamuzi wa kumtenga rasmi, baadae akabadilika na siku hizi anatuzidi wakongwe kwa mahudhurio


Mnamwitaje Mkatoliki

hana kipaimara
hana ndoa
hashiriki Jumuiya

so yeye alikuwa na imani yake kama yeye msimuhukumu
 
Kanisa kama linafundisha kulipiza kisasi...waumini wake watakuwaje? Biblia inasema samehe saba mara sabini...no wonder siku hizi tunawatu wengi wanajifanya wanasali sana na wengine wanaomba tuwaombee lakini deep down wamejaa visasi na roho mbaya. Tumtumikie Mungu na Sio Makanisa Period!
 
Yah sina hakika kwa sababu tatizo kuu alikuwa kafir, sasa kwa mujibu wa dini ya haki ukifa kafir ni finari.
Afadhali umekiri kuwa hauna uhakika na unachochangia, so it's better you stay aside uwaachie wenye uhakika
 
Mkuu mimi ni mkatoliki na nimelelewa katika maadili ya kikatoliki lakini siku hizi mambo yamebadilika sana, enzi zetu sisi wakati tunakua haya mambo ya jumuiya na michango ya kila leo hayakuwepo
Hayakuwepo sababu kuna watu(wafadhili) walikuwa wanatoa sasa wale wazungu wamekata/wamepunguza ile misaada ndo mana tunaanza kuminyana wenyewe, sasa kwakuwa tulizoea vya bure, kanisa linajengwa mtu hutoi hata Mia, Leo ukiambiwa uchangie ndio unaanza kuona unaibiwa
 
View attachment 561914

KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limekataa kuendesha misa ya maziko ya mfanyabiashara bilionea Faustine Mrema kwa madai hakuwa na Sakramenti ya ndoa na mke wake wala kipaimara.

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu, Jimbo Kuu la Arusha Padri Festus Mangwangi amekiri suala hilo na kuongeza kuwa marehemu enzi za uhai wake hakuweka heshima na kanisa.

“Marehemu ni mkatoliki wa kuzaliwa, lakini hakuwahi kuwa na sakramenti ya ndoa na mke aliyezaa naye watoto wala kupata Kipaimara. Kanisa haliwezi kumzika kabisa, kawaida mazishi ya Kanisa Katoliki ni heshima inayotolewa kwa mhusika kama anastahili.

“Huyu hakuwahi kufunga ndoa kanisani, alijitenga na kanisa kwa hiyo kusema tumemtenga si kweli, yeye ndiyo alijikataa hakutaka kutafuta heshima yake na kanisa akiwa hai,” alisema Padri Mangwangi.

Kuhusu kutokwenda kwenye Misa za Jumuiya ambayo nayo ni moja ya taratibu muhimu inayowataka waumini wa kikatoliki kushiriki ibada za nyumba kwa nyumba Padri Mangwangi amesema, hata ibada hizo nazo pia marehemu alikuwa hashiriki.

“Jumuiya ni utaratibu wa kanisa unaowataka waumini wawe na ushirika wa karibu ikiwamo kufahamiana marehemu pia alikuwa hashiriki kabisa sasa unaanzaje kumzika mtu kwa heshima za Kanisa Katoliki?” amehoji Padri Mangwangi.

Wakati Kanisa hilo likijivua kushiriki Misa ya heshima ya maziko ya marehemu Mrema hiyo jana, Askofu Dk. Eliud Issangya wa Kanisa la Kimataifa la Kiinjili, alilazimika kuongoza Ibada hiyo ya maziko iliyofanyika Hoteli ya Ngurdoto, wilayani Arumeru.

Chanzo: Mtanzania
wafu hawajui neno lolote,hao wakatoliki hawajui walitendalo kwanza hakuna misa ya wafu,hatawangemfanyia ibada haitadadilisha chochote kwa historia ya marehemu kiimani kufuatanana na mafundisho ya Biblia takatifu.waache unafiki
 
wafu hawajui neno lolote,hao wakatoliki hawajui walitendalo kwanza hakuna misa ya wafu,hatawangemfanyia ibada haitadadilisha chochote kwa historia ya marehemu kiimani kufuatanana na mafundisho ya Biblia takatifu.waache unafiki
Sasa Kama hakuna misa ya wafu mbona mkiikosa mnahangaika na kuleta kashfa
 
Kanisani alifunga ndoa na mmoja ndiye kanisa linamtambua. Huyo mwingine wakwake
Utetezi dhaifu sana ! Kwani kanisa linaruhusu kufungisha ndoa mbili kwa mtu mmoja , mmeamua kuwatenga watenda dhambi basi watengeni wote .
 
Sasa Kama hakuna misa ya wafu mbona mkiikosa mnahangaika na kuleta kashfa
labda familia yako siyo wote.hao RC si wamewaaminisha watu kwamba kuna adhabu ya dhambi ndogo na dhambi kubwa eti mateso duniani au toharani ndo maana watu wanachanganyikiwa ili wapate hiyo misa tena misa yenyewe mpaka utoe hela kwanza (sadaka) ndo waendeshe hiyo ibada.waache unafiki
 
Mmmh tunaanza kuhukumu ...the..bible says " usihukumu usije ukahukumiwa" ...... ..... Hauwezi ukajua kila muumini ana imani gani ndani yake hata kama anahudhuria kanisani _____ wengine ni sawa na vichwa vilivyo baki tu Ila kiwiliwili kwa Shetani .....


NB.. Usihukumu usije ukahukumiwa ..... Biblia imetuwekea mitego mingi ndg zangu ..
N:B hapo haukumu ,hapo anatimiza taratibu za kanisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee sikuwahi kufahamu kama ni mkatoliki hadi leo kwenye thread hii...ni kweli yeye ndiye aliyelitenga kanisa...Nadhani Jumuiya yake ni ile ya mitaa ya Ikulu ndogo pale Arusha.


Umeona eee na hakuwahi hata kupata kipaimara that means alikuwa na imani yake anayoijua yeye! all in all RIP
 
*_Anaandika Bernard Mukasa_*

UFAFANUZI KUHUSU KANISA KATOLIKI KUTOKUWAFANYIA MAZIKO YA KIKANISA BAADHI YA WAAMINI WAKE:

Jana mitandao ya kijamii nchini ilienea habari za kanisa kutokumzika tajiri mmoja kwa sababu alikufa katika hali ya "kinyumba" bila ndoa takatifu, na kwamba hakuwa mshiriki hai wa masuala ya kanisa.

Baada ya hapo kukatokea maneno mengi sana baadhi ya watu wakilishanbulia kanisa katoliki kwamba limekosea na linakosea kwa utaratibu huo, kwa maelezo mepesi kwamba suala la mtu kwenda mbinguni ni wajibu wa Mungu na siyo kazi ya kanisa kuhukumu (huenda wamesahau kwamba kanisa halijaihukumu roho ya marehemu bali limekataa kuuzika mwili wake tu ardhini).

Basi nimewiwa kufafanua kidogo niwezavyo kuhusu suala hili.

Karibu.......

Maziko ya kikanisa hayamfanyi mmoja aliyefariki aende mbinguni wala Jehanamu, bali yanamkumbusha mwombolezaji aliyebaki hai wajibu wake wa kuishi katika ushirika na kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kumzika au kutokumzika mtu kikanisa siyo jambo la kubeza ingawa ni kweli siyo linalompeleka marehemu mbinguni au motoni. Tukumbuke mwili wa marehemu unabaki ardhini. Kinachoenda mbinguni au motoni ni roho.

Lakini maziko ya kikanisa ni jambo lenye maana kubwa kutukumbusha tunaobaki duniani kwamba Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na ambalo Kristo mwenyewe ndiye kichwa chake *(Waefeso 5:23)* linataka waamini tuige mfano wa mwenzetu aliyeishi na kumaliza maisha yake akiwa na ushirika na kanisa, ndiyo maana linafanya maziko ya kikanisa kama sherehe ya kumpongeza, kumuaga na kutuonesha mfano wake ili tuufuate. Na kama ameishi na kumaliza maisha yake bila shirika kamili na Kristo kwa njia ya kanisa ambalo ni mwili wa huyo Kristo, kanisa linakataa kumzika ili kutuambia kwamba mfano wake siyo ufaao kuigwa.

*Kwa nini ni muhimu Mkristo ashiriki maisha ya kanisa badala ya kuishi kivyakevyake tu?*

Kwa sababu Kristo alitaka hivyo. Wakati anawaaga mitume wake na wanafunzi wake aliwataka WABAKI KATIKA UMOJA, NA WAKAE HIVYO HATA ROHO MTAKATIFU MZINDUZI RASMI WA KANISA AKIJA AWAKUTE WAKIWA PAMOJA NA WAMOJA.

Tutakumbuka hata sala ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatiwa mikononi mwa wauaji aliwaombea wanafunzi wake WABAKI WAMOJA kama yeye na Baba walivyo MMOJA *(Yohane 17:11)*.

Hivyo maisha ya ukristo ya kivyakovyako kwa kujitenga na kanisa Siyo mpango wa Kristo bali mpango wako binafsi. Siyo mfano tunaopaswa kuuiga wala kuuendekeza.

Kungia mbinguni kuurithi uzima wa milele kunamdai mtu atimize masharti makuu mawili (Luka 10:25-28):

1. Mapendo kwa Mungu
2. Mapendo kwa jirani.

Lakini huwezi kumpenda Mungu nusunusu. Yaani ukampenda kichwa na ukamchukia mwili. Kama kanisa ni mwili wa Kristo, wawezaje kusema unampenda Yesu (Mungu nafsi ya pili) na bado huna muda na mwili wake yaani kanisa lake? Mnafiki wewe.....!

Na kama hukumpenda Mungu (kichwa na mwili) na hukumpenda jirani, utawezaje kuurithi uzima wa milele? Ni vigumu.

Ni vema kujitahidi kuiepuka njia hiyo, ndiyo maana kanisa linautumia msiba kutukumbusha njia njema na kutuonya juu ya njia isiyo njema.

Kumbuka Yesu alisema atakayemkiri yeye Yesu (ambaye kanisa ni mwili wake) mbele za watu, Yesu pia atamkiri mbele ya baba, na atakayemkana Yesu mbele za watu Yesu pia atamkana yeye mbele ya Baba yake wa Mbinguni atakapofika mbele ya kiti cha utukufu wa Mungu (Mathayo 10:32-33).


*Mfano wa taratibu za ki-kanisa ambazo ukijitenga nazo siyo rahisi kuupata uzima wa milele ni huu:*

Ukiuishi ukristo wako peke yako nyumbani mwako huna nafasi ya kushiriki EKARISTI TAKATIFU au kwa maneno mengine KOMUNYO au wengine wanaita CHAKULA CHA BWANA au wengine wanaita MKATE WA BWANA.

Lakini Yesu mwenyewe alisema:

" *Kweli nawaambieni,* Msipokula huu mwili wangu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho"

*Yohane 6:53-54*

Zingatia vizuri hayo maneno ya mwanzo niliyoya-bold. Yesu anaanza kwa kusisitiza akisema *"Kweli nawaambieni,..*

Kwa nini Yesu alisisitiza?

Kwa sababu alijua kuna wengi watapuuzia suala la kukomunika (kushiriki chakula cha Bwana) wakidhani watakuwa na uzima wa milele kwa kuishi tu majumbani kwao bila kuja kanisani ambako ndiko chakula hicho hutolewa, wakijidanganya kwamba maadam waliishabatizwa (na wengine walibatizwa kwa maji mengi ya mto wote au bahari nzima) basi hiyo inatosha kwa wao kuurithi uzima wa milele.

Pia alijua wapo ambao wanaweza kuwa wanasali na kutoa sadaka kubwakubwa lakini wanaishi maisha yanayowafanya wasistahili kushiriki chakula cha Bwana, wakidhani ni rahisi kuupata uzima wa milele bila chakula hicho.

By the way..., hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa neema (Waefeso 5:2).

Neema ya Mungu (yaani uwepo wa Yesu Kristo katika maisha na mazingira ya mwanadamu) haipatikani katika kujitenga wewe binafsi, bali inapatikana kwa kuungana na wenzako kwa jina la Yesu.

Yeye mwenyewe alisema:

"Wakutanikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao"

Mathayo. 18:20.

Na kama Yesu yupo katikati ya walio na umoja/ushirika katika yeye, basi neema ya Mungu inapatikana katika ushirika huo na siyo katika ubinafsi na kujitenga. Na kwa kuwa tunaokolewa kwa neema, ni rahisi zaidi kuokolewa tukiwa ndani ya kanisa kuliko kuokolewa tukiwa tumejitenga na mambo ya kanisa.

Kwa hiyo ndugu yangu..., ni muhimu sana kushiriki mambo ya kanisa. Na ni muhimu sana kwa kanisa kuonesha shukrani nanpongezi (appreciation) kwa yule anayekufa katika ushirika na kanisa, na kuonesha kuhuzunishwa na yule anayekufa akiwa hana shirika na kanisa.

Neno la Mungu linasema "Heri watu ambao wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naam, watapumzika kutoka katika taabu zao, maana matunda ya jasho lao yatawafuata" (Ufunuo 14:13).

Mstari huo wa mwisho kunukuu ni muhimu sana kwako ndugu yangu. Kwamba ukifa umetengana na Bwana kwa matendo yoyote ikiwemo kutengana na mwili wa Bwana Yesu (Kanisa lake) una ole. Na ukifa ukiwa umeungana naye kwa matendo yoyote ikiwemo kuungana na mwili wa Bwama Yesu (Kanisa lake) una heri. Na amemalizia kwa kusema "matendo yako yataambatana nawe" hata baada ya kufa. Ndiyo maana umekufa, lakini sifa za jitihada za jasho lako tunazihubiri hata wakati wa mazishi yako. Na kinyume chake, sifa mbaya ulizoacha tunazikana hata baada ya kufa kwako kwa kuyakana mazishi yako.

Tumsifu Yesu Kristo.


Ben Mukasa.
 
Namkumbuka sana mwalimu Nyerere. Alikuwa mkatoliki safi.

"Hakuna dhehebu/dini ambalo halina miiko! Hakuna. Hakuna! Waislamu wana miiko yao, wasabato wana miiko yao, wabudha wana miiko yao. Huwezi kufuata imani fulani bila kujali miiko. Juzi juzi hapa tajiri mmoja hivi hapo Arusha amekufa alikuwa haendi jumuia, wala hapokei sakramenti. Kwa jinsi kanisa katoliki lilivyo serious! Alipokufa bila kupepesa macho walisema tu huyu hatumfanyii ibada ya mazishi! Watu walipoanza kusemasema wala hawakujali. Tajiri mzima .......ooeehhh? Hutaki kujihusisha na usharika? Unataka kuishi kihunihuni tu? Ukitaka kuwa mkatoliki Lazima Ujiheshimu! Kama unataka kuishi kihunihuni nenda huko vichochoroni makanisa yamejaa. Kanisa katoliki ni kanisa takatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app


Aiseeeeeh!
 
Back
Top Bottom