Kanisa Katoliki lagoma kumzika bilionea wa Ngurudoto

Na huwezi kuwa muumini wa Katoriki bila ya kutoa michango, husipotoa pia unaonekana unafanya makusudi na unatengwa... Hizi dini ni biashara kabisa
Acha uongo wa kupotosha watu.Hakuna huo utaratibu wa kulazimishwa kutoa michango ndani ya kanisa wala si kweli kwamba usipotoa inaonekana unafanya makusudi.Sisi ndio waumini na ndio tunaoujua ukweli.Usifananishe Ukatoliki na madhehebu mengine binafsi ya kibiashara
 
Mim pia ni muumini, kuna muda inaniradhimu mpaka niikope biashara yangu ilikulipa iyo michango, ukiongezea ya jumuiya huwa mpaka nawaza niishi kipagani
 
Mimi situmii biblia.
wewe ndio inabidi utumie biblia kunipinga kwamba hawatumwi na Mungu
Kumbe hautumii Biblia lakini kwenye point yangu hapo juu ulinipinga kuwa haujaona mahali Mungu amelipa kanisa mamlaka pamoja na kukupa reference.Anyway point yangu ni kwamba hata kama biblia haitamki moja kwa moja lakini lugha inayotumika ni ya wazi kabisa.Anaposema "nimekukabidhi funguo" maana yake nimekupa mamlaka "lolote mtakalolifunga duniani,na mbinguni limefungiwa" maana yake kanisa likisema hapana na mbinguni ni hapana na likisema ndiyo na mbinguni ni ndiyo (kwa jambo lolote).Na ndio maana kanisa lina Sakramenti ya kitubio/maungamo.

"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni"

Petro ndiye aliyekabidhiwa mamlaka ya kuliongoza kanisa la Kristu na ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo ambalo Kristu mwenyewe alisema atalijenga na kulipa mamlaka hayo na milango ya kuzimu italijaribu lakini haitalishinda kama tunavyoshuhudia!
 
Mim pia ni muumini, kuna muda inaniradhimu mpaka niikope biashara yangu ilikulipa iyo michango, ukiongezea ya jumuiya huwa mpaka nawaza niishi kipagani
Weka ushahidi mkuu wa hayo madeni na michango tujue ni michango ya nini hiyo ambayo unalazimishwa kutoa! Usipende kuongea uongo.Kanisa ni Taasis Rasmi ya MUNGU Viongozi wanapowekwa wakfu wanapewa kazi ya Kuchunga au utume lakini Mungu ndio kiongozi Mkuu.Tuwe makini tusiingize siasa au ushabiki sababu Mungu toka Karne awezi akaangalia Kanisa likichafuliwa au kufarakanishwa. USIJITAFUTIE LAANA AU MAPIGO KWA MUNGU kuna mada nyingi za kujadili lakini EPUSHA ULIMI WAKO. Kanisa likiaibishwa sio ASKOFU,PADRE au MCHUNGAJI anayeaibika bali ni MUNGU mwenyewe. usiwe sehemu ya kumwangusha Aliye Juu.
 
Mim pia ni muumini, kuna muda inaniradhimu mpaka niikope biashara yangu ilikulipa iyo michango, ukiongezea ya jumuiya huwa mpaka nawaza niishi kipagani
Acha uongo wewe, Kanisa huwa halidai mtu michango hadi kuwa deni, labda kama umechanganya ulikopa kwa mtu binafsi
 
Acha uongo wewe, Kanisa huwa halidai mtu michango hadi kuwa deni, labda kama umechanganya ulikopa kwa mtu binafsi
Inaonekana ni mnufaika wa mfumo, sipo kwaajiri ya kubishana wala kumshawishi mtu. ELENDELEA KUNUFAIKA
 
Weka ushahidi mkuu wa hayo madeni na michango tujue ni michango ya nini hiyo ambayo unalazimishwa kutoa! Usipende kuongea uongo.Kanisa ni Taasis Rasmi ya MUNGU Viongozi wanapowekwa wakfu wanapewa kazi ya Kuchunga au utume lakini Mungu ndio kiongozi Mkuu.Tuwe makini tusiingize siasa au ushabiki sababu Mungu toka Karne awezi akaangalia Kanisa likichafuliwa au kufarakanishwa. USIJITAFUTIE LAANA AU MAPIGO KWA MUNGU kuna mada nyingi za kujadili lakini EPUSHA ULIMI WAKO. Kanisa likiaibishwa sio ASKOFU,PADRE au MCHUNGAJI anayeaibika bali ni MUNGU mwenyewe. usiwe sehemu ya kumwangusha Aliye Juu.
Hata mim ningeamua kuwaza kiimani kabla ya kureply uzi huu basi ningekuwa na mtazamo kama wako.. Tufanye nimekosea kuelezea hili swala hapa.
 
Kumbe hautumii Biblia lakini kwenye point yangu hapo juu ulinipinga kuwa haujaona mahali Mungu amelipa kanisa mamlaka pamoja na kukupa reference.Anyway point yangu ni kwamba hata kama biblia haitamki moja kwa moja lakini lugha inayotumika ni ya wazi kabisa.Anaposema "nimekukabidhi funguo" maana yake nimekupa mamlaka "lolote mtakalolifunga duniani,na mbinguni limefungiwa" maana yake kanisa likisema hapana na mbinguni ni hapana na likisema ndiyo na mbinguni ni ndiyo (kwa jambo lolote).Na ndio maana kanisa lina Sakramenti ya kitubio/maungamo.

"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni"

Petro ndiye aliyekabidhiwa mamlaka ya kuliongoza kanisa la Kristu na ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo ambalo Kristu mwenyewe alisema atalijenga na kulipa mamlaka hayo na milango ya kuzimu italijaribu lakini haitalishinda kama tunavyoshuhudia!
kwa hiyo wewe ndio petro?
 
Acha kunukuu na kutafsiri vibaya maandiko ya Mungu
Mmmh tunaanza kuhukumu ...the..bible says " usihukumu usije ukahukumiwa" ...... ..... Hauwezi ukajua kila muumini ana imani gani ndani yake hata kama anahudhuria kanisani _____ wengine ni sawa na vichwa vilivyo baki tu Ila kiwiliwili kwa Shetani .....

NB.. Usihukumu usije ukahukumiwa ..... Biblia imetuwekea mitego mingi ndg zangu ..
 
Kwani hiyo dini yenu ni mali binafsi ya mtu?
Sio mali ya uma ni utaratibu waliojiwekea na kujiunga hulazimishwi..ukiona hufurahii taratibu zao unahamia kwingine au unaanzisha kanisa lako na hakuna atakae kuuliza.
 
Ukristo ni pale unapo batizwa. Hizi sakramenti nyingine zinaumuhimu kadiri ya hatua.

Nashangaa sana wanaowahukumu kwa hizo nyingine..maana hajaukana ubatizo wake.

Makaasisi wawe wanatimiza wajibu wao kwa wakristo wa namna hii..lakini pia waendelee kuwatia moyo wenginr kukamilisha hzo sajramenti nyingine.
Binafsi nilishaacha kwenda church..nikifa wasiponizika ni sawa tu.
Ukijiunga na kikundi flani basi fata taratibu zao kama walivyojiwekea, ukishindwa temana nao.
 
Unasema sio mali ya uma ni utaratibu waliojiwekea wenyewe na kama sitaki nihamie kwingine.
Mbona umerahisisha hivyo yaani kama kuhama kwenye kundi la mziki au timu ya mpira wakati dini ni jambo la milele kama kweli wewe ni muumini wa hiyo dini.
Otherwise labda uniambie dini yenu ni kikundi fulani cha watu kama saccos
Sio mali ya uma ni utaratibu waliojiwekea na kujiunga hulazimishwi..ukiona hufurahii taratibu zao unahamia kwingine au unaanzisha kanisa lako na hakuna atakae kuuliza.
 
Kanisa limepewa mamlaka ya kuhukumu
Dhehebu la Katoliki ni la ajabu sana.Sijui wanashindwaje kuona kwamba maombi,however you may pray,hayamsaidii mtu aliyekufa.Prayers kwenye msiba ni kwa ajili ya waliobaki,sio aliyekufa.Kama yeye mwenyewe alishindwa kutengeneza maisha yake na Mungu,no body can help him.Uongozi wa Katoliki uache kudanganya waumini wao.

Imani za Katoliki ni so unbiblical,ndio maana nimeliita "dhehebu." Kanisa ni people who truly believe in Jesus Christ,Catholics don't,they believe in doctrines coined by the Catholic drnomination au kama unataka mapokeo.
 
Unasema sio mali ya uma ni utaratibu waliojiwekea wenyewe na kama sitaki nihamie kwingine.
Mbona umerahisisha hivyo yaani kama kuhama kwenye kundi la mziki au timu ya mpira wakati dini ni jambo la milele kama kweli wewe ni muumini wa hiyo dini.
Otherwise labda uniambie dini yenu ni kikundi fulani cha watu kama saccos
Siamini katika dini yoyote, naona maluweluwe tu.
 
Dhehebu la Katoliki ni la ajabu sana.Sijui wanashindwaje kuona kwamba maombi,however you may pray,hayamsaidii mtu aliyekufa.Prayers kwenye msiba ni kwa ajili ya waliobaki,sio aliyekufa.Kama yeye mwenyewe alishindwa kutengeneza maisha yake na Mungu,no body can help him.Uongozi wa Katoliki uache kudanganya waumini wao.

Imani za Katoliki ni so unbiblical,ndio maana nimeliita "dhehebu." Kanisa ni people who truly believe in Jesus Christ,Catholics don't,they believe in doctrines coined by the Catholic drnomination au kama unataka mapokeo.
Kwanza kabisa nakukumbusha Katoliki sio dhehebu.Kanisa mwanzo lilikuwa moja na wengine walimeguka toka tulipo na kuanzisha madhehebu. Ni kama Chuo Kikuu cha Dar zamani kilijumuisha Sokoine, Ardhi na Muhimbili. Sasa baadaye hivi vimekuwa vyuo vinavyojitegemea lakini katika kuwa vyuo vinaondoka na baadhi ya vitengo tu na kuacha vingine, mfano Muhimbili wana medicine tu, Ardhi wana land tu, Sokoine wana agriculture tu, ukitaka vyote pamoja waweza kuvipata tu katika kilicho chuo kikuu cha Dar. Ni mfano ulio na madhaifu lakini nadhani unaweza kufundisha kidogo. Hivyo Sokoine kuuliza kwa nini chuo kikuu cha Dar wana kitengo cha sheria, jibu ni kuwa wewe umeachaje kutokuwa na sheria. Yaani wao wa madhehebu wangekuwa na mantiki kuuliza tunachofanya sisi kama tungekianzisha baada ya wao kuondoka, au tungekuwa tumeanza pamoja, lakini wao wameanza baadaye, miaka mingi baada ya mitume. Yaani madhehebu yote yaliyopo leo hakuna ambalo lilianzishwa wakati mitume wakiwa hai. Kanisa pekee waliloacha mitume ndilo tulilonalo sisi, na ndiyo maana ya Kanisa KATOLIKI (universal) na la MITUME. Kuwa lilianza na mitume na ndilo pekee waliloacha. Wengine wakajimega toka hapa na kuanzisha madhehebu, hivyo madhehebu yale hayakuanza na mitume, ila imani waliyonayo imeanza na mitume. Kanisa pekee lililoanzishwa na mitume ndilo hili tulilonalo. Madhehebu mengine yote ya ukristo yameanzia kwa imani ya mitume lakini hayakuanzishwa na mitume. Hii ndiyo tofauti yetu kubwa. Ndiyo maana huwezi kusema letu ni dhehebu, sababu hili likiwa dhehebu tunakosa dini iitwayo ukristo. Tutajiuliza sasa dini iitwayo ukristo ni ipi? Maana mpaka Yesu anakufa hakukuwa na ukristo. Ukristo umeanza na mitume. Na mitume na waliacha kanisa moja na siyo madhehebu. Sasa yule aliyeachwa na mitume na aliyemwachia na wakaachiana mpaka tulipo alibaki hakutoka kwenda kuanzisha dhehebu, ndiyo maana tunasema ule kila walichoacha kipo tulipo sisi na si huko nje.

Maana yake ni kuwa ukitaka tafsiri ya uhakika ya maandiko kadiri walivyoelezwa mitume na Yesu huwezi kuipata nje, maana wenye hiyo tafsiri kama ilivyoelezwa na mitume na waandishi wa maandiko hawakutoka, walibaki na kufundisha walio ndani. Nje waliacha kutafuta tafsiri kadiri walivyoelewa wao na siyo kadiri ya maelezo ya mitume. Kuna tofauti kubwa kati ya kujisomea kitabu cha sayansi kilichoandikwa na Copleston, na kufundishwa sayansi na Copleston, aliyeandika kitabu cha sayansi. Bila shaka aliyefundishwa ataelewa zaidi kuliko asiye na mwalimu anayetegemea tu kujua kwake kusoma. Nimetoa mfano huu mara kadhaa, kuwa kujua kusoma haitakufanya ujue kuwa H2O ni alama ya maji, kama huna mwalimu wa kukuelekeza. Kujua kusoma kutakufanya useme Hechi Two Ooh badala ya water. Na shida hii tunaipata kwa mfano kwa waitwao YEHOVA WITNESS. Wanasema jina la Mungu ni Yehova, lakini ukweli ni kuwa walishindwa kujua kuwa Wayahudi waliandika jina la Mungu kama YHWH bila silabi kwa sababu ilikuwa marufuku kutamka jina la Mungu, hivyo kwa kuandika hivyo iliwasaidia hata waliosoma wasiweze kutamka. lakini neno halisi ya YHWH ni YAHWEH. Wao sababu hawana elimu hiyo wakasoma kama Yehova na kwa vile W ya Wayahudi ilikaa kama V ndo ikawa kabisa wamehalalisha. Ndugu zangu, Yesu alikaa na wanafunzi miaka mitatu akiwafundisha. Paulo alikaa na mitume kwa muda mrefu tu kabla hajaanza kuhubiri. Hii inatuambia nini? Inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi baada ya watu kujifunza na siyo kabla. Yesu hakushindwa kuwapa mitume Roho Mtakatifu na wawe na elimu yote, lakini aliwapa Roho Mtakatifu baada ya kuwafundisha kwa miaka mitatu. Nasi basi tujifunze kwanza, ndipo tumuite Roho Mtakatifu. Kinyume cha hapo huyo si Roho Mtakatifu. Ili mwalimu akufundishe formula ile ya H2O yabidi uwe kwanza na basics za syllaby, consonants, na numbers. Ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi. Ama sivyo tuache hata kujifunza kusoma na kuandika tukae nyumbani tumuombe Roho Mtakatifu atupulizie kujua kusoma na kuandika. Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa namna hiyo. Na zaidi tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia wengine pia. Roho Mtakatifu anaweza mtumia jirani yako pia kukufundisha wewe anachotaka ukijue. Miujiza ya kazi za Roho Mtakatifu hutokea kila siku katika maisha yetu, hata katika mambo yale tuyaonayo kuwa ni ya kawaida sana kwetu. Yatubidi tu kufungua macho yetu ya imani kuyaona.
 
Dini hizo za kuletwa,wenyewe sio mungu halafu wanamuhukumu.
Nyie mzikeni,mengine atajuana na mungu,ndio maana nawapenda Sana waislamu,mtu hata asiende msikitini Maisha yake yoote,ili mradi ni muislamu,siku akifariki,Basi mashehe watamzika tu,mengine wanamuachia mungu ndiye atakua amfanye Nini marehemu
 
Back
Top Bottom