Kanisa Katoliki lagoma kumzika bilionea wa Ngurudoto

stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
585
1,000
Nikizikwa na kanisa hiyo heshima naipeleka wapi? Inanisaidia nini? kama naenda motoni itanipeleka mbinguni? Na ambao hawazikwi na kanisa hawana heshima?
Sidhani kama mizinga ya jeshi rais anapoapishwa au anapozikwa askari ina umuhimu wowote juu ya muhusika kwakuwa haibadilishi chochote ila ni ishara ya heshima tu na kuwakumbusha wengine kuishi maisha ya kutenda wema kwa watu wote.Narudia kusistiza kuwa sidhani kama ungependa mwili wako au wa ndugu yako utupwe tu msituni.Kumbuka hata wana wa Israeli walihifadhi mifupa ya mababu zao na kuitunza kila walipokwenda.
 
Waaai

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,196
2,000
Sidhani kama mizinga ya jeshi rais anapoapishwa au anapozikwa askari ina umuhimu wowote juu ya muhusika kwakuwa haibadilishi chochote ila ni ishara ya heshima tu na kuwakumbusha wengine kuishi maisha ya kutenda wema kwa watu wote.Sidhani kama ukifa utapenda mwili wako utupwe tu msituni.
YESU alikufa kifo cha heshima kwa binadamu au cha aibu? Aina yake ya kifo imeathiri vipi heshima yako kwake na kwann?
 
BILLY ISISWE

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,334
2,000
Makanisa ya zamani yaliyotokana na kuhasi. Sheria ni kama za wakatoliki. Sii kama walokole.
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,488
2,000
Ukiona hivyo ujuwe alikuwa hatoi michango mikubwa kwenye kanisa, dini imekuwa biashara siku hizi
Mimi sio Mkatoriki but naona kama umetengeneza assumption mwenyewe na ukaitolea jibu hiyo assumptions na ukafanya na judgment kabisa bila kujisumbua kutafuta proves yake! Sorry kwa kuchangia UZI wa miaka 4 iliopita
 
Apr 12, 2017
28
45
Mmmh tunaanza kuhukumu ...the..bible says " usihukumu usije ukahukumiwa" ...... ..... Hauwezi ukajua kila muumini ana imani gani ndani yake hata kama anahudhuria kanisani _____ wengine ni sawa na vichwa vilivyo baki tu Ila kiwiliwili kwa Shetani .....

NB.. Usihukumu usije ukahukumiwa ..... Biblia imetuwekea mitego mingi ndg zangu ..
Mkuu si hukumu,hayo ni maamuzi ya kanisa,hakuna hukumu hapo ni kanisa kama kanisa limeona hastahili kupata huduma ambayo wakati akiwa hai hakuithamini.
 
stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
585
1,000
Hata madictator hupigiwa mizinga lakini heshima yao halisi kwa jamii ya mtu mmoja mmoja ni tofauti. Marehemu aliyekuchangia figo ukaishi asipozikwa na kanisa sababu paroko kakataa haidhuru heshima uliyo nayo kwake. Haifuti historia yake na umuhimu wake kwenye maisha yako, Kuna mambo mengi sana binadamu tunafanya kama maigizo.

However kupewa heshima na kanisa si jambo baya ni kiashiria kizuri kuwa ulikuwa mtu wa imani sio mpagani, hilo sipingi.
Usilolitambua ni kwamba Kanisa ni sehemu ya jamii.Wewe mtu mmoja uliyesaidiwa figo pia ni sehemu ya jamii na huenda ukawa muumini pia.Matendo yako na maisha yako kiujumla yanapaswa kufuata na kuiishi misingi ya imani katoliki.Kutoa msaada pekee haiwezi kuwa kigezo cha kuwa mfano katika jamii pasipo na kielelezo cha kuishi maisha ya matendo mema na ya mfano kwa jamii.Unaweza kuwa jambazi lakini unatoa misaada.Unaweza kutoa figo lakini ni muuaji au mzinzi.Ndio maana kanisa likaweka vipimo vyake au miongozo ya kuishi imani ya Kristu ambayo ni kama hayo yaliyoelezwa,Kuhudhuria misa takatifu,kuhudhuria jumuiya,kushiriki ekaristi takatifu,Sakramenti ya kitubio,kutembelea wagonjwa n.k
 
Sawa. Kuna swali niliuliza, Kifo cha YESU kilikuwa cha heshima kwa jamii au cha aibu? Kifo chake kimeathiri vipi heshima yake kwako na kwanini?
Mipango ya kanisa ya kutunuku heshima ina maana pale tu mtu anapokuwa na heshima kweli, ila kama ana heshima na kanisa halikuiona hiyo heshima hayo ni maigizo.
 
colony

JF-Expert Member
Jul 17, 2017
259
500
Hajahukumiwa umeambiwa wamekataa kumzika kwa sabab ya taratibu za Mazishi ya kikatoliki...

Hukumu ataenda kuipata aendako, jaribu kuwa muelewa
Mmmh tunaanza kuhukumu ...the..bible says " usihukumu usije ukahukumiwa" ...... ..... Hauwezi ukajua kila muumini ana imani gani ndani yake hata kama anahudhuria kanisani _____ wengine ni sawa na vichwa vilivyo baki tu Ila kiwiliwili kwa Shetani .....

NB.. Usihukumu usije ukahukumiwa ..... Biblia imetuwekea mitego mingi ndg zangu ..
 
stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
585
1,000
YESU alikufa kifo cha heshima kwa binadamu au cha aibu? Aina yake ya kifo imeathiri vipi heshima yako kwake na kwann?
Mkuu naona umeanza kuchanganya files.Kifo cha Yesu ni kusudio maalum kwa mwana wa Mungu.Hapa tunazungumzia kifo kwa muumini au asiye muumini.Ila ukitaka tuzungumzie hilo pia sawa.Kwanza Yesu alizikwa kiheshima mno.Tunaelezwa jinsi matajiri walivyoleta manemane ya thamani na kumwaga juu ya kaburi lake.Sasa sijajua hapo amehusikaje,Ila Yesu alikufa vile ili Leo sisi tuishi vyema na tuzikwe kwa heshima zote na kanisa na jamii kiujumla!
 
Bilionea alivyofariki hapakuwa na matajiri waliofika kwenye mazishi yake? Kifo chake hakikuwa mpango wa MUNGU?

WW NI MFIA VIONGOZI, SI KILA WAKATI VIONGOZI WANAONGOZWA NA ROHO KUFANYA MAAMUZI YA KANISA. NDIO MAANA KUNA NYAKATI KANISA LINABADILI AU KUFUTA SHERIA.
 
stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
585
1,000
Sawa. Kuna swali niliuliza, Kifo cha YESU kilikuwa cha heshima kwa jamii au cha aibu? Kifo chake kimeathiri vipi heshima yake kwako na kwanini?
Mipango ya kanisa ya kutunuku heshima ina maana pale tu mtu anapokuwa na heshima kweli, ila kama ana heshima na kanisa halikuiona hiyo heshima hayo ni maigizo.
Nadhani nimekujibu hapo juu.Alafu hauwezi kuwa mwema na mwenye heshima kwa jamii alafu kanisa lisikuone! Hakuna hicho kitu! Kama muumini wa kawaida kabisa masikini asiyejulikana anazikwa kwa heshima na kanisa wewe ni nani usionekane! Usilolijua ni kwamba unapokuwa muumini mwema wa kawaida kabisa kanisa linakutazama! Huwezi kwenda kupokea ekaristi takatifu ukiwa na dhambi! Lazima ukatubu kwanza.Na usiposhiriki ekaristi takatifu ni dhambi! Sasa niambie hapo unawezaje kuwa nusu nusu!
 
Wanaosema umetenda dhambi ni hao hao binadamu ambao walimuua pia MUNGU. Hao hao pia wanafanya makosa ya hapa na pale. Ni kwann sheria za kanisa huwa zinafika mahala zinabadilishwa? Usiwe mfia viongozi mkuu. Anayetoa taarifa za huyu hafai ni binadamu lolote linaweza kitokea kukawa na taarifa zinazopingana na namna MUNGU anavyomjaj mhusika.
 
stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
585
1,000
Bilionea alivyofariki hapakuwa na matajiri waliofika kwenye mazishi yake? Kifo chake hakikuwa mpango wa MUNGU?

WW NI MFIA VIONGOZI, SI KILA WAKATI VIONGOZI WANAONGOZWA NA ROHO KUFANYA MAAMUZI YA KANISA. NDIO MAANA KUNA NYAKATI KANISA LINABADILI AU KUFUTA SHERIA.
Mkuu kanisa halikuamua kumzika kwa heshima ya kikanisa! Shida iko wapi? Sawa amezikwa na mabilionea nayo ni heshima yake kwa upande mwingine! Lakini kanisa kama kanisa limeamua kutomzika kwa heshima! Kifo ni mpango wa Mungu sawa lakini haibadilishi utaratibu ndani ya kanisa.Alafu usifananishe kabisa na kifo cha Yesu kwakuwa Yesu ndiye mwanzilishi wa kanisa na alizikwa kwa heshima zote na laiti kama kanisa la sasa lingekuwepo wakati huo basi angezikwa kwa heshima zote za kanisa.Viongozi wa kanisa lazima waheshimiwe kwa kuwa wanaongoza kanisa pekee la Kristu.
 
Upo sahihi. Viongozi waheshimiwe ila nao ni binadamu.
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,780
2,000
ndoa yake na dini yenu vina uhusiano gani?ishu ya ndoa ni ishu personal na kuzika ni ibada ya wote inakuwaje mnachanganya hivi vitu viwili?
Kama alifanya dhambi ya kutooa kisheria yeye si ndio atahukumiwa na Mungu nyinyi mnapata hasara gani?
Hapana Mkuu, Kuishi bila ndoa, kutokupewa kipaimara hadi unaingia kaburini ni moja ya uhaini ktk hili dhehebu achilia mbali kuzaliwa mkatoliki. Huku hakunaga ile ya kwamba usipoingia umesimama utaingia umelala, Huku ni kwamba usipoingia ukiwa umesimama basi hata ukiwa umelala huingii.. Tusali jamani hatujui saa yetu lini
 
stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
585
1,000
Wanaosema umetenda dhambi ni hao hao binadamu ambao walimuua pia MUNGU. Hao hao pia wanafanya makosa ya hapa na pale. Ni kwann sheria za kanisa huwa zinafika mahala zinabadilishwa? Usiwe mfia viongozi mkuu. Anayetoa taarifa za huyu hafai ni binadamu lolote linaweza kitokea kukawa na taarifa zinazopingana na namna MUNGU anavyomjaj mhusika.
Hatuwi wafia viongozi mkuu! Bali tunaongozwa na kanisa sio viongozi.Hao viongozi wamewekwa wakfu na kanisa kuongoza kanisa.

Math 16:5
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Kwa hiyo Yesu alikosea kutoa mamlaka hayo kwa kanisa? Kwamba Yesu hakujua hizo doubts unazozisemea za kuwa hawa ni binadamu tu waliomuua msalabani na bado akawapa mamlaka? Usiwe much know mkuu viongozi wanafanya maamuzi kwa kuongozwa na roho mtakatifu na yanapofanyika maamuzi si maamuzi ya viongozi bali ni maamuzi ya kanisa.
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,780
2,000
Sasa kama alifanya kosa la kipaimara si umuachie Mungu wenu atamhukumu huko alikoenda kwa nini mnamhukumu nyinyi ni kama nani mbele za Mungu?
Ushasema kijana ambaye hajaoa unataka nini sasa? Wangapi vijana ambao hawajaoa na wamezikwa kikatoliki?
Hujui ni kosa kuingia kwenye ndoa kabla ya Ubatizo na Kipaimara?

Jumuiya ni ni sehemu ya kuwaweka watu sehemu moja kwenye vigango vyao. Na michango ni ya kawaida sana si kama unavyotaka kuaminisha. Ukweli ukiutenga ukatoliki usilalamike hapo mbeleni.

Binafsi nilisumbuka sana kubatiza mtoto kwasababu sikuwa na Jumuiya, ilinibidi nitoke Dar mpaka Bukoba ambako wazazi wapo na hiyo Jumuiya najulikana ndio nikafanikiwa kubatiza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom