Kanisa Katoliki la Tanzania, kabla halijaporomoka, fanyeni hivi:

Yaani nakushangaa mtoa maada unaangalia uwingi wawaumini kwa Gwajima ndio unapata kujudge kanisa katoriki..Umechelewa sana ...Sisi tunajitambua hatukurupuki..Hatuna viongozi wasiokuwa na Elim na uelewa wakutosha. endelea kuhangaika iposiku utajuatu.
 
Moja kati ya nyuzi za kijinga kuwahi kuziona humu!! Huo utaratibu wa kanisa ni universal we unataka tz ndo wajirekebishe!!??
 
leta ushahidi wa Yesu alipokuwa anakumywa pombe
pia ni wapi Yesu aliruhusu kuabudu miungu ( masanamu ) mnayokuwa mnayaabudu kuyaheshimu kwenye njia ya msalaba, Rejio maria, pia kuomba kwa kupitia jina la maria
badala ya kutumia jina la Yesu ?

Ninyi kiukweli mnamrudisha kristo msalabani awakomboe upya
Nami nilikuwaga na mawazo kama yako
lakini nilipoangalia ushahidi kwenye Biblia nikaona Niko mbali na kristo
maana yeye anasema wekeni uovu wote.

Alhamisi kuu, last supper, unafikiri walikuwa wanakunywa nini? Alichochukua akasema kunyweni hii ndiyo damu yangu unadhani kilikuwa ni kitu gani unadhani ni juice? Anaposema "Yohani mbatizaji alikuja hakula wala hakunywa mkasema amepagawa, mwana wa mtu amekuja anakula na kunywa manasema huyu anakula na kunywa pamoja na wenye dhambi, mkasema ni mlevi na mlafi." Unadhani alichokuwa wanakula na kunywa pamoja na hao wanaoitwa wenye dhambi ilikuwa juice? Tangu lini mtu anayekunywa juice akawa mlevi au akaitwa mlevi? Someni Biblia kwa hekima ya kimungu siyo kwa kuongozwa na mawazo ya waasi wenu waliyojifanya wanajua zaidi wakosa utii wakaanzisha makanisa kidhi mahitaji yao.

Unafahamu maana ya kuabudu sanamu wewe? Unafahamu lejio Maria wewe? Unafahamu maana ya msalaba wewe?

Halafu nawashangaa niyi walokole, Mlishasikia mkatoliki akiwafuatilia kuwauliza kwanini mnafnya hiki au kile kuhusu imani yenu? Si mlisha chagua kujiona kuwa mmeshafika, hamna dhambi? Kwanini mnajishughulisha na sisi wadhambi? Pilipili usiyoila inakuwashaje? Hii ni roho ya ibilisi inawasukuma kumtafutia waamini wengine ili muongezeke idadi. Ongozweni na Roho Mtakatifu ili muijue siri hii ya Mungu.
 
KANISA KATOLIKI TANZANIA.

Kanisa kwasasa liko katika mpito mgumu sana na bado halijagundua, ndani ya Kanisa kumechangamana mambo mengi sana yanayokinzana kifikira. Kanisa linaonekana kutaka kuangushwa kiroho na limekosa mtetezi kiroho, baadhi ya viongozi wamefungwa imani zao na hawaoni ndani tena na wamekuwa vipofu wa roho kabisa.

Mambo ambayo Kanisa linapaswa kuyafanya kwasasa:

1. Kufanya mabadiliko ya Kadinari endapo kama hakutakuwa na mbinu mbadala ya kumjenga upya Kiongozi wetu wa kiroho ili kuendana na mazingira mapya ya kiroho. Msiogope, mpaka sasa tuna Mapapa wawili, anayeongoza Kanisa Papa Fransisko na Papa aliyejiuzuru Papa Benedikto. Hata hili la Makadinari laweza fanyiwa kazi kwa muda.

2. Mapadre na Masista wote waliofanya makosa wakasimamishwa waondolewe vifungo vyao nakufanyiwa Recruitment mpya ya kiroho ili waendelee na kazi ya Mungu. Mnapomfunga Padre au Sista mnafunga Kanisa kiimani.

3. Mapadre walioondoka na kuacha Upadre na kuamua kuoa, warudishwe na kuwafanya kuwa Mapadre Walei huku wakiendelea na familia zao, wakitokea makwao.

4. Mashemasi wote waliokatizwa nakuamua kuoa, wapadrishwe na kuwa Mapadre walei.

5. Mafrateri waliofukuzwa kabla ya Ushemasi warudishwe na kutendewa haki zao

6. Watawa ambao wameanzisha familia wapewe vyeo vya kikanisa ili kulijenga upya kanisa

7.Wote waliowahi kupita seminaries wapewe nafasi ya kuhudumu shule za kanisa maana tayari ni hadhina ya Kanisa.

Nina mengi lakini sio lazima yafanyiwe kazi yote. Nawatakia mfungo Mtakatifu wa Kwarezima.

Ndimi kijana wenu;
Deogratius Nalimi Kisandu
MKOMBOZI WENU.
Mwanza, Tanzania.
Umeoa?
 
Mleta mada ameleta mtazamo wake. Nawe una mtazamo wako. Niwaambie kitu cha kweli kabisa. "Mbinguni hautaenda kwa ukatoliki wako, ama kwa usabato wako, ama kwa ulokole wako. Mbinguni utaenda kwa matendo yako ya kumpendeza MUNGU."
Wapo wanaojiita Wakristu(Yaan wa kristu). Wafuasi wa Kristo. Matendo yao ni kinyaa kitupu......wanafiki wakubwa.

Narudia kwa mwenyekuelewa na aelewe. Dhehebu halikupeleki mbinguni kamwe. Matendo yako!
 
KANISA KATOLIKI TANZANIA.

Kanisa kwasasa liko katika mpito mgumu sana na bado halijagundua, ndani ya Kanisa kumechangamana mambo mengi sana yanayokinzana kifikira. Kanisa linaonekana kutaka kuangushwa kiroho na limekosa mtetezi kiroho, baadhi ya viongozi wamefungwa imani zao na hawaoni ndani tena na wamekuwa vipofu wa roho kabisa.

Mambo ambayo Kanisa linapaswa kuyafanya kwasasa:

1. Kufanya mabadiliko ya Kadinari endapo kama hakutakuwa na mbinu mbadala ya kumjenga upya Kiongozi wetu wa kiroho ili kuendana na mazingira mapya ya kiroho. Msiogope, mpaka sasa tuna Mapapa wawili, anayeongoza Kanisa Papa Fransisko na Papa aliyejiuzuru Papa Benedikto. Hata hili la Makadinari laweza fanyiwa kazi kwa muda.

2. Mapadre na Masista wote waliofanya makosa wakasimamishwa waondolewe vifungo vyao nakufanyiwa Recruitment mpya ya kiroho ili waendelee na kazi ya Mungu. Mnapomfunga Padre au Sista mnafunga Kanisa kiimani.

3. Mapadre walioondoka na kuacha Upadre na kuamua kuoa, warudishwe na kuwafanya kuwa Mapadre Walei huku wakiendelea na familia zao, wakitokea makwao.

4. Mashemasi wote waliokatizwa nakuamua kuoa, wapadrishwe na kuwa Mapadre walei.

5. Mafrateri waliofukuzwa kabla ya Ushemasi warudishwe na kutendewa haki zao

6. Watawa ambao wameanzisha familia wapewe vyeo vya kikanisa ili kulijenga upya kanisa

7.Wote waliowahi kupita seminaries wapewe nafasi ya kuhudumu shule za kanisa maana tayari ni hadhina ya Kanisa.

Nina mengi lakini sio lazima yafanyiwe kazi yote. Nawatakia mfungo Mtakatifu wa Kwarezima.

Ndimi kijana wenu;
Deogratius Nalimi Kisandu
MKOMBOZI WENU.
Mwanza, Tanzania.
Mmh..mbona avatar ya MKOMBOZI ina neno BANNED, mods wamemlambisha ban au ni mbwembwe tu?
 
Back
Top Bottom