Kanichunia baada ya kumwambia namuhitaji awe mpenzi wangu..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanichunia baada ya kumwambia namuhitaji awe mpenzi wangu.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by tindikalikali, Nov 2, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Ni rafiki yangu toka o'level, hatujawahi kwaruzana wala kupishana kauli. Kwa kipindi chote nimejitahidi kumuonesha kwa vitendo kwamba namjali na kumpenda. Miaka imepita tukiwa marafiki na nimeweza kumfahamu vizuri kitabia. Hivi majuzi niliamua kuvunja ukimya, na nimwandikia hivi "naomba unielewe ninachotaka kusema, sidhani kama itakuwa busara kwangu kumung'unya maneno, kwa kifupi nakuhitaji uwe mpenzi wangu, sisemi haya kwa bahati mbaya kwani najua nini nafanya na kumaanisha. Kumbuka ni ngumu kuukwepa ukweli, hata nisingesema leo basi ningesema kesho, naomba hekima na busara itawale maamuzi yako".....toka nimemtumia hiyo text kauchuna kimya wakati siyo tabia yake, sifikiri kama nimekosea kumwambia niliyomwambia, lakin nifanyeje ili nimlete katika mud yake ya mwanzo, maana nahisi hata urafik unaweza kwisha. Ushaur wenu wadau unahitajika.

  UPDATED
  Jamani nawashukuru wote mlionipa ushauri kunikosoa na kunipa zaidi. Tumepanga tukutane leo jioni, kitakachojiri nitawajuza. jumapili njema kwenu nyote
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hata ningekuwa mimi ningekuchunia.
   
 3. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kwanini dada, ebu funguka ili nijue nilipokosea.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  He!
  Mi mwenyewe sijaona kosa hapo!
  Labda kwa vile ni miaka mingi toka nilipotongoza kwa mara ya mwisho!
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ningeuchuna kwasababu ningekuwa nafikiria cha kukujibu.
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mara ya mwisho umetongoza lini?

  Hakuna kosa hapo.
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Umetongoza mno siriaz. Mdada anahisi mkiwa wapenzi yatakuwa siriaz mno. Unatongoza kwa vituo kama unaomba kazi ikulu?!!!
   
 8. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  hapo nimekuelewa, na nahisi ndicho anachokifanya. Bado najiuliza ikiwa nimchunie pia au ndo nitaharibu?
   
 9. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mkuu hilo sikurifikiria, inawezekana ametishika ati?
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mwambie unampa muda wa kufikiria hilo swala taratibu. Halafu uchune.
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  nashukuru na itabidi nifanye hivyo sababu moyo ushapenda.
   
 12. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Acha woga wewe, mtoto wa kiume lazima ujiamini. Umefanya upumbavu kumtumia sms kqa issue muhimu kama hiyo, ulipaswa kutafuta muda wa kutosha umtoe outing ya nguvu mnaenda sehemu tulivu then mnakaa na kuongea vizuri mkiwa mmetulia sehemu isiyo na bughudha then unaongea naye vizuri kwa kujiamini huku ukimtazama usoni.
  Ktk hayo maongezi yenu jitahidi sana kumhakikishia juu ya mustakabali wa maisha yake ya baadaye ktk uhusiano wenu, hayo mambo kwao ni muhimu sana.
  Kuwa kwake kimya kusikutishe, huenda amepatwa na mshtuko coz haamini kama uko serious ama lah, na pia njia ulotumia ni ya kitoto zaidi inamfanya akuone kuwa hauko serious. Kama unaweza mpigie simu.
   
 13. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mkuu unayoyasema inawezekana yana ukweli ndani yake, lakini nikimpigia simu si inawezekana nikawa naendeleza unaoitwa utoto?
   
 14. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  ukiwasha moto, unakomaa na kama kuuzima ni yeye
   
 15. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hamna unajua wanawake wanapenda sana kupigiwa simu. Hiyo itakusaidia kujua yuko kwenye mudi gani, kuliko kukaa unajiuliza maswali mengi na kudhani umeharibu kumbe amefurahia ujumbe. Halafu ujue watoto wa kike kamwe hawazoi kutongozwa, lazima atakuwa na aibu tu labda ile mikahaba iloshindikano. Ila ukipiga mtake hali tu na wala usiulizie chochote kuhusu ujumbe labda mpaka aanze yeye.

  Ila ni muhimu sana ukatafuta siku nzuri mkae pamoja kwa utulivu umseleze bayana tena bila kupepesa kope.
   
 16. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yah!Itaonekana kweli unaendeleza utoto maana plan uliyoanza nayo ilikuwa ya kitoto pia!Usingetumia sms method.Sasa bado hujapoteza point.Nenda na plan B,Mtafute umvae face to face!Naujitutumue kweli,,halafu ujipe moyo kwamba hata akikataa hamna kesi na wala hawezi kukuchapa.GO AHEAD!
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mahakamani mtu akisomewa shitaka halafu akauchuna maana yake anakubaliana na kosa! Mkuu hiyo ngoma inakuhusu jiandae kuicheza kwa raha zako!
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndo ilikuwa zangu ukiwa rafiki yangu then unambie me love u ndo mwisho wa mawasiliano ha ha ha
   
 19. Rashdind

  Rashdind Senior Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  umetisha bro.
   
 20. Ansah Miles

  Ansah Miles JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Next time usirudie kuandika andika text ni tabia za kitoto na kutokomaa vizuri,wasichana wengi ni wajanja sana na wanahitaji mtu mwenye msimamo na msimamo unauonyesha wapi,unauonyesha kwenye mazungumzo ya ana kw ana na si kutumiana msg,umuhimu wa ana kwa ana unamsoma mwenzako(body language) anavyobadilika kulingana na unaloongea kwa wakati huo na kama muud inabadilika unajua namna ya kui-control mapema....anyway tusiandike mengi nafasi unayo mtafute upange mashambulizi vizuri uso kwa uso jino kwa jino wajanja wanafanya hivo...
   
Loading...