Kaniambia nisome Zaburi 109. Naomba mnisaidie kunifafanulia

Taured

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
806
670
Wadau Kuna mdada nilikutana nae humu mitandaoni tukaelezana ya kwetu mpaka na contacts tukapeana tukatafutana mpaka tukaonana!

Tukakubaliana tuingie kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa sharti la kupima afya kwanza! Kabla ya kupima afya huyu mdada alinipeleka mpaka kwa ndugu zake wa karibu nikakaribishwa vzr sana chakula na vinywaji vya kutosha nikahisi Niko peponi
Basi baada kwenda kupima afya majibu hayakuwa mazuri kwa upande wa huyu mdada! Ilikuwa patashika kuukubali ukweli kwamba tayari ameathirika!

Baada ya ushauri na nasaha nyingi ikabidi akubali hali yake na aanze rasmi dozi. Sasa kazi ikabaki namna gani atawaeleza hao ndugu zake maana lazima wajue majibu. Alivyofika kwao baada ya kutoka hospital hali ikawa mbaya siku 2 halali mpka ndugu yake wa karibu akalazimika kunipigia simu akiniuliza umemfanyaje ndugu yetu mbona alitoka mzima hapa lakini baada ya kurudi hali yake imebadilika?

Na maneno mengine mengi na akanisihi nikwambie ukweli ni Nini kimetokea? Na hatosema popote na niamini kabisa anachosema! Kweli ni mama mtu mzima na hata huyu dada alinieleza kabisa kwamba huyo ni mtu wake wa karibu sananibkama mama yake !
Basi mm nilimwambia ukweli wa tatizo la mdogo wake akanishukuru kwa kuwa mkweli na akahaidi hatomwambia chochote kwamba nimesema!

Pale hospital walitushauri mengi na kwamba kama tunapendana basi upendo usifena mm nikamtoa hofu kwamba nitaendelea kuwa nae karibu sitomtelekeza akiwa na shida aniambie kweli nimeendelea kumpa ushauri kumtia moyo na kumpigia simu na kumjilia hali kadri ninavyoweza! Tatizo liko hapa?

Majuzi alikuja kliniki kuchukua Dawa awamu ya pili na mm nilikuwa bizebize alitamani twende wote! Sikwenda ila baada ya kutoka nilihakikisha tunaonana tukaongea mengi tukala na kunywa! Katika maongezi akanisimulia jinsi alivyotaabika siku ya kwanza na kukosa usingizi!

Mimi nikamwambia kwamba nilipigiwa simu na dadako kuhusu afya yako nikaona ameshtuka sana he alikupigia nikasema ndiyo ila sikumwambia tatizo lako nikamsihi akuulize ww mwenyewe ! Ikimbukwe kwamba nilisha muuliza kwamba je umemwambia dadako tatizo lako?

Akanijibu kwamba hakukuwa na namna ya kukwepa maana hata alipoaga kuja kuona na mm alisema anenda kupima hospitali kwa hiyo majibu lazima angeyatoa? Lakini dada yake alinambia kwamba hakuema kitu na baada ya kuona hali yake si nzuri na usingizi hapati ndo akaamua kunipigia!

Sasa majuzi baada ya kutoka kuchukua dozi mawasiliano na mm yamekuwa shida. Nikimtext anajibu short tu na baadae akasema nimuache kabisa! Na mwisho kabisa kanitumia meseji nisome Zaburi 109: mimeisoma mpaka sijaelewa kamaanisha Nini Wakati sioni Kosa langu

Watalaamu wa maandiko tusaidiane hapa!
 
Kavunja ahadi waliyokubaliana ndo mana kammaindi kwann amsimulie dada ake sjui mama ake kama ameathirika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom