Kaniacha kisa kumwambia abadili dini

bidam90

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
271
184
Habari naombeni ushauri!!nimekuwa kwenye mahusiano na binti almost miaka minne japo ni dini tofauti yeye muislamu,mimi mkristo!!Tumefanya vitu vingi sana pamoja na kushirikiana katika mengi tu tangu tukiwa chuo mpaka baada ya kumaliza!in short anajua kila kitu kuhusu mimi nami pia hakuna nisichojua kuhusu yeye!!

Ukweli tumependana sana,mwanzoni tuliona suala la dini halitakuwa tatizo sana binti alijitahid sana kujifunza mambo yanayohusu dini yangu mpaka kuingia kanisani mda mwengine lakini alikuja kubadilika ghafla baada ya kwao kujua na kumgombeza sana kwanin anafanya mambo yaliyo kinyume na dini yake hivyo sikuendelea tena kumuhimiza kujifunza dini yangu.Aliacha kwenda kanisan na kuacha kabisa kufwatilia dini yangu!
Tuliendelea kuwa kwenye mahusiano pasipo kuingiza tena suala la dini!

Lakini lilikuwa ni suala linalomuumiza kila mtu hasa future yetu na watoto wetu ni ipi!na je vp wazazi watakubaliana nasi! Kusema ukweli wazazi na ndugu zangu wasingekubali kabisa hili suala!!nilimficha binti mwanzon na kumtia moyo tu kuwa wazazi wataelewa na kunikubalia kumuoa hivyo hivyo nilifanya hivi ili nisimpoteze na kumkatisha tamaa.

Siku zikazidi kwenda binti akawa hana amani kwani alikuwa anaitaka sana ndoa akaamua kwenda kuwaambia wazazi wake kuhusu mimi na walikubali!ila ukija upande wangu ni suala gumu sana wazazi na ndugu kuelewa!

Ikabidi tu nimueleze wazi kuwa upande wangu hawakubali wanataka abadili dini kwanza japo nilijua ni jambo gumu kwake na hukukubaliana nalo.Mwisho nikamuambia basi itabidi tufunge ndoa ya bomani akakubaliana nayo!wakati namueleza yote hayo wazazi wangu sijawaambia lolote na wala hawajui kuhusu mahusiano yangu na binti.

Siku zikawazinazidi kwenda huku nasita kufanya lolote sababu najua wazazi na ndugu zangu watanipinga.Binti akawa hana amani kwani marafiki zake wanaolewa yeye na mimi tumekwama.Ilifika kipindi binti akawa ananinunia kabisaa wala hajisikii kuongea na mie wala hataki kukutana kimwili sababu ya mawazo ya ndoa.

Nilimuelewa hali alonayo na kumuonea sana huruma kwani watu kibao wa dini yake wanaenda kwao kutaka kumuoa lakini anawakataa sababu yangu hilo lilikuwa linaniumiza kwani mda unazidi kwenda na hamna nachofanya!!

Sikuwa na jinsi ikabid niongee na mama yangu nimueleze kila kitu kuhusu mimi na binti mama alikataa kabisa na kuniambia hilo haliwezekani na hata binti akibadili dini bado litakuwa suala gumu kwani mwisho wa siku atarudi tu dini yake ya mwanzo!!

Nikambembeleza sana mama na kumueleza tulipotoka mbali na binti na jinsi tunavyopendana lakini mama aliishia kuniambia tu tafuta wa dini yako!
Ikabidi tu nimueleze binti ukweli kuwa home wamekataa kabisaa hata ndoa ya bomani hivyo nikamshauri abadili dini ili hili suala liwe jepesi kwetu na hasa future ya watoto wetu waje wapate malezi mazuri!!Binti alikataa kabisa na kuanza kunilaumu nimempotezea mda wake bure na kwanin sikumueleza mapema!alinishukuru na kuniambia maisha mema asanteni sana!!

Yaani kiukweli binti ananichukia sana mimi mpaka ndugu zangu!!Moyo unaniuma kwani nampenda sana na wala sio nia yangu kumpotezea mda au kutokumuoa ila changamoto kubwa ni dini!kila mmoja wetu hataki kubadili kumfwata mwenzake!!

Nimekwama sielewi nifanye nini?wazazi na ndugu zangu wananipinga na hawakubaliani na hili!huku binti nae kanikasirikia hataki hata kunisikia na namba zangu kafuta na kuniblock!hahitaji kuongea lolote na mie kashafanya maamuzi ya kuniacha anasema haikuwa fungu lake mimi kumuoa!!

Naumia sana hasa mda wote tulokuwa pamoja na upendo wangu kwake!Anaona mie nimempotezea mda na simpendi kwani nimekuwa upande wa wazazi na ndugu zangu pia ni selfish nataka abadili yeye tu dini na sio mimi!!
 
Nawasifu huo muda pia mlokaa pamoja

Mkuu tafta wa dini yako hata mama kakuambia hivo, kwanza using'ang'anie kua na mtu ambae unaona kabisa future yenu ina kiza, kama unaona haitafua dafu mbeleni achaneni despite hiyo miaka mmekaa, ona tu hamkupangiwa kua pamoja na kila mmoja akafunga ukurasa mana mwisho wa siku lazima maisha yaendelee

Mahusiano mengi ya dini tofauti hayadumu haswa ikiwa kuna familia au familia zenu zote mna misimamo na dini zenu, usifosi kabisa kurudiana naye tafta wa dini yako tu huo ndio ukweli japo mchungu.
 
Dont be blinded by your human emotions.

Muoane kwa ndoa ya bomani huku nyie ni dini tofauti then watoto wenu watakuja kufuata dini ya baba au mama? Au watakuwa na dini yao mpya ya bomani?

Acheni mapenzi ya utoto, fikirieni maisha yenu miaka 10,20,30 yatakuwaje? Sio kuwa vipofu sababu ya kupendana kwenu.

Wazazi na ndugu zenu wako sahihi. Kama mmoja wenu hawezi badili dini achaneni tuu maana huko mbele mnatengeneza bomu.

Unforgetable
 
Mapenzi ya dizaini hii huwa yanahitaji kujua msimamo wa kidini wa mwenzako hasa mnapokuwa na dini tofauti mwanzoni kabisa mwa mahusiano yenu.

Tofauti za kidini zimekuwa ni tatizo kubwa sana,kwani kuna watu unakuta tayari washajenga familia( watoto) wakitaka kuoana familia na ndugu wamekuwa wakitoa vikwazo.

Pole sana mkuu tafuta wa dini yako. Huyo wa sasa naamini hata hisia juu yako zimeanza kupungua na pia analofikiria akilini mwake ni ndoa tu.
 
Naamini suluhisho Mama ameshakupatia. Ikiwa ulihitaji maamuzi mazuri, basi bi mkubw wako ashamaliza. Sasa sijajua nia ya wewe kukileta hiki jukwaani hapa. Au unataka tukushauri uslim?
Maana naona unaleta hoja za kutoka mbali na binti,
 
Pole ila majibu unayo.Ushasema dini ni kikwazo..option ilikua ndoa ya bomani watoto waje kufuata dini yako sasa umeshindwa wewe, binti wa watu hana kosa. Simply chanzo cha tatizo unacho na hitimisho unalo as well.Mliyofanya pamoja ni merely histry!
 
Kumwambia mtu abadili dini ni kosa ambalo niliapa kutokuja kulifanya iwe kwa mwanamke au kwa mtoto wangu na hata watoto zangu nimewambia wasije kujalibu kosa hili

Kama unaona huwez kuishi na mtu wa imani tofaut bhas ni vyema uwe unawauliza mapema ili ujue kama ni wa imani unayotaka!

katika vijana wangu kadhaa nilionao wapo watatu ambao mama zao ni Muslims,sikuwah kuwambia mama zao maswala ya kubadili na hata watoto wangu wawili walipofika umri flani waliamua kufata dini za mama zao na nililidhia kwa moyo mmoja maana daima naamini kuishi na mwanamke dini tofaut haikuondolei hadhi ya yako ya kuwa mume na pia kuwa na mtoto dini tofaut na ww haikuondolei hadhi yako ya kuwa baba yake
Pawaga
 
Hatuoi dini,tunaoa MTU,kubadilisha dini,sio swala la siku moja,nyie mlitaka mbadilishe majina,na taratibu za kuabudu.

Muanze kuabudu sehemu nyingine,ambayo amuamini!

Hivi unaanzaje tu ghafra kuwa Mkristo au Islam?kama wito huo hautoki moyoni,na sababu pekee,iwe baada ya mafundisho ya kina,na ukaweza kuona ukweli upo wapi.sio presha za kuoana.

Nyie nyote,bado hamjakomaa,swala dogo kama hilo,linawapa shida?

Chukua mtoto,piga mimba,weka ndani!
Ndoa inafungwa Mbinguni,hapa duniani,ni taratibu tu!
 
Mayahudi huwa wanawashauri wakristo kuwa kumfanya muislamu kuingia kwenye ukristo ni kitu kigumu sana, wasiwekeze juhudi zao katika kumfanya muislamu kuwa mkristo kwa kuamini Yesu ni mwokozi wa maisha yake hilo halitowezekana.

Wanachotakiwa kufanya ni kumweka muislamu kwenye mazingira magumu ya kufanya dini yake, kama vile akose swala kwenye baadhi ya vipindi, asikilize miziki aingie kwenye uzinifu akiwa pamoja na imani yake.

Ila kamwe hatomkubali Yesu kuwa mwokozi wa maisha yake KATU KATU KATUUU!!
 
We jamaaa badili dini fasta baada ya muda unaongeza mke unamiliki watoto kama wanne hivi
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom