Kangi Lugola; Weka Sawa Rekodi, Hii Kitu Ulishinda, Ulisamehewa au Walipotezea?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,702
71,013
Umepewa kazi takatifu sana na bahati nzuri umeianza Kwa mbwembwe nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuvaa bendera ya taifa na kutembea na ilani ya ccm.

Lakini kama ilivyo mashaka kwa mchungaji au shehe mwenye rekodi ya ugoni kumpa kutatua migogoro ya ugoni, hivyo hivyo ni ngumu kumuamini Waziri mwenye tuhuma za kudai rushwa (sio kuomba) kumpa asimamie wizara inayo pambana na rushwa wakati kesi yake imeisha bila uwazi.

Ni wakati Kangi asimame hadharani atueleze majibu ya maswali ya hapo juu kuliko kukazana na mfupa wa Lissu uliomshinda Mwigulu mtangulizi wake.

malisa_gj___Bt6eiK9h3ga___.jpeg
 
Elezea vizuri maana wengine smartphone tunemepata 2018 mwishoni kwahio hatuna habari..
Jamaa alikuwa na kesi ya wizi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona TV na radio zote zimezungumza sana kashfa yake na wabunge wenzie kudai Kwa mkurugenzi Gairo rushwa milioni 30 ili kamati yao isimlipue?
Walisomewa mashtaka baadae DPP akaondoa kesi.
Ila kuna tetesi ambazo tutaziweka baada ya uchunguzi kuhusu hatua hiyo ya kuondoa nini kilikua nyuma ya pazia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha, siku moja nikiwa nabadilishana mawazo na afisa mmoja wa polisi mkubwa kwa ngazi ya kitaifa "alisema"
Lugola hana lolote akishikishwa kitu kidogo atabwabwaja au hata kukusafisha kwa omo, hana lolote na ipo siku baada ya wadhifa wake tutamburuza selo
Umepewa kazi takatifu sana na bahati nzuri umeianza Kwa mbwembwe nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuvaa bendera ya taifa na kutembea na ilani ya ccm.
Lakini kama ilivyo mashaka kwa mchungaji au shehe mwenye rekodi ya ugoni kumpa kutatua migogoro ya ugoni, hivyo hivyo ni ngumu kumuamini Waziri mwenye tuhuma za kudai rushwa (sio kuomba) kumpa asimamie wizara inayo pambana na rushwa wakati kesi yake imeisha bila uwazi.
Ni wakati Kangi asimame hadharani atueleze majibu ya maswali ya hapo juu kuliko kukazana na mfupa wa Lissu ulio mshinda Mwigulu mtangulizi wake.
(Mods hili suala halipo mahakamani hivyo linakadilika)View attachment 1023705

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi?
Vetting inafanyika kweli siku hizi?
Miaka ya nyuma mtu akiwa na tuhuma tup, faili halirudi na kura ya ndio.
Lakini sijui bana!
 
Mimi siti ya pili nasubiri wajuzi watupe mrejesho wa huyo mvaa bendera.
 
Hivi?
Vetting inafanyika kweli siku hizi?
Miaka ya nyuma mtu akiwa na tuhuma tup, faili halirudi na kura ya ndio.
Lakini sijui bana!

Baada yakufanya vetting kikamilifu na bado tukaonekana kuangukia pua mara zote,basi tulikaa tukatumia busara na kuona basi ngoja tuwape wachawi watulelee watoto wetu.

Kumbe jasili haachi asili,hata kwa kuibia.
 
Hivi?
Vetting inafanyika kweli siku hizi?
Miaka ya nyuma mtu akiwa na tuhuma tup, faili halirudi na kura ya ndio.
Lakini sijui bana!
Kwenye vetting kuna tatizo kubwa kuliko inavyoweza kudhaniwa. Uteuzi unafanywa kwa kukomoa watu, kwamba "ngoja niwaonyeshe". Kuna watu wanakalia hizi ofisi kubwa za serikali lakini huku kwa wananchi inaonekana ni aibu na kuifanya serijkali ionekane kuwa ni ya hovyo hovyo na haiheshimiki tena!
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom