Kangi Lugola; Weka Sawa Rekodi, Hii Kitu Ulishinda, Ulisamehewa au Walipotezea?

Mbona TV na radio zote zimezungumza sana kashfa yake na wabunge wenzie kudai Kwa mkurugenzi Gairo rushwa milioni 30 ili kamati yao isimlipue?
Walisomewa mashtaka baadae DPP akaondoa kesi.
Ila kuna tetesi ambazo tutaziweka baada ya uchunguzi kuhusu hatua hiyo ya kuondoa nini kilikua nyuma ya pazia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona unatuuliza sisi,subiri huo uchunguzi wako ukamilike ndo utuambie huo umbea wako
 
Umepewa kazi takatifu sana na bahati nzuri umeianza Kwa mbwembwe nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuvaa bendera ya taifa na kutembea na ilani ya ccm.

Lakini kama ilivyo mashaka kwa mchungaji au shehe mwenye rekodi ya ugoni kumpa kutatua migogoro ya ugoni, hivyo hivyo ni ngumu kumuamini Waziri mwenye tuhuma za kudai rushwa (sio kuomba) kumpa asimamie wizara inayo pambana na rushwa wakati kesi yake imeisha bila uwazi.

Ni wakati Kangi asimame hadharani atueleze majibu ya maswali ya hapo juu kuliko kukazana na mfupa wa Lissu ulio mshinda Mwigulu mtangulizi wake.

(Mods hili suala halipo mahakamani hivyo linakadilika)

View attachment 1023705

Sent using Jamii Forums mobile app
niliweka jana wakalifuta
 
Hivi?
Vetting inafanyika kweli siku hizi?
Miaka ya nyuma mtu akiwa na tuhuma tup, faili halirudi na kura ya ndio.
Lakini sijui bana!

Mkuu vetting ikifanyike? Watoto wa pendwa wa mkulu wakina Bashite wakose hizo nafasi za utukufu na kula bata. Hapana mkulu hawezi kukubali.
 
Back
Top Bottom