Kangi Lugola: Watuhumiwa kufia mikononi mwa polisi ni Mitego ya kifo. Kwani wanaokufa wakifanya mapenzi mnachoma Kitanda?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397


Katika siku za hivi karibuni kumetokea tabia mbaya na chafu na ovu kabisa ya Mahabusu kufia kwenye vituo vya Polisi. Mahabusu wanapelekwa wanapata mateso yanayopelekea vifo vyao, kuna baadhi ya jamii zimekataa kuchukua maiti kwenda kuzizika

Kangi Lugola: Mwananchi kufa, anakufa wakati wowote na mahali popote . Sijui kwenye Quran lakini kwenye Biblia ukisoma Muhubiri 9:12 kifo ni mtego, kifo humnasa mtu wakati wowote na mahali popote

Mtu anaweza kufa akiwa polisi, akiwa anafanya mapenzi, anaweza akafa akiwa kwenye gari anasafiri na aweza kufia hata humu Bungeni kwahiyo isije ikachukuliwa kwamba nayefika kituo cha polisi ni kwamba ameteswa

Lakini nikiri kuwa kuna matukio ya Watu kufia mikononi mwa Polisi, na pale ambapo matukio hayo yanajitokeza huwa tunafanya uchunguzi na ikibainika Polisi wanahusika huwa tunachukua hatua

> Na ndio maana tunawazuia wananchi wasichukue sheria mkononi na kwenda kuchoma kituo cha polisi. Mbona huyu anayefia akifanya mapenzi mbona hawaendi kuchoma kitanda?
 
Ni kweli Binadamu anaweza Kufa Sehemu yoyote ile na Wakati wowote ule lakini kila Kifo kinazo Sababu zake ,hao wanao fia Vituo vya Polis pia sababu zipo na kubwa ni kipigo na Mateso makali.Wana wachukua Ndugu zetu wakiwa wazima kabisa na kuturudishia Maiti ,sio sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom