Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Katika siku za hivi karibuni kumetokea tabia mbaya na chafu na ovu kabisa ya Mahabusu kufia kwenye vituo vya Polisi. Mahabusu wanapelekwa wanapata mateso yanayopelekea vifo vyao, kuna baadhi ya jamii zimekataa kuchukua maiti kwenda kuzizika
Kangi Lugola: Mwananchi kufa, anakufa wakati wowote na mahali popote . Sijui kwenye Quran lakini kwenye Biblia ukisoma Muhubiri 9:12 kifo ni mtego, kifo humnasa mtu wakati wowote na mahali popote
Mtu anaweza kufa akiwa polisi, akiwa anafanya mapenzi, anaweza akafa akiwa kwenye gari anasafiri na aweza kufia hata humu Bungeni kwahiyo isije ikachukuliwa kwamba nayefika kituo cha polisi ni kwamba ameteswa
Lakini nikiri kuwa kuna matukio ya Watu kufia mikononi mwa Polisi, na pale ambapo matukio hayo yanajitokeza huwa tunafanya uchunguzi na ikibainika Polisi wanahusika huwa tunachukua hatua
> Na ndio maana tunawazuia wananchi wasichukue sheria mkononi na kwenda kuchoma kituo cha polisi. Mbona huyu anayefia akifanya mapenzi mbona hawaendi kuchoma kitanda?