Kangi Lugola safari ya kuondoa jinamizi la ajali hapa kwetu lawezekana

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,223
35,148
Mh. Kangi Lugora yawezekana tukafika kwenye hatua ya kupumzika kutuma rambirambi kuhusiana na ajali za barabarani lakini kufika hapo mlima wa kupanda slope yake ni balaa. There's a very steep mountain to climb.

Angalia haya kwa wenzetu:

US lawmaker caught speeding tells cop he often does so

Kumbuka katika zilizokuwa reported peke yake, jana wamekufa wawili wakiwa na gari ya serikali (SM).

Leo affiliate wa channel Ten kafariki na gari binafsi.

Kufika katika hatua hiyo ambayo sote tunaitamani sana ya kumaliza ajali, sense nzima ya slope ninayoiongelea ni kama hii hapa:

1. Karibisha maoni ya wadau wakupe uzoefu. Penye wengi hapa haribiki Jambo.

2. Jifunze uzoefu wa nchi nyingine na ajali. Tanzania si kisiwa. Nchi nyingine utaratibu wao barabarani ukoje? Uko kama kwetu? Je kwetu ni bora zaidi? Je una mapungufu?

3. Rekebisha vipaumbele vya polisi tokea kushinikiza na kukusanya mapato vs usalama barabarani kama msingi wao wa kwanza wa kuwapo kwao kama institution.

4. Wekeza katika kuona kuwa haki inatendeka kivitendo kila linapohusishwa jeshi la polisi. Kwa nini semi hizi ziendelee kuwapo?: " kuingia polisi ni bure bali kutoka kwa pesa." Matumizi ya nguvu peke yake kushinikiza mambo hakujengi.

5. Kuwa macho na polisi watoa matamko na hasa yanayo kinzana na sheria zilizopo. Simamia polisi kusimamia sheria na si kutunga sheria kupitia katika matamko yao. Asiwepo aliye juu ya sheria.

Ni ukweli usiopingika kuwa ukifungua milango utapata michango ya mawazo itakayopalilia ahadi yako kuhusiana na ajali kuwa ya mafanikio.

Mafanikio yako katika hili ni mafanikio yetu.

Hatupo nyuma yako bali tuko bega kwa bega nawe, kama alivyopenda kusema hayati Kenyatta (rip).
 
Nikimuona tu namfananisha na boss wangu. Sizani kama anapokea maoni.
 
Kama kashindwa kumsikikiza mkewe anayempa utamu Kila siku je ataweza kutusikikiza sisi tunaompa kura Mara moja kwa miaka mitano?
Uchafu ni hulka, kama sio hulka Basi ni masharti ya mganga
Wife wake alifariki mwaka jana,so mchizi yuko free kutupia masurupwete!
 
Kama ulivyosema uchafu ni hulka ya mtu au masharti ya Mganga,kutokua na mke sio sababu yakuvaa hovyo hovyo,suruali kubwa kama shuka la unga la mashineni!!

Mwenzake alikua anatembea na skafu ya bendera ya Tanzania shingoni,but now tupo nae uraiani,so asipende sana sifa kwa stone,stone hua hatabiliki!!

Sasa hivi mwanae kipenzi hawapatani kabisa,unaweza shangaa anytime akaimba nae!!
 
Kama ulivyosema uchafu ni hulka ya mtu au masharti ya Mganga,kutokua na mke sio sababu yakuvaa hovyo hovyo,suruali kubwa kama shuka la unga la mashineni!!

Mwenzake alikua anatembea na skafu ya bendera ya Tanzania shingoni,but now tupo nae uraiani,so asipende sana sifa kwa stone,stone hua hatabiliki!!

Sasa hivi mwanae kipenzi hawapatani kabisa,unaweza shangaa anytime akaimba nae!!

yule sio mchafu ila rafurafu hayuko decent, kuna watu watasema hapa kazi tu, Marekani uchaguzi uliopita ndio wamevunja mwiko wa kutochagua raisi handsome, wengi wanapenda raisi wao awe handsome, huenda Trump alipita kwa sababu alipambanishwa na dame.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom