Kangi Lugola: Ni marufuku kuanzisha mijadala juu ya kutekwa kwa Billionea Mo Dewji

Any way. Katika mijadala ndio kuna suluhisho la jambo. mara nyingine majibu yanapatikan akwenye mijadala hiyo. Kukataza ni kuminya upenyo wa kujua mengi nje ya pazia. Tusijiwekwe na kufungwa ndani ya box. kwenye mijadala mnaweza mkakusanya ushahidi wa kuwasaidia kuweza kumpata MO.

Ushauri tu na sio mjadala
 
Katoa sababu gani huyu kangi? Au tu Luna watu hawajisikii vizuri jambo likiwa motoo
 
Wasalaam, kwa mujibu wa gazeti la Serikali (habari Leo) toleo la leo

IKIWA ni siku nane tangu mfanyabiashra maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘MO’ atekwe na watu wasiojulikana, mijadala mbalimbali minne imetawala miongoni wa watu na kwenye mitandao ya kijamii, imebainika.

Dewji (43) alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11, mwaka huu katika Hoteli ya Colloseum, Oysterbay Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kufanya mazoezi (gym) na kusababisha hali ya taharuki katika jamii ya kitaifa na kimataifa huku mijadala mbalimbali ikiendelea.

Mijadala hiyo inahusu Sh bilioni moja zilizopangwa kutolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa ya kupatikana kwa bilionea huyo. Pia kuna mijadala kuhusu kumuombea arudi salama, mijadala ya kamera za hoteli alipotekewa lakini pia tahathari zinazotolewa juu ya utekaji.

Hata hivyo, akielezea moja ya mijadala hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliwaonya wale wanaoanzisha mijadala kuhusu mfanyabiashara huyo kuacha, kwani wanavyofanya nikuwazidishia simanzi wanafamilia wa mfanyabiashara huyo. Alisema, “Uchunguzi unaendelea, na kuna watu wanaosambaza taarifa ambazo ni za simanzi kwa wanafamilia wa mfanyabiashara huyo.

Ni vyema wakaacha kwani si jambo jema kipindi hichi ambacho wanapitia kwenye wakati mgumu.” Zawadi ya Sh bilioni moja Mapema Jumatatu wiki hii, msemaji wa familia ya bilionea huyo, Azim Dewji alieleza kuhusu zawadi ya Sh bilioni moja iliyotolewa kwa ajili ya yeyote atakayeweza kusaidia kupatikana kwa MO.

Baada ya tukio hilo, mitandaoni na mitaani watu mbalimbali wameibuka huku wengine wakitania kuhusu fedha hizo nyingi kuwahi kutangazwa kama zawadi hapa nchini. Ukipita kwenye mitandao ya kijamii, wengine wameandika; “Niko bize natafuta bilioni moja, wengine wameandika bilioni moja inaweza kuliwa bataa (Kustarehesha) kwa miaka 27.”

Lakini wengine wasema ‘Hii bilioni moja, si nikiipata nitaishi kifalme?’ Kuna baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi ambao wamekuwa wakitoka hadharani au kutumia mitandao kumuombea MO arudi salama. Hii pia ni moja ya mambo yanayojadiliwa zaidi tangu tukio hilo lilipotokea mapema wiki iliyopita.

Mijadala ya kamera za hoteli Kuna baadhi wanaohoji kuhusu kamera za usalama (CCTV) zilizokuwa zimefungwa kwenye hoteli hiyo, ambapo baada ya tukio kutokea, zilidaiwa kuwa hazifanyi kazi na hivyo taarifa juu ya watekaji hazikupatikana.

Mijadala hiyo inakua kutokana na kile ambacho wengi wanaeleza kuwa hoteli aliyotekewa bilionea huyo ni hoteli kubwa na ya kifahari, ambayo ilipaswa kuwa na mifumo bora ya ulinzi na usalama.

Tahadhari ya utekaji Baada ya tukio hili la mfanyabiashara huyo, wengi wamejiuliza kuhusu usalama. Licha ya Jeshi la Polisi kusema limeimarisha ulinzi kila kona, bado mijadala inahoji kuhusu hatari ya watu wengine kutekwa. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipozungumza na gazeti hili kwa simu jana alisema hawajafanikisha kumpata mfanyabiashara huyo na kazi ya uchunguzi inaendelea.
==========

Ushauri wangu:
Naona ni bora wakashirikisha vyombo vyote vya ndani vya ulinzi na usalama pia kuwashirikisha wananchi wote ili safari hii tuwajue watu wasiojulina ikibidi tujue hata vivuli vya hawa watu wasiojulikana maana wanalichafua taifa letu Tanzania.

Mwenyezi mungu tuokoe.
Samahani lakini ushamba si sababu ya kutoa matamko yasiyo na tija.
Jamal Kashoggi aliyeuwawa na nchi yake Saudia, anaongelewa asubuhi, mchana na usiku na waandishi wa habari.
Sasa ukwei wote unaonekana wazi.
Mficha kidonda maumivu yatamuumbua.
 
Haya ndiyo matokeo ya kuteuliwa watu kuwa viongozi wa idara bila ya kuzingatia elimu zao na vigezo maalum vya kumfanya astahiki kuwa kiongozi wa idara hiyo. Tunaongozwa na viongozi wasiokuwa na hekima na busara za uongozi. Ndiyo maana unasikia kila leo kiongozi mmoja anaripuka kuongea upuuzi tu. Shida tupu kwa kweli.

Back
Top Bottom