Kangi Lugola aburuzwa mahakamani leo, kesi yaahirishwa tena hadi 29/06/2017

nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
4,385
2,151
Amani iwe kwenu!

Awali ya yote nami nitumie muda huu, kumpongeza Rais wetu Dr. JPM na tume yake ya mchanga wa madini kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa taifa letu.

Sasa niende kwenye mada;
Leo tar.26.05.2017 katika mahakama ya ardhi mjini Musoma "The district land and housing Tribunal Musoma " mbunge wa Mwibara atakuwa na wakati mgumu kujibu tuhuma zake za.kupora ardhi ya mjane kinyume cha sheria.

Mh.Kangi kwa makusudi ameamua kuuza majengo yake yote kwa kanisa Katoliki jimbo la Bunda wakati yako katika sehemu ya mgogoro ulioko mahakamani.

Kanisa limenunua likijua kuna kesi mahakamani,sielewi kulikuwa na haraka ya nini kwa kanisa katoliki parokia ya Kibara jimbo la Bunda kununua majengo yaliyochini ya kiwango, kwa sababu yalijengwa ili kuwadanganya wananchi wamchague mbunge kwa madai kwamba, atatoa elimu ya ufundi kwa vijana wao kitu ambacho kangi ameshindwa kukitekeleza.

Mengi zaidi nitawaletea kutoka mahakama ya ardhi mjini Musoma eneo ambalo kesi leo inasikilizwa.

Naambatanisha na majengo ya kangi yaliyosehemu ya mgogoro na kuuzwa kwa kanisa wakati kesi iko mahakamani.

---Updates --
Naam, kesi ya msingi ilyopangwa kusikilizwa leo mahakama ya ardhi Musoma imehairishwa tena kwa mara ya 6 mfululizo toka mwaka jana tar.11.04.2016

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tar.29.06.2017 saa mbili asubuhi. Hakimu amepata dharura yuko safari.

Kutoka hapa mahakama ya ardhi mjini Musoma sina la ziada narudisha kwenu kwa uchambuzi zaidi.

Wasalaam.

1495774078826.jpg
1495774078826.jpg
 
Mbona unasema nyumba zimejengwa na lughola halafu mjane amedhulumiwa. Samahani ufafanuzi kidogo
 
Kesi ndiyo inaenda mahakamani. Lakini nuruyamnyonge umeanza kutoa hukumu dhidi ya Lugola.
Nakuomba uiache Mahakama ifanye KAZI yake.
Usitafute public sympathy.
 
Mkuu nakuelewa sana lakini hapa tunapeana taarifa tu. Kazi iko mahakamani na mahakama itafanya kazi yake. Hapa hatumuhukumu mtu. Ila kwa nafasi yake hakustahili kupora ardhi ya mjane.
 
Amani iwe kwenu!

Awali ya yote nami nitumie muda huu, kumpongeza Rais wetu Dr. JPM na tume yake ya mchanga wa madini kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa taifa letu.

Sasa niende kwenye mada;
Leo tar.26.05.2017 katika mahakama ya ardhi mjini Musoma "The district land and housing Tribunal Musoma " mbunge wa Mwibara atakuwa na wakati mgumu kujibu tuhuma zake za.kupora ardhi ya mjane kinyume cha sheria.

Mh.Kangi kwa makusudi ameamua kuuza majengo yake yote kwa kanisa Katoliki jimbo la Bunda wakati yako katika sehemu ya mgogoro ulioko mahakamani.

Kanisa limenunua likijua kuna kesi mahakamani,sielewi kulikuwa na haraka ya nini kwa kanisa katoliki parokia ya Kibara jimbo la Bunda kununua majengo yaliyochini ya kiwango, kwa sababu yalijengwa ili kuwadanganya wananchi wamchague mbunge kwa madai kwamba, atatoa elimu ya ufundi kwa vijana wao kitu ambacho kangi ameshindwa kukitekeleza.

Mengi zaidi nitawaletea kutoka mahakama ya ardhi mjini Musoma eneo ambalo kesi leo inasikilizwa.

Naambatanisha na majengo ya kangi yaliyosehemu ya mgogoro na kuuzwa kwa kanisa wakati kesi iko mahakamani.

---Updates --
Naam, kesi ya msingi ilyopangwa kusikilizwa leo mahakama ya ardhi Musoma imehairishwa tena kwa mara ya 6 mfululizo toka mwaka jana tar.11.04.2016

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tar.29.06.2017 saa mbili asubuhi. Hakimu amepata dharura yuko safari.

Kutoka hapa mahakama ya ardhi mjini Musoma sina la ziada narudisha kwenu kwa uchambuzi zaidi.

Wasalaam.

View attachment 514631View attachment 514631
Tupe kwa kifupi mjane alipokonywaje
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom