Kangi Lugola kuanza kukagua agizo lake la pikipiki kwenye vituo vya Polisi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
Waziri Lugola kupita vituo vya polisi kukagua bodaboda zinazoshikiliwa
Waziri Lugola kupita vituo vya polisi kukagua bodaboda zinazoshikiliwa

IMG-20190606-WA0158.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuanzia Juni 15 mwaka huu ataanza ziara katika vituo mbalimbali vya polisi kukagua utekelezaji wa agizo lake kuhusu jeshi hilo kuzishikilia bodaboda.

Mei 20 mwaka huu akiwa Bungeni Lugola alitoa maagizo kwa polisi akitaka pikipiki zinazokamatwa na kuwekwa vituoni ni zile zilizohusika katika uhalifu, zilizoibiwa na zisizo na wenyewe badala ya kuziweka kituoni bodaboba zenye makosa ya kofia ngumu au kupakia abiria zaidi ya watatu
Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Mwibara (CCM) ametoa kauli jana na kuahidi kupita hadi vituo vya polisi kuangalia utekelezaji wa agizo lake.
IMG-20190606-WA0156-300x200.jpg

“Nitapita kila kituo kwa nyakati tofauti kuangalia utekelezaji wa agizo hili. Hawatajua siku, saa wala dakika watashtukia nimeibukia kwenye kituo chao, nataka suala hili liishe ili tuondoe malalamiko ya muda mrefu ya vijana hawa kuhusu bodaboda zao.”

Aliongezea kuwa:“Nawaambia nikikuta kituo chako kuna bodaboda umezikamata tofauti na makosa niliyoanisha ile kauli ya ‘ama zao, ama zangu’ niliyoisema Bungeni itatimia siku hiyo,” alisema Lugola
 
Please my Minister,kama unapitia humu JF ungejufunza mengi na bila shaka kazi yako ingekuwa rahisi zaidi,elewa Wizara yako ni moja ya security cluster ya nchi means ni wizara moja nyeti sana,kwa waziri wangu kukimbizana na bodaboda hata sikuelewi kabisa,hii kazi waachie maafisa wa polisi(traffic)wewe umetoa agizo its ok,mambo nyeti ya kufuatilia nchi yetu ni pamoja na kupambana na human trafficking(hii ni mbaya sana ndani ya nchi yetu),Drugs(nchi yetu ni moja ya transit kubwa ya drugs),money laundering its worse ndani ya nchi yetu,pia mshauri our no 1 aigawe hii wizara ya mambo ya ndani katika wizara mbili;wizara ya polisi(ulinzi na usalama wa raia) na wizara ya mambo ya ndani(uraia na uhamiaji),hii itarahisha utendaji wa kuwahudumia wananchi,hasa kwa kuhakikisha raia wote wana life books na wameandikishwa na kurekodiwa kwenye central data systems ya nchi.
 
Boda boda ni size yake kabisa, wala usimpe majukumu asiyoweza,namsihi akimaliza hapo atoe na za simu kwa machangudoa ili wakusumbuliwa na polisi wampigie simu.
 
Anakagua wakati boda boda zimejaa vituoni police ndio wamefanya ulaji kupitia boda boda kupata rushwa au kuwabambikia kesi ni rahisi sana itasaidia kupunguza kero zisizo na kichwa wala miguu..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom