Kangi Lugola: Kauli ya Rais isije ikapotoshwa, hakuna anayeruhusiwa kulima kwenye chanzo cha maji

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. Kangi Lugola, amesema kuwa kauli ya Rais John Magufuli kuruhusu kilimo pembezoni mwa mto isipotoshwe watu wakanza kwenda kuvamia vyanzo vya maji na kuanza kulima. Hakuna anayeruhusiwa kwenda kwenye chanzo cha maji.

"Kauli ya Rais isije ikapotoshwa wakavamia maeneo na kuanza kulima, hakuna anayeruhusiwa kwenda kwenye chanzo cha maji".

Hayo ameyasema leo kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.
========

kirerenya wrote;

Baada ya rais kutoa ya kauli ya kuruhusu wananchi walime mpaka mtoni kusudi maji yakija yachukue mazao yao.​

Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais muungano na mazira mh Kangi Lugola leo bungeni amekuwa akiitetea kauli hiyo huku akisema rais hajavunja sheria na kwamba ametumia sheria ya mazingira namba 20 kifungu 57.

Kifungu hicho cha 57 kinampa rais au waziri kutoa kibali kibali cha kulima au kuendesha shughuli za kibinadamu katika eneo la mita sitini kando ya mto.

View attachment 626631

Mheshimiwa Lugola ameendelea kufafanua kuwa rais amewaagiza kuandaa mpango wa kuwaruhusu wananchi hao kulima katika eneo hilo bila kuathiri mazingira.
 
Naibu Waziri amesema leo bungeni mjini Dodoma kuwa kauli ya Rais John Magufuli kuruhusu kilimo pembezoni mwa mto watu wakaenda kuvamia vyanzo vya maji, "Kauli ya Rais isije ikapotoshwa wakavamia maeneo na kuanza kulima, hakuna anayeruhusiwa kwenda kwenye chanzo cha maji". Alisema Naibu Waziri Kangi Lugola

Tayari amekali kuti kavu
 
Baada ya rais kutoa ya kauli ya kuruhusu wananchi walime mpaka mtoni kusudi maji yakija yachukue mazao yao.​

Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais muungano na mazira mh Kangi Lugola leo bungeni amekuwa akiitetea kauli hiyo huku akisema rais hajavunja sheria na kwamba ametumia sheria ya mazingira namba 20 kifungu 57.

Kifungu hicho cha 57 kinampa rais au waziri kutoa kibali kibali cha kulima au kuendesha shughuli za kibinadamu katika eneo la mita sitini kando ya mto.

kifungu 20.JPG

Mheshimiwa Lugola ameendelea kufafanua kuwa rais amewaagiza kuandaa mpango wa kuwaruhusu wananchi hao kulima katika eneo hilo bila kuathiri mazingira.
 
Uwe muelewa, ataja kifungu cha sheria kinachomruhusu raisi au waziri muhusika kuruhusu kutumia ardhi iliyopo ktk kingo za mto, kabla hujaandika fikiri kwanza, kuandika hivyo nia yako kuupotosha umma, umwelewe vibaya raisi, basi utaeleweka vibaya ww

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona kama vile wewe ndiye sijakusomaaa. Jipange kwanza ndo unikosoe
 
Inapotoshwaje?kwani aliyeongea alitumia lugha ya kichina?Kwahiyo watanzania wote hatuna uwezo wa kuelewa kilichozungumzwa?kama lugha iliyotumika ilikuwa ni kichina sasa mkalimani aliyetafsiri mawazo ya mkuu alikuwa wapi?Na hii kazi ya kufafanua aliyoifanya hapa alipewa na nani? Watanzania tusifanywe mataahira.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom