Kangi Lugola: Kama waziri ataonyesha wapi katika bajeti ameweka ruzuku ya wavuvi najiuzuru ubunge

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
887
0
Mbunge huyo bingwa wa hoja kama ukawa amesema kama waziri ametenga ruzuku za wa vuvi katika bajeti yake atajiuzuru ubunge wake na kumpa waziri cheki ya milion 50,mbunge huyo amesema serikali ya ccm haiwapi ruzuku wavuvi hivyo amewataka watenge ruzuku za wavuvi haraka sana
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,598
2,000
Ha! Ha! Ha! Huyo jamaa anawahenyesha sana MAGAMBA ! Unajua bhana wakongwe walishasema kitambo sana kwamba MBWA UKIMJUA JINA TU basi hakusumbui !
 
Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,024
1,195
dah kaz kweli kweli watamfukuza na kumnyanganya kadi ya ccm

Hakuna anayeweza kumgusa maana haina impact hata ukimfukuza maana wanajua atarudi bungeni hata bila kupingwa hata na mgombea wa ccm jimboni kwake!
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,111
2,000
Hivi kwanza,kwa nini serikali inaendekeza ruzuku? Wachumi wetu wanaelewa principles za ruzuku kweli? Au ndio doing the same thing and expecting different results?

Naomba Mbatia aliangilie hili na kuliweka sawa kwenye bajeti yake.
 
theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
Sasa shida kuwekwa kwenye bajeti au pia kuhakikisha watalipwa.Sababu hizi bajeti utasikia ofisi ilitengewa bilion 1 zimefika 50million sasa na upewe hiyo break down yake?CAG mwenyewe huwa anakoma.
 
Tiba

JF-Expert Member
Jul 15, 2008
4,596
2,000
Hivi kwanza,kwa nini serikali inaendekeza ruzuku? Wachumi wetu wanaelewa principles za ruzuku kweli? Au ndio doing the same thing and expecting different results?

Naomba Mbatia aliangilie hili na kuliweka sawa kwenye bajeti yake.

Kama sijakosea, Lugola anayo degree ya uchumi au? Kama ndivyo basi ana uhakika na anachozungumza. Kama wakulima wa pamba, kahawa, pareto n.k wanapewa ruzuku kwenye pembejeo, kwa ni ruzuku isitolewe vile vile kwa wavuvi? Nafikiri hapo ndipo aliko base arguement yake.

Tiba
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,111
2,000
Kama sijakosea, Lugola anayo degree ya uchumi au? Kama ndivyo basi ana uhakika na anachozungumza. Kama wakulima wa pamba, kahawa, pareto n.k wanapewa ruzuku kwenye pembejeo, kwa ni ruzuku isitolewe vile vile kwa wavuvi? Nafikiri hapo ndipo aliko base arguement yake.

Tiba

Mimi nauliza kwa nini serikali inaendelea kutoa ruzuku, hasa kwa hao wakulima wa pamba,kahawa,pareto n.k. kama sekta imeshindwa kujiendesha kibiashara ni kuachana nayo tu.

ni michezo kama hii ndio inasababisha serikali kuendelea kutoa ruzuku kwa mashirika ambayo yamefail kujiendeshesha as business entities. TANESCO, TTCL,AIR TANZANIA N.K

sasa huyu kangi anataka kuiongeza serikali mzigo mwingine. what the hell is going on, on this part of the word?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom