Kangi Lugola: Kama risasi zilikuwa zikipigwa kiholela kwanini dereva wa Lissu hakupigwa na risasi hata moja?

Mhe. Rais aliwahi kusema kwamba huwa anawateua vichaa kama yeye, nafilkiri huyu Mkangi ni zaidi ya kichaa!
 
Hii kauli imenisikitisha sana.Kwa kweli kama haya ndio majibu dhidi ya usalama wa Wabunge na Raia,basi hali ni mbaya tofauti na tulivyofikiri.

Kangi Lugola inampasa kufahamu kuwa Uwaziri wake ni sababu ya Ubunge,huu ubunge huwa una kikomo,lakini kauli yake na matamshi hayana kikomo,yatadumu mpaka zile nyakati ambazo ukweli halisi juu ya shambulio hili utakapofahamika hata ikiwa baada ya miaka 20.

Kama waziri mwenye dhamana,hakutakiwa kujiuliza haya maswali ya kipumbavu kama sisi raia,tena yeye ni polisi mstaafu na Waziri mwenye vyombo vya kijasusi,yeye ndio alipaswa kuja na majibu.Sisi pia tunajiuliza,mpaka leo Naibu Waziri anakaaje eneo lisilo na CCTV,Naibu Spika anakaa mahali pasipo na CCTV?Je walinzi waliokuwa lindo nao hawajsema lolote?RPC wa Dodoma ilikuwaje ashindwe kukamata wavamizi eneo nyeti kama Area D?

Kauli ya Lugola imeonyesha kuwa Ulinzi kwa viongozi na raia sio kipaumbele na kwamba jeshi letu la polisi linachafuka katika kadhia hii.

Jamani mnatupa shida sana tuliojitoa kwa ajili ya huyu mtu na kumkampenia.Msifanye tujute.Leo Mwigulu kapata ajali watu wanashangilia?Tumefika huko kama Taifa?
Na wewe mkuu Barafu tunakuheshimu sana pamoja na kwamba wewe mdogo wangu! Hupaswi kujiuliza Mara mbili mbili kwamba huu mpango umeagizwa kutoka juu! Serikali unajua yote hayo! Bashite inajulikana kwamba siku Lissu anapigwa marisasi alkuwa Area D na siku hiyo jioni yake alilala Murogolo!
 
Kama risasi zilikuwa zikipigwa kiholela kwa nini dereva wa Lissu hakupigwa na risasi hata moja?- Waziri Kangi

Hii kauli anauliza waziri mwenye dhamana ya ulinzi baada ya kukanusha uwepo wa cctv kamera baada ya mwaka na miezi 7.

Lakini hajasema pia kama huwa hakuna walinzi? Na kamera kweli hazipo hata kwa Karemani & Tulia?

Na hajashangaa madereva wa Mwigulu na Kigwangala wametoka wazima kwenye gari ila anashangaa kwa Lissu?

Inamaana anataka kusema aliyepiga risasi ni dereva? Inamaana jeshi limeahindwa kuwakamata wapigaji risasi?

Na hataki kusema wale askari waliondolewa na nani? Yaani aliyetoa amri askari kuondolewa eneo lile.

IMG-20190213-WA0024.jpeg

Sent from my TECNO CX Air using Tapatalk
 
Kwa majibu haya ya lugola,kwanini lissu asiendelee kuwadharirisha kwa hoja?.

Na kadiri wanavyo jipanga kuvuta muda wa hili jambo eti litapita ndivyo wanavyo zidi jidanganyaa.
 
Leo nilikuwa nasoma biblia kitabu cha 2 mambo ya nyakati mstari wa 22.Unahusu mfalme Ahazia mwana wa Yoharamu mfalme wa Yuda. Ukiendelea mstari wa 4 mfalme alipowaua nduguze wote kwa upanga ba baadhi ya wakuu wa Israel pia. Mstari wa 7 unasema "Walakini Mungu hakupenda…" Ukiendelea mpaka mstari wa 14 "Tazama Bwana atawapiga pogo kubwa watu wako na watoto wako na wake zako na Mali yako Yote". Ukiendelea mstari wa 18 mpaka 20 ndio ikawa fungu Kazi ya mfalme aliyemwaga damu ya watu "Na baada ya hayo Yote Bwana akampiga matumbo kwa ugonjwa usioponyeka. 19 Ikawa baada ya siku ikiisha miaka miwili, matumbo yake yakatokea kwa sababu ya ugonjwa wake..." mwisho alifariki bila kutamaniwa. Yaani Hilo neno Leo limenipa moyo kuwa Mungu halali kila kitu kimekuja kwa sababu na ni naamini kwa Sasa asilimia 85 ya viongozi wote wanaoshuhudia hivi vitu ni wakristo wazuri na maadiko hayatasimama. BIBLIA ni maandiko yanayoishi. Mbarikiwe msome neon la Mungu

Utaambiwa mchochezi tena unashirikiana na mabeberu haaaaa haaaa.
 
Kama risasi zilikuwa zikipigwa kiholela kwa nini dereva wa Lissu hakupigwa na risasi hata moja?- Waziri Kangi

Hii kauli anauliza waziri mwenye dhamana ya ulinzi baada ya kukanusha uwepo wa cctv kamera baada ya mwaka na miezi 7.

Lakini hajasema pia kama huwa hakuna walinzi? Na kamera kweli hazipo hata kwa Karemani & Tulia?

Na hajashangaa madereva wa Mwigulu na Kigwangala wametoka wazima kwenye gari ila anashangaa kwa Lissu?

Inamaana anataka kusema aliyepiga risasi ni dereva? Inamaana jeshi limeahindwa kuwakamata wapigaji risasi?

Na hataki kusema wale askari waliondolewa na nani? Yaani aliyetoa amri askari kuondolewa eneo lile.
sokwe mwingine huyu mara kulikuwa hakuna kamera. Kama ana mke au watoto aonywe kwA laana anayoichimba.
 
Siku zote aalikuwa wapi kutoa majibu au anafikiri ,wenzie hawakuwa na wazo la kujibu hivyo .yeye Ndio kajiona mjanja .
 
Hili swali anamwuliza nani? Wananchi wanatarajia wahusika/wenye mamlaka watoe majibu kumbe nao wanauliza maswali!! Hongera awamu ya 5!!
 
Bado tuna safari ndefu sana yakujikomboa.Kama ayo ndo majibu ya waziri mwenye dhamana kazi ipo.Ukiona majibu yanakua ya namna hii jua ile kauli ya uongo ni mrefu na ukweli ni mfupi ni sahihi.Muda si mrefu itajulikana tu kwasababu ukweli una tabia yakujidhihirisha.
 
Kama risasi zilikuwa zikipigwa kiholela kwa nini dereva wa Lissu hakupigwa na risasi hata moja?- Waziri Kangi

Hii kauli anauliza waziri mwenye dhamana ya ulinzi baada ya kukanusha uwepo wa cctv kamera baada ya mwaka na miezi 7.

Lakini hajasema pia kama huwa hakuna walinzi? Na kamera kweli hazipo hata kwa Karemani & Tulia?

Na hajashangaa madereva wa Mwigulu na Kigwangala wametoka wazima kwenye gari ila anashangaa kwa Lissu?

Inamaana anataka kusema aliyepiga risasi ni dereva? Inamaana jeshi limeahindwa kuwakamata wapigaji risasi?

Na hataki kusema wale askari waliondolewa na nani? Yaani aliyetoa amri askari kuondolewa eneo lile.
Hii serikali imeshashindwa kwa kila kitu,je amesema kitu gani kilizuia huyu dereva asikamatwe muda wote alipokuwepo hapo Dodoma hospital au dereva alikimbia baada ya tukio- viongozi wetu hata aibu hawana tena.shame
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuna haja ya dereva ya Mbunge wa Singida Mashariki, Adam Bakari kueleza kwanini alipohisi kuwa wanafuatiliwa na watu wa siojulikana siku ya kushambuliwa kwa Lissu hawakuchukua hatua ya kulipeleka gari kituo cha polisi.

Kangi Lugoa ametoa kauli hiyo jana Jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema maelezo ya dereva huyo yanatia shaka, wanataka awaeleze mambo kadhaa yatakayosaidia uchunguzi wa tukio hilo.

"Kwa hali ya kawaida ni jambo la kushangaza risasi zote hizo wanasema 38, hata moja haikumpata dereva huyu,” alisema Lugola.

Waziri huyo pia amehoji risasi hizo kutoharibu kisanduku kilichopo katikati ya gari hilo sehemu ya mbele, kinachotenganisha dereva na abiria.

Kuhusu eneo hilo kuondolewa kamera za CCTV, Lugola amesema nyumba za Serikali jijini Dodoma hazina kamera hizo.

“Huu ni upotoshwaji mkubwa ambao unalenga kuwadanganya wananchi na kuwataka waichukie Serikali yao na Rais John Magufuli na mimi kama waziri wa mambo ya ndani sitokubali,” alisema.

Alibainisha kuwa eneo alilokuwa akiishi mbunge huyo linalindwa na askari wa kampuni binafsi za ulinzi, si polisi na kubainisha kuwa kutokana na utata huo ndio maana wanamtaka mbunge huyo na dereva wake kutoa maelezo kukamilisha upelelezi.

“Wao ndio walikuwepo watuambie hawa waliompiga risasi ni wanawake au wanaume, ni wanene au wembamba, warefu au wafupi,” alisema.
 
Back
Top Bottom