Kangi Lugola huu udhalilishaji wa traffic Dar umetia kinyaa, wanafunga makonda kama majambazi, na kuwapiga mbata wakati wanaingiza kwenye gari!!

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,299
2,000
wana JF,

Tukio lilotokea leo mbele ya macho yangu limenifanya nisiweze kulivumilia mpaka nikaandika. Leo majira ya saa nne na robo pale makumbusho stand, mimeshuhudia traffic akimwingiza konda ndani ya gari kwa kumsukuma na kumsindikiza kwa makonde na mbata, wakati huo mwingine akiwa amefungwa pingu mkono mmoja kwenye nguzo ya gari, ilibidi nishuke nikaulizia kulikoni leo kuna nini mbona traffic wako wengi na pia wanafanya kazi kwa vitisho sana, nikaambiwa leo wanafanya ukaguzi hawa wana maksa mbali mbali kama vile usafi wa gari na konda mwenyewe kama una makosa unapelekwa polisi kwa hatua zaidi.

Hili la usafi nakubaliana nalo kabisam hata la ubora wa magari pia, lakini hili la kupigwa na kufungwa pingu bado kizungu mkuti, makonda na madreva wanaotolewa kwenye magari hawana siraha kabisa, wengine hata miili yao ya kinyonge hawa nguvu lakini vitendo vya udhalilishwaji vinavotokea ni zaidiya ukaguzi.

Mh, Lugola kama traffic wamepewa rungu ya kuwa wanapiga watu na kuwafunga kazi basi kuna siku watakosa msaada kama wamaopigwa nao wakiamua wafanye wanachofanyiwa.

Kwa taarifa ya leo kama kuna watu wamepelekwa kulala ndani (makonda na Madreva) nendeni mkawaulize mjihakikishie niliyoyasema kama yametokea kweli, kama wameachiwa nendeni makumbusho mkapeleleze.

Msiniulize picha maana ningeweza kuunganisha kuwa nimeingilia polisi
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
4,372
2,000
Chuki dhidi yao wanasababisha wao wenywe ndio maana hua wakijichanganya hua wanaipata fresh
 
kajekudya

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
1,062
2,000
Askari wanna shida ya kukosa Weledi, lakini pia wakati mwingine wanashindwa kujiamini. Kuna siku nilikuta kundi la Wajeda wakifanya ukaguzi sehemu, baada ya kunikagua wakaniomba kitambulisho, nikawaambia sina, bana nikafanya kosa moja kuwambia kanafasi kangu kwenye Selikali ya Anko. Bwanawee jamaa nikaona kabisa wamepanic na wakaanza kuhisi nakataa kutoa kitambulisho makusudi, Jamaa wakanizunguka kama kumi hivi na mabunduki, niliogopa sana. Lakini nikajiuliza mimi mtu mmoja na nimeshakaguliwa, sina silaha yoyote, kulikuwa na haja gani kunizunguka na Mabunduki jumlisha vitisho juu. Kiukweli they are too robot!!
 
BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,037
2,000
Wana maagizo ya kukusanya kiwango fulani kwa mwezi. Na siku zote anaeumia ni mlalahoi. Kama ulifikiri kuna serikali ya wanyonge unajidanganya sana.
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,052
2,000
Mimi kwa mtazamo wangu nafikiri ya kwamba kwa usafi wa gari, mmiliki wake ndiye anawajibika moja kwa moja. Ila kwa upande wa makondakta na madereva, wengi wao ni wachafu sana kutokana na mavazi wanayoyavaa kutoyali wala kuyapenda, hili ni Jambo dhahiri kabisa. Nafikiri zaidi ya kwamba, hawa watu hawakushirikishwa katika kuyachagua kama "dressing code" zao zinavyoelekeza (kama zipo?!?

Nafikiri pia ya kwamba, kupitia vyama vyao vya madereva na makondakta, wangepewa fursa ya kuchagua mavazi fulani wanayoyavaa wanayoyatamani na kuyapenda, mathalani jeans na T-shirts ambazo zingewafanya wawe nadhifu, wasiwe wanavaliana na wenye kuyathamini (angalizo, sivyo milegezo). Katika mchakato huo jeshi la polisi nalo lishirikishwe pia katika kutoa elimu zaidi, ili kuepuka kutumia nguvu tu pasipo sababu za lazima katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,543

Tatizo lenu hamfikiri nje ya box, hamuoni tatizo la abiria kujazwa kama mihogo kwenye daladala. Ikija Ebola nchi hii idadi ya Morogoro itakuwa kama sifuri.
Sijui itaundwa Tume tena?
Au watasema ni
 
"Elimu jamani, watu hawajui hatari ya Ebola"
Ni watu gani hao, kama sio watekelezaji wa sheria za usalama barabarani?
 
Betoratekha

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
328
1,000
Heshima ya polisi katika nchi hii ipo chini ikilinganishwa na heshima ya Gaidi maana ni Bora gaidi kuliko polisi wa nchi hii.
 
Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
802
1,000
Tatizo lenu hamfikiri nje ya box, hamuoni tatizo la abiria kujazwa kama mihogo kwenye daladala. Ikija Ebola nchi hii idadi ya Morogoro itakuwa kama sifuri.
Sijui itaundwa Tume tena?
Au watasema ni
Hujaelewa mleta Uzi kilichomfanya akupe habari hii.Shida si ukamataji wa makosa.Bali ni kumuadhibu Konda kwa kumfunga pingu na kumpiga.Kitu ambacho hakipo kisheria.Mwisho wa siku wakipewa 3000/=issue yote inaisha.Wanatumia ubabe ili uwape Rushwa
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,299
2,000
Hujaelewa mleta Uzi kilichomfanya akupe habari hii.Shida si ukamataji wa makosa.Bali ni kumuadhibu Konda kwa kumfunga pingu na kumpiga.Kitu ambacho hakipo kisheria.Mwisho wa siku wakipewa 3000/=issue yote inaisha.Wanatumia ubabe ili uwape Rushwa
Wewe umenielewa . mtu avae viatu vya makondo makosa ya magari ya mabosi wao kesi wanapewa wao badala ya kuitwa kwa utaratibu wanafungwa pingu na kuingizwa uvungu wa magari kama majambazi. Ingawaje uzi huu wa muda lakini hili tukio niliona live
 
isambe

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
2,161
2,000
Kweli unamtetea konda au dereva wa daladala!,unayajua maudhi yao hao viumbe huko?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom