Kangi Lugola: Hakuna mtu muongo kama CAG Assad! Akithibitisha madai yake nitajiuzulu

Hapo waongo wao. Ujue hizo sare wamezishona na kuzijaza kwenye hayo makontena baada ya Assad kuwapitia,ndio wakastukia itakuwa soo
 
Kama Magu hamfukuzi kazi Lugola basi amebariki kauli za dhihaka kwa CAG.
Wizi wa mzigo huo wa sare za polisi alianza Rais mwenyewe na hata katibu mkuu Mambo ya Ndani alitoa taarifa yake na TAKUKURU wamehusishwa uchunguzi huo.
Hivyo kauli ya CAG kuwa mtu muongo kuliko wote Tz amemaanisha hata Rais ni muongo na TAKUKURU walewale walio msamehe rushwa yake ya kule Kilosa nao ni waongo.
Kweli mtembea na Ilani hana adabu!
 
Vijana wasomi wa Bunda fursa hii 2020 kule Mwibara maana barabara ya Kisorya bado hata lami hajawamalizia miaka 5 imeisha tayari.
 
IMG_2965.JPG
 
CAG naona amekuwa mwiba mkali kwa watawala.Sasa wanaibuka kutoka mafichoni kujitetea kwa hoja mufilisi.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Lugola amesema hakuna mtu muongo kama CAG na kwamba yupo tayari kuweka uwaziri wake rehani, ikiwa itabainika kuwa taarifa zake za ukaguzi kuhusu sare hewa za jeshi la polisi zilizogharimu Sh16bilioni ni ya kweli.

Kutokana na ukaguzi alioufanya, Profesa Assad alisema ukaguzi ulibaini mahitaji ya kitaalamu kutoka idara inayotumia mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS), ulibaini kuwa mahitaji ya kitaalamu kutoka idara inayotumia mfumo huo hayakuzingatiwa wakati wa kuthamini na kutoa zabuni.

“Malipo ya Sh3.30 bilioni yalifanyika kwa mzabuni kwa ajili ya huduma ya matengenezo na msaada wa kitaalamu wa mfumo wa utambuzi wa alama za vidole,” amesema.

Alisema huduma hiyo ilipangwa kufanyika kwenye mikoa nane ya kipolisi ya Temeke, Mwanza, Simiyu, Tabora, Kigoma, Geita na Kinondoni lakini Polisi ilishindwa kuthibitisha kuwa matengenezo hayo na msaada wa kitaalamu ulifanyika.

Profesa Assad alisema vifaa vya utambuzi wa alama za vidole vyenye thamani ya Sh1.73 bilioni havikufungwa kwenye magereza 35 kama ilivyoainishwa badala yake, vilihifadhiwa katika ofisi ya upelelezi Makuu ya Polisi.

“Malipo ya Sh604.39 milioni kwa ajili ya mafunzo kwa wataalamu 30 hayakufanyika,” amesema.

Alisema jeshi la Polisi lilishindwa kuionyesha timu yake ya ukaguzi zilipo monita 58 za kompyuta aina ya Dell zenye thamani ya Sh159.16 milioni zilizopelekwa kwenye kitengo cha cha uchunguzi wa kisayansi cha Makao Makuu ya Polisi (Forensic).

Pia, alisema monita 213 za kompyuta aina Dell zilizolipiwa Sh195.22 milioni kwa mzabuni Lugumi Enterprises Limited lakini mzabuni hakuzikabidhi.

Pia, alisema ukaguzi wa ununuzi wa sare za askari umebaini jeshi hilo lilipa Sh16.66 bilioni zililipwa bila kuwapo na ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa sare hizo za polisi wa Boharia Mkuu wa Polisi.

“Pia nilibaini maoni ya kisheria ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanayohusu uwasilishaji wa kiapo cha nguvu ya kisheria (Power of Attorney) na leseni halali ya biashara hayakuzingatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara wa Mambo ya Ndani wakati wa kusaini mkataba namba ME 014/PF/2015/2016/G/30 Lot 2 uliohusu ununuzi wa sare za polisi,” alisema.

Profesa Assad alisema anapendekeza Jeshi la Polisi lihakikishe vifaa vya utambuzi wa alama za vidole vinafungwa maeneo husika na kuanza kutumika ilivyokusudiwa.

MY TAKE:

Tunaomba msimdhuru CAG wetu Assad wala kumsumbua. Tunataka mbishane kwa hoja sio Vitisho. Msanii wa Bongo Fleva Roma Mkatoriki aliimba "WEKA SILAHA CHINI TUBISHANE KWA HOJA".

Kwa hili Swala naomba Lugola na Polisi wako muwe wapole kama mnanyolewa.

Kumbuka: Mwigulu Nchemba alijaribu kimshambulia Assad akaondoka kwenye uwaziri akamuacha Assad anadunda. Assad ni kitukuu cha mtume.

=====

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema hajawahi kumuona mtu muongo katika nchi hii kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.

Amesema anauweka rehani uwaziri wake ikiwa itathibitika kuwa taarifa za ukaguzi wa CAG kuhusu sare hewa za Jeshi la Polisi zinazofikia Sh. bilioni 16 ni ya kweli.

“Sijawahi kuona mtu muongo kama CAG, Jeshi la Polisi hakuna sare hewa. Ninaomba maofisa wa ofisi ya CAG twende nao stoo wakaone sare mpya za jeshi la polisi. Kama nasema uongo nitajivua nguo na ninaweka uwaziri wangu rehani” Kangi Lugola - Waziri Mambo ya Ndani

Waziri Lugola aliuweka rehani uwaziri wake huo, wakati akijibu hoja za Wabunge alipokuwa akihitimisha mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/2020 ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Amesema sare hizo ziko katika makontena



Hao Ndio mawaziri wa kutupeleka uchumi wa kati wa viwanda Kweli?????!!!!! Hana wasaidizi? Hana washauri???
 
Waziri Kangi Lugora Jana amemtuhumu CAG kuwa ni muongo kwa kuandika taarifa ya kutokununuliwa kwa sare za jeshi la Polisi ilihali fedha zilishatolewa

Video hiyo chini inaonyesha jambo hilo lilishazungumzwa hata na Rais mwaka 2017

Kwa hiyo hapa muongo ni nani kati ya watu hawa watatu

Rais na CAG wanasema hazijanunuliwa na fedha zimeliwa

Kangi anasema ni uongo na sare zimenunuliwa na kama hazipo atavua nguo hadharani

Nasubiri kuona
 
Back
Top Bottom