chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Mbunge Kangi Lugola wa CCM amekosoa bajeti ya mwaka huu kwamba ni ya kukumbatia mafisadi kwa kuwa wametengea ofisi ya CAG pesa kidogo, amesema bajeti ya mwaka jana ilikuwa ni bilioni 74 lakini akashangaa mwaka huu kutengewa bilioni 44 tu
Amekosoa vikali ofisi ya CAG kubaniwa bajeti na kudai kuwa mafisadi hawatatambulika kwa kuwa CAG amenyimwa fedha na Magufuli hatapata majipu ya kutumbua kwa kuwa mtambua majipu ameminywa.