Kangi Lugola aripoti ofisi za TAKUKURU Dodoma kwa mahojiano

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
IMG-20200131-WA0006.jpg


#HABARIZAHIVIPUNDE:Aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola asubuhi hii, ameitikia wito wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma, ambapo amewasili katika ofisi za TAKUKURU saa 1.24.

=====

Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) makao makuu jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa.

Lugola amefika katika ofisi hizo leo Ijumaa Januari 30, 2020 saa 1.24 asubuhi akiwa katika gari ndogo aina ya Klugger rangi nyeusi na hakuingia nayo ndani ya geti.

Akiwa amevalialia kaunda suti nyeusi huku mkono wa kulia akiwa ameshikaiIlani ya CCM na mkoba mweusi, alionekana mwenye kujiamini zaidi na akielekea moja kwa moja eneo la mapokezi ndani ya jengo hilo lililoko mtaa wa Jamhuri.

Moja ya maofisa wa Takukuru alimuongoza kuingia ndani ya jengo ambako alikwenda kukaa eneo la mapokezi mahali walipokuwa wamekaa waandishi na wakatakiwa kumpisha.
"Hata ninyi mpo huku, oh hata wewe nawe upo, haya hamjambo, habari zenu," alisalimia Lugola akipunga mkono uliobeba ilani ya CCM.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru amesema baada ya Lugola kuhojiwa, saa 3.30 atahojiwa aliyekuwa Kamishina wa Zimamoto, Thobias Andengenye, saa 8.00 atahojiwa aliyekuwa Katibu Mkuu, Jakob Kingu ambaye sasa ni balozi na saa 12 jioni atahojiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.

Kuhojiwa kwa watumishi hao ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu mkataba tata walioingia katika manunuzi ya vifaa vya zimamoto.

Pia soma: Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na Ramadhani Kailima watinga TAKUKURU kuhojiwa
 
View attachment 1341731

#HABARIZAHIVIPUNDE:Aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola asubuhi hii, ameitikia wito wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma, ambapo amewasili katika ofisi za TAKUKURU saa 1.24.
Kwa hiyo anapoonyesha katiba ya CCM anataka kutupa ujumbe gani?, kwamba CCM imejaa Wala rushwa kwa hiyo watamtetea mlarushwa mwenzao
 
Back
Top Bottom