Kangi Lugola amwashia moto Waziri mkuu bungeni, anataka afukuzwe kazi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Ni Kafulila na Kangi Lugola asemwa kuwa ni mzigo na kauli za tunafuatilia, yanazungumzika, tutaangalia, tupo kwenye mchakato, nimeshaagiza.

Na kwa ujumla hayafanyiwi kazi kwa maana hiyo haeshimiki na anadharaulika sana kwa maana hiyo ni mzigo.
 
Mh.Kangi lugola akiendelea kuchangia taarifa za kamati za oversite,amemshauri rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi waziri mkuu wa Tanzania kama anaitakia mema nchi hii.kasema Pinda ameshindwa kuwajibika mwanzo hadi mwisho.my op.Wabunge wa ccm sasa wanakumbuka shuka kumekucha.
 
Mbunge wa Mwibara (CCM) Kangi Lugoda ameshauri Rais JK awatimue kazi mara moja Waziri Mkuu Pinda na Waziri wa TAMISEMI Hawa Ghasia kutokana na uzembe kazini ukiwemo wa kuachia sh. Bil. 644 za wafadhili zikiwa ni msaada kwa TAMISEMI kutafunwa kifisadi na hakuna hatua zimechuliwa! Amehoji udhaifu mwingi ulioko katika TAMISEMI ikiwemo kuendelea kulipwa mishahara kwa watumishi feki na wafu. Amehoji upole wa Pinda akisema upole hauna dawa wala tiba, na akahoji ni hadi lini Bunge litaendelea kushauri? Ametaka mtindo wa Timuatimua uwe adapted na JK mara moja ili kuweka mambo sawa!
 
hata me sikuamini kuwa na mbunge wa ccm anatamka hivyo,hasa aliposema umasikini wa nchi yetu,mchawi wetu ni mmoja tu,mh waziri mkuu,kwakweli ka wabunge wetu wote wangeachana na siasa za zidumu fikra safi za mwenyekiti wa chama na kuanza kuwachana live mawaziri wazembe tungefika mbali.
 
Duuh! Nahisi kama watanzania wanaweza kuingia kichwa kichwa kushangilia Pinda kutimuliwa(japo ni sawa kwa sababu ni dhaifu) bila wao kutambua uhalisia wa mambo, lakini yote kwa yote tusubirie tuone Mwisho wake.
 
Mkuu ni pesa gani? za Wafadhili.....ni zile zilizotolewa na Wolrd Bank kwa ajili ya kuboresha makazi yaliyojengwa kiholela Dar hasa Kata ya kiwalani Minazi Mirefu? Aiiiiyaa.........Sasa naanza kuamini ya kuwa Minazi mirefu Kiwalani inatakiwa iwe sehemu ya makumbusho ili wageni ambao hawapata kuiona Dar es salaam miaka ya 1970 ilionekanaje? basi wataletwa Minazi Mirefu Kiwalani.......Mfadhili katoa pesa jengeni Minazi Mirefu nyinyi hamtaki tena Munamuongopea kuwa mtajenga wakati si kweli......si mungemuachia tu pesa zake kama kweli ni hizo sitawaamini tena H/mashauri ya Ilala.............
 
Ushauri mzuri,lakini najenga shaka na serikali yetu 'sikivu' kama itaona sababu ya kuwajibishana.
 
Huyu jamaa CCM sio mahali pake na nuona mlango wake wa kurejea mjengoni kupitia CCM ukizidi kufungwa..
 
Mkuu ni pesa gani? za Wafadhili.....ni zile zilizotolewa na Wolrd Bank kwa ajili ya kuboresha makazi yaliyojengwa kiholela Dar hasa Kata ya kiwalani Minazi Mirefu? Aiiiiyaa.........Sasa naanza kuamini ya kuwa Minazi mirefu Kiwalani inatakiwa iwe sehemu ya makumbusho ili wageni ambao hawapata kuiona Dar es salaam miaka ya 1970 ilionekanaje? basi wataletwa Minazi Mirefu Kiwalani.......Mfadhili katoa pesa jengeni Minazi Mirefu nyinyi hamtaki tena Munamuongopea kuwa mtajenga wakati si kweli......si mungemuachia tu pesa zake kama kweli ni hizo sitawaamini tena H/mashauri ya Ilala.............

Hakufafanua sana ni fungu lipi hasa, lakini alikuwa akiizungumzia Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali. Alionyesha hasira zake dhidi ya 'usoft' wa Pinda kwa kusema hata hapo Bungeni kulikuwa na mawaziri wanne na manaibu mawaziri wawili tu leo asubuhi, ikiwa ni uthibitisho wa wazi kwamba mawaziri hawamheshimu wala hawamjali akiwa ndio kiongozi wa masuala ya serikali Bungeni!
 
Jamani mimi huona kigeugeu pale Maccm yanapoikosoa serekali yao tukufu. Yapo mawili, huyo mpiga debe anatamani akumbukwe na JK kabla hajamaliza mda wake. Ampe uwaziri hata kwa siku moja tu au anatamani awe upinzani aikosoe hiyo serekali kwani anaona alipo kugumu na kumeelemewa. Ni maoni yangu tu
 
Back
Top Bottom