Mh.Kangi lugola akiendelea kuchangia taarifa za kamati za oversite,amemshauri rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi waziri mkuu wa Tanzania kama anaitakia mema nchi hii.kasema Pinda ameshindwa kuwajibika mwanzo hadi mwisho.my op.Wabunge wa ccm sasa wanakumbuka shuka kumekucha.
Mbunge wa Mwibara (CCM) Kangi Lugoda ameshauri Rais JK awatimue kazi mara moja Waziri Mkuu Pinda na Waziri wa TAMISEMI Hawa Ghasia kutokana na uzembe kazini ukiwemo wa kuachia sh. Bil. 644 za wafadhili zikiwa ni msaada kwa TAMISEMI kutafunwa kifisadi na hakuna hatua zimechuliwa! Amehoji udhaifu mwingi ulioko katika TAMISEMI ikiwemo kuendelea kulipwa mishahara kwa watumishi feki na wafu. Amehoji upole wa Pinda akisema upole hauna dawa wala tiba, na akahoji ni hadi lini Bunge litaendelea kushauri? Ametaka mtindo wa Timuatimua uwe adapted na JK mara moja ili kuweka mambo sawa!
KANGI ni moja ya wabunge wachache wenye akiri timamu wanaopatikana CCM.Tatizo cyo MIZENGO tu ila ni SYSTEM yote ya Chama tawala ilishaoza miaka 25 Iliyopita.
Hakufafanua sana ni fungu lipi hasa, lakini alikuwa akiizungumzia Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali. Alionyesha hasira zake dhidi ya 'usoft' wa Pinda kwa kusema hata hapo Bungeni kulikuwa na mawaziri wanne na manaibu mawaziri wawili tu leo asubuhi, ikiwa ni uthibitisho wa wazi kwamba mawaziri hawamheshimu wala hawamjali akiwa ndio kiongozi wa masuala ya serikali Bungeni!