Kangi Lugola amuweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects

Aidha, amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini
--------

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni mhandisi mshauri wa kampuni ya Y&P Architects, Benjamin Kasiga ambaye anadaiwa kutoa taarifa ya uongo kwa waziri huyo kuhusu ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji mkoani humo.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi Agosti 27, 2018 wakati Lugola na katibu mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu walipofika katika kituo hicho kwa kushtukiza.

Lugola alipokuwa anakwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu kama polisi walitekeleza agizo lake.

Hata hivyo, Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi, hivyo akamuuliza kamanda wa polisi wa mkoa huo, Lucas Mkondya sababu za kutotekelezwa agizo lake.

“Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndiyo madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Polisi na hii ndiyo tabia yenu. Najua ndiyo mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi,” alihoji Lugola.

“RPC hawa polisi wako wanafanya nini? OCS njoo hapa, kwa nini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” aliamuru Lugola.

Hata hivyo, Mkondya alimweleza Lugola kuwa polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.

Chanzo: Mwananchi
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects

Aidha, amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini

Nadhani hapo ulimaanisha Central Police, kwa hiyo ukaona uweke neno "Kati" :D:D:D:D:D:D:D
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects

Aidha, amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini
Weka picha tafadhali, wengine hatujawahi kuona buibui amenaswa na utando wa buibui
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects

Aidha, amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini
Kwa kosa gani
 
kwa awamu I will not be surprised if the whole incident is scripted. As we speak huyo anaesadikika kuwekwa ndani yupo kwenye kiyoyozi anakunywa juice.
Kama ni kweli basi hongera zake kwa kuishi kulingana na kauli zake.
 
vitendo vya kiajabu mno,political principal wa waizara ana uwezo wa kumtia ndani polisi!!kazi kweli kweli yaani nigekuwa na uwezo ningempeleka huyu waziri kwa ziara ya kimafunzo pale Rwanda na Botswana ili akajifunze jinsi polisi wao wanavyofanya kazi kwa misingi ya wajibu wa kisheria.
 
Back
Top Bottom