Kangi Lugola amezionya asasi zisizo za kiserikali ambazo zinatumia mwanya wa kukosoa Serikali kwa kuitukana na kupotosha jamii

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amezionya asasi zisizo za kiserikali ambazo zinatumia mwanya wa kukosoa serikali kwa kuitukana na kupotosha jamii.

Lugola alitoa onyo hilo jana, alipokuwa akizindua Ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mkoani Dodoma na kampeni ya miaka 25 ya kituo hicho pamoja na uzinduzi wa tuzo ya Majimaji ambayo hutolewa kwa mtu ambaye ametoa mchango mkubwa wa kisheria katika jamii.

Alisema siku za hivi karibuni serikali imebaini kuwapo kwa asasi zisizo za kiserikali ambazo zinatumia mwanya huo kukosoa serikali, lakini badala ya kukosoa wamekuwa wakiitukana.

“Wanaenda mbali zaidi kwa kuipotosha jamii kwa kusema serikali ya awamu ya tano haijafanya kitu, uanaharakati wa aina hii ndani ya asasi zisizo za kiserikali ni uanaharakati usioitendea haki serikali, kwani wananchi wameshuhudia serikali ikijenga miundombinu mingi ya barabara, madaraja ikisomesha wanafunzi bure,” alisema.

Alisema pia serikali inahakikisha misingi ya demokrasia na utawala wa sheria vinazingatiwa, hivyo si vyema kuwapotosha Watanzania.

“Kwa hiyo sio vyema wala busara kuwaambia Watanzania serikali haijafanya kitu ilhali watu wanaona na huu ni upotoshaji,” alisema.

Aidha, alisema wamebaini kwamba inapotokea haki kuminywa ndipo milipuko ya kwamba kuna kuvunjika haki ya binadamu hutokea.

“Rai kwa kituo mwendelee kufanya kazi kwa weledi bidii na moyo wa kujituma ili kuhakikisha Watanzania wenye shida mbalimbali wanafikiwa na kutatuliwa shida zao kwa misingi ya sheria na taratibu za nchi na haki inaambatana na wajibu, hivyo ni vyema tunavyohubiri haki za binadamu, tuhubiri pia na wajibu wa kila raia,” alisema.

Kangi alisema anatamani siku moja lianzishwe shirika lisilo la kiserikali linalohubiri na kutetea suala la wajibu kikatiba.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, alisema kituo hicho kitahakikisha mipango ya serikali inatekelezwa kwa urahisi kwa kuwaandaa wananchi kutambua wajibu wao.

“Tunaamini kwamba jamii inayoheshimu na kulinda haki za binadamau pia itaheshimu wajibu na kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza amani na ushirikiano wa umoja wa kitaifa,” alisema.

Alisema kituo hicho kinaadhimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwake na kimeunga mkono jitihada za serikali za kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kwa kufungua ofisi yake jijini humo.
 
Hata Serikalli ya waroma enzi za Yesu Kristo ilikosolewa sasa itakuwa hii yenu wajemeni?
 
Siku watakapo ifungia Jamii Forums, watasababisha wananchi wengi tuwe mateja maofisini na majumbani mwetu.

Maana ndiyo media pekee ambayo tunaweza kutolea hisia zetu za kweli, tofauti kabisa na huko kwingine.

Mungu aiepushie mbali Jf dhidi ya dhuluma ya hawa miungu watu wanaotaka kusifiwa na kuabudiwa bila sababu za msingi, usiku na mchana.
 
Hivi watanzania tumekuwa wajinga? Ina maana hatuna macho na masikio? ...Swali la kizushi? Hivi hili angalizo linatakiwa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya habari au waziri wa mambo ya ndani?
 
Watoe muongozo kuwa maneno gani ni matusi ya kuitukana serikali!

Kuna yule aliyemtolea Kabudi mfano kuwa huwa anawaambia pumbavu nyingi tu,neno hilo likitumika kuitambulisha serikali ni jinai pia?!!
 
Back
Top Bottom