nuruyamnyonge
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 4,390
- 2,163
Amani iwe kwenu!
Yule mbunge machachari wa jimbo la mwibara mzee wa kininja,mh.spika;" niruhusu nivae kininja" ili niwatumbue mafisadi wa escrow vizuri bila kuwaonea aibu, naye amejikuta kwenye tuhuma nzito za kutumbuliwa majipu.
Mh.Kangi Lugola amekumbwa na kashifa kubwa majuzi tu, kashifa ya kuomba rushwa na hatimae kuburuzwa mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam.
Jana Kangi alishindwa kutokea mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili dhidi ya ufisadi wa ardhi kwa raia wa jimbo lake. Maswali ni mengi kuliko majibu, inawezekanaje mbunge akashindwa kuhudhuria kesi inayomkabili mahakamani wakati taarifa za wito alipelekewa mara mbili?
Nianze kwa kusema hivi! Hapa sileti majungu nawaletea ukweli usiotiliwa shaka, ukweli wa kiwango kilichotukuka mbele ya mwenyezi Mungu na viumbe vyake vyote. Kangi ameidharau mahakama na wapiga kura wake. Kama jambo hili litachokonolewa vizuri tutawajua wabunge wetu ni wezi na wala rushwa wakubwa wakijifisha kwenye mgongo wa maskini kuwasaidia chumvi na sabuni wanapowatembelea.
Nimeamua kujitolea ili nitoe mchango wangu kwa raia ili mbunge achukuliwe hatua za kisheria dhidi ya huu ufisadi wa kutaka kujimilikisha mali kinyume cha sheria.
Iko hivi, kangi anawatolea vitisho wamiliki wa ardhi tangu mwaka 2005 kwa madai kwamba hilo ni eneo lake. Nani kati ya miongoni mwa familia alimuuzia hasemi. Vitisho vimezidi kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Mgogoro umepelekwa mahakamani ili ukweli ujulikane lakini mbunge hajitokezi mahakamani. Anaogopa nini? Anawatuma wapambe wake ikafikia hatua ya kuondoa mipaka ya asili(katani) lakini bado anaikimbia mahakama.
Wito wangu kwa Kangi (Mbunge) jitokeze kwenye huu Uzi wangu ukanushe Kama nakusingizia au ni majungu. Tarehe 21.03.2016 hukwenda mahakani. Tar.11.04.2016 hukufika mahakamani, haya Tar.04.05.2016 itakuwaje?
Karibuni kwa kuchangia.