Kangi Lugola aagiza NEMC kumpa maelezo kwanini nyumba ya Lwakatare haijabomolewa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Lugola ametoa muda kwa NEMC hadi leo Alhamisi Oktoba 26, 2017 saa 10:00 jioni awe amepata taarifa ili aweze kutoa uamuzi iwapo ibomolewe au la.

=======

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola ameagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kufikisha mezani kwake maelezo ni kwa nini nyumba ya mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) haijabomolewa.

Lugola ametoa muda kwa Nemc hadi kesho Alhamisi Oktoba 26,2017 saa 10:00 jioni awe amepata taarifa ya maandishi ili aweze kutoa uamuzi iwapo ibomolewe au la.

Naibu waziri ametoa agizo hilo leo Jumatano Oktoba 25,2017 wakati Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipokutana na watendaji wa Nemc.

Lugola amefikia uamuzi huo baada ya Nemc katika taarifa yake kueleza Serikali imeshindwa kuivunja nyumba hiyo kutokana na zuio lililopelekwa mahakamani na Mchungaji Rwakatare tangu mwaka 2012.

Nemc imesema kesi ikiisha na uamuzi kutolewa hakutakuwa na shaka wala kigugumizi katika kuivunja nyumba hiyo.

Ka kauli hiyo, Naibu Waziri Lugola amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba, hatima ya jengo hilo lazima ijulikane mapema ili kuondoa sitofahamu iliyopo.

“Rais Magufuli ameniteua kufanya kazi hii na anajua kwa nini alinichagua mimi. Naamini anajua uwezo wangu na utendaji kazi wangu, siko tayari mtu wa nafasi yoyote kuniangusha na kunifanya nishindwe kutimiza malengo yangu. Sitaki migongano ya aina yoyote inayoweza kuniangusha, hakuna jiwe litakaloachwa kusalia juu ya jiwe,” amesema.

Awali, wajumbe wa kamati walihoji uhalali wa nyumba hiyo kubaki bila kuguswa licha ya kujengwa eneo lisiloruhusiwa kisheria.

Nyumba hiyo ipo mtaa wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambayo iliamriwa kubomolewa lakini hilo halikufanyika kutokana na Rwakatare kuweka zuio mahakamani.

Akizungumzia suala hilo, mjumbe wa kamati, Khatibu Haji (Konde -CUF) amesema kumekuwa na hali ya kulindana katika jengo hilo, huku Serikali ikiendelea kuwaonea wanyonge.

“Tunashuhudia Watanzania wanyonge wengi wakipoteza makazi yao na kuishi kwa mahangaiko baada ya kuangushiwa nyumba zao, lakini hakuna kitu chochote kinachoendelea kuhusu nyumba ya Mchungaji Rwakatare na jambo hili linaibuliwa na kuzimwa kuna nini huko,” amehoji Khatibu.

Amesema haileti picha nzuri kwa Serikali kuonyesha inawaonea wanyonge na kuwatetea wenye uwezo jambo linalosababisha kuwagawa watu kwa matabaka.

Khatibu hakuwa peke yake, Martha Mlata (Viti Maalumu -CCM) alitaka hatua kali zichukuliwe kwa waliomruhusu Rwakatare kujenga katika eneo lisiloruhusiwa kisheria.

“Huu ni uonevu ambao haupaswi kuvumiliwa. Macho na masikio ya Watanzania yamechoka kusikia nyumba za wanyonge zikivunjwa lakini Serikali inaendelea kulinda hekalu la mtu mmoja ambalo limejengwa mahali pasipohusika. Haikubaliki hata kidogo, kuna nini katika nyumba ya Mchungaji Rwakatare,” amehoji Gimbi Masaba (Viti Maalumu -Chadema).
 
Kweli tupu....kuna watu wana "makaratasi" ya mahakama lakini nyumba zao zimebomolewa. Au huyo Mch. ni zuio la mahakama tofauti?
 
Kule kimara mbona hawakujiuliza hivi badala yake walibomoa haraka haraka pamoja na wengine walikuwa na kesi zinaendelea mahakamani na hazikuwa zimetolewa maamuzi!?
 
siku hizi mahakama ni obsolete, zuio la mahakama halionekani kua "sababu" ya msingi mbele ya "naibu waziri" au kiongozi mwingine yeyote aliyeteuliwa na raisi. Jaji mkuu na idara yake wametiwa mfukoni mwa raisi, shame
 
Wafike mwisho basi na hilo sakata lao huyo mama alale kwa amani maana kila siku nyumba nyumba si waziri alisema hawatavunjiwa hata kama maeneo waliyojenga sio rasmi au huyu mama ye ahusiki
 
Ndo tatizo la sheria za nchi yaan zina macho na zinaona vzuri na kutambua nyumba hii ni ya nani na ole waki ijue hii nyumba ni ya pambafu wa mbagala hapo ndo utajuta
 
Ukibomoa nymba hiyo usisahau kubomoa na siikirifu utekelezaji uende sambamba mh.waziri ili lisiwepo jiwe juu ya jiwe
 
Jibu la swali lake mbona ni simple tu, huyu haijui vizuri ccm watamNAPElize shauri yake we mwache tu
 
Lugola, kazi siyo kubomoa, kuna mengi zaidi ya kufanya kwa manufaa ya wengi!
Hili liwe secondary, usifanye kama bosi wako anavyofanya!
mimi nilitaka wajiulize kwa nini mpaka leo eneo x halina maji ya bomba au eneo y umeme bado ?nataka maelezo kwa nini eneo z daraja au barabara haijajengwa?
sio hizi kwa nini mbowe rwakatare sumaye mwajuma ndala ndevu mzee dipinde hajabomolewa?vipaumbele vya ajabu sana viongozi wetu wamekuja navyo!
 
Hii nyumba ya Mchungaji wa CCM iliombewa sana tena maombi mazito hadi yenyewe ikasogea mbali kabisa na mipaka ya NEMC. Walipokwenda kutaka kuivunja wakakuta imesogea umbali unaotakiwa. Wakatangaza kuwa nyumba imesogea mahali salama. Msiganye mchezo na maombi ya wachungaji wa CCM
 
Mbona hajazungumzia ile ya ana mkp, iliwekewa x ukuta ukabomolewa ukajengwa mwingine kupoteza ushahidi!
 
kick za mawazili wetu alipoingia ofisini baada ya kuteuliwa nyumba ya rwekatare ndio kipaumbele chake
 
Kimara,Mbezi, luguruni, kibamba na maili moja kuulikuwa mazuio mengi ya mahakama LAKINI HAWAKUJALI HILO WALIBOMOA TU. kusema kweli inauma sana sana kama mahakama zinapuuzwa kaisi hicho na zenyewe zimekaa kimya tu.
 
Back
Top Bottom