Kangi Lugola aagiza kuundwa tume ya Kuchunguza Polisi kumpiga na kumuingizia chupa sehemu za siri Juma Yahya

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuunda Kamati Maalumu itakayochunguza tukio la kijana Musa Yahya ambaye anadai kupigwa na Polisi nakuingiziwa chupa sehemu za siri akiwa katika Kituo cha Polisi loliondo nakupelekea mguu wake kuoza akiwa kituoni.

Tukio hilo la kijana huyo, Mussa Yahya ambaye alikuwa na wenzake watano, wanatuhumiwa kuiba vitu vya wageni katika kambi ya kitalii iliyopo wilayani Ngorongoro Mkoani humo, na kupelekea kushikiliwa na askari polisi ambao wanalalamikiwa kuwapiga na kuwafanyia vitendo vya kikatili vilivyopelekea kuoza mguu wake wa kushoto, na kumfanya atembee kwa shida baada ya nyama za miguu kukatwa.

Akiwa katika ziara Wilayani Longido, na kufanya mkutano wa hadhara mjini Namanga, kijana huyo ambaye aliambatana na kaka yake, alimweleza Waziri Lugola katika mkutano huo, alipigwa na kuteswa kwa siku tisa huku yeye na wenzake wakiwa wamefungwa mikono na miguu huku wakiwa wanapigwa katika nyayo za miguu hadi kupelekea mguu wake kuoza.

“Nikiwa mimi na wenzangu, baada ya kuteswa na askari hao, tukapelekwa hospitali, na baada ya vipimo, ndipo mimi nikaambiwa na madaktari mguu wangu umeoza na wakakata nyama ya mguu wangu, nimepata mateso sana, pia walinifanyia ukatili sehemu za siri kwa kuniingizia chupa,” alisema Yahya.

Kufuatia malalamiko hayo pamoja na kaka yake Omary Yahya ambaye aliambatana naye katika mkutano huo wa Namanga, Waziri Lugola alimaliza ziara Wilayani Longido na kuelekea Wilaya ya Karatu na baadaye akafika Wilaya ya Ngorongoro mahali ambapo tukio hilo la kupigwa kwa kijana huyo lilitokea.

Akizungumza jana na mamia ya wananchi mjini Waso, Loliondo, Wilayani Ngorongoro, Lugola alisema kutokana kwa tukio hilo la kikatili lililotokea wilayani hapo, alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuhakikisha unafanyika uchunguzi huru ili haki itendeke kwani wananchi wamelalamika juu ya tukio hilo.

“Nilipata malalamiko haya nikiwa Namanga kutoka kwa aliyejeruhiwa, na nilimuona majeraha yake jinsi alivyokuwa ameteswa, hivyo basi ili nijue ukweli zaidi wa tukio hili, namuagiza Katibu Mkuu aunde Kamati kwa ajili ya kuchunguza kwa kina kuhusu tukio ili,” alisema Lugola huku akishangiliwa na mamia ya wananchi walihudhurika mkutano huo.

Lugola aliongeza kuwa, “Tunataka haki itendeke katika tukio hilo na matokeo yake yawe hadharani kwani hatuwezi kulalamikiwa tukaaa kimya na hata wale askari wachache ambao sio waadilifu wananchi watambue kuwa Jeshi la Polisi ni jeshi ambalo linaajiri vijana waliopata mafunzo ya kiweledi, wamefundishwa jinsi ya kukamata wahalifu, matumizi yapi yatumike endapo mtuhumiwa ameshindwa kutii agizo la polisi, sio kutumia nguvu kiasi ambacho kinaleta taharuki katika jamii, Kamati hiyo italeta majibu sahihi kuhusiana na tukio hilo,” alisema Lugola.

Lugola alisema, alishatoa maagizo kuwa, mahali popote polisi wakikutana na jambazi lenye silaha ya moto lazima askari ajihami kwa kupambana na jambazi huyo mwenye silaha, ili askari huyo asiweze akaja kupoteza Maisha wakati anacho kitu cha kujihami.

Lugola alifafanua kuwa, kuna makosa mengine ya kawaida kama hilo lililotokea katika kambi ya watalii huku akisema askari hawaruhusiwi kutumia nguvu zilizopita kiasi ikiwa kuleta vifo au na kuwasabishia wananchi majeruhi ya kudumu, hivyo alilitaka Jeshi la Polisi nchini wasiendelee kutumia nguvu kupita kiasi katika kushughulika na wahalifu popote pale.

Akasisitiza kuwa, endapo askari yoyote atakayebainika kutumia nguvu kupita kiasi na kuleta madhara, hafai na lazima atamchukulia hatua.

Lugola amemaliza ziara yake Mkoa wa Arusha ambapo alitembelea Wilaya zote akiangalia utendaji kazi wa Taasisi zake pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa mara baada ya kuteuliwa kuwa Waziri, mwezi Julai mwaka jana.

Maagizo aliyoyatoa mara baada ya kuteuliwa, dhamana zitolewe saa 24, wananchi kutokubambikizwa kesi, pikipiki kuondolewa vituo vya polisi ambazo hazina sifa kuwepo katika vituo hivyo..
IMG_20190220_214205.jpeg

MY TAKE;

Ninja Kaanza vizuri. Tutegemee tume pia kuundwa kwa swala la Lissu, Mawazo, Gwanda na Ben Saanane. Miili ya kwenye Viroba coco beach, watu waliopotea Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) nk.

Kangi Lugola asionee Dagaaa bali aonee Kambale. Dagaa wamejifunza kwa Kambale kupiga watu risasi.
 
Haki inatendeka Tanzania
Nchi yetu bado majanga ni mengi?Mangapi ambayo waziri hayajui?Haya,asingeenda huko angejuaje?Ni sehemu ngapi ambapo kuna wahanga wengi lakini hawana pa kusemea?
Mfumo wa kipolisi nchi hii ni tatizo kubwa sana!
Na bado hapo Mkuu wa nchi anakazia hataki kusikia polisi anakamatwa akiwa kazini,sasa na hao walikuwa makazini!
 
Hayo maagizo ya mkuu nchi umeyatoa wapi?
Waziri anapita huko wilayani kupata mabaya na mazuri kwa uhalisia wake.
 
Polisi wakaguliwe n watumbuliwe halafu sheria ibadiliswe kila polisi lazima awe amesomea diploma ya sheria kabla ya kuajiriwa hiii itapunguza wahuni wa wafelia kupata kazi
 
Lugola is a toothless dog. Mpaka ma-RPC wanampuuza!

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuunda Kamati Maalumu itakayochunguza tukio la kijana Musa Yahya ambaye anadai kupigwa na Polisi nakuingiziwa chupa sehemu za siri akiwa katika Kituo cha Polisi loliondo nakupelekea mguu wake kuoza akiwa kituoni.

Tukio hilo la kijana huyo, Mussa Yahya ambaye alikuwa na wenzake watano, wanatuhumiwa kuiba vitu vya wageni katika kambi ya kitalii iliyopo wilayani Ngorongoro Mkoani humo, na kupelekea kushikiliwa na askari polisi ambao wanalalamikiwa kuwapiga na kuwafanyia vitendo vya kikatili vilivyopelekea kuoza mguu wake wa kushoto, na kumfanya atembee kwa shida baada ya nyama za miguu kukatwa.

Akiwa katika ziara Wilayani Longido, na kufanya mkutano wa hadhara mjini Namanga, kijana huyo ambaye aliambatana na kaka yake, alimweleza Waziri Lugola katika mkutano huo, alipigwa na kuteswa kwa siku tisa huku yeye na wenzake wakiwa wamefungwa mikono na miguu huku wakiwa wanapigwa katika nyayo za miguu hadi kupelekea mguu wake kuoza.

“Nikiwa mimi na wenzangu, baada ya kuteswa na askari hao, tukapelekwa hospitali, na baada ya vipimo, ndipo mimi nikaambiwa na madaktari mguu wangu umeoza na wakakata nyama ya mguu wangu, nimepata mateso sana, pia walinifanyia ukatili sehemu za siri kwa kuniingizia chupa,” alisema Yahya.

Kufuatia malalamiko hayo pamoja na kaka yake Omary Yahya ambaye aliambatana naye katika mkutano huo wa Namanga, Waziri Lugola alimaliza ziara Wilayani Longido na kuelekea Wilaya ya Karatu na baadaye akafika Wilaya ya Ngorongoro mahali ambapo tukio hilo la kupigwa kwa kijana huyo lilitokea.

Akizungumza jana na mamia ya wananchi mjini Waso, Loliondo, Wilayani Ngorongoro, Lugola alisema kutokana kwa tukio hilo la kikatili lililotokea wilayani hapo, alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuhakikisha unafanyika uchunguzi huru ili haki itendeke kwani wananchi wamelalamika juu ya tukio hilo.

“Nilipata malalamiko haya nikiwa Namanga kutoka kwa aliyejeruhiwa, na nilimuona majeraha yake jinsi alivyokuwa ameteswa, hivyo basi ili nijue ukweli zaidi wa tukio hili, namuagiza Katibu Mkuu aunde Kamati kwa ajili ya kuchunguza kwa kina kuhusu tukio ili,” alisema Lugola huku akishangiliwa na mamia ya wananchi walihudhurika mkutano huo.

Lugola aliongeza kuwa, “Tunataka haki itendeke katika tukio hilo na matokeo yake yawe hadharani kwani hatuwezi kulalamikiwa tukaaa kimya na hata wale askari wachache ambao sio waadilifu wananchi watambue kuwa Jeshi la Polisi ni jeshi ambalo linaajiri vijana waliopata mafunzo ya kiweledi, wamefundishwa jinsi ya kukamata wahalifu, matumizi yapi yatumike endapo mtuhumiwa ameshindwa kutii agizo la polisi, sio kutumia nguvu kiasi ambacho kinaleta taharuki katika jamii, Kamati hiyo italeta majibu sahihi kuhusiana na tukio hilo,” alisema Lugola.

Lugola alisema, alishatoa maagizo kuwa, mahali popote polisi wakikutana na jambazi lenye silaha ya moto lazima askari ajihami kwa kupambana na jambazi huyo mwenye silaha, ili askari huyo asiweze akaja kupoteza Maisha wakati anacho kitu cha kujihami.

Lugola alifafanua kuwa, kuna makosa mengine ya kawaida kama hilo lililotokea katika kambi ya watalii huku akisema askari hawaruhusiwi kutumia nguvu zilizopita kiasi ikiwa kuleta vifo au na kuwasabishia wananchi majeruhi ya kudumu, hivyo alilitaka Jeshi la Polisi nchini wasiendelee kutumia nguvu kupita kiasi katika kushughulika na wahalifu popote pale.

Akasisitiza kuwa, endapo askari yoyote atakayebainika kutumia nguvu kupita kiasi na kuleta madhara, hafai na lazima atamchukulia hatua.

Lugola amemaliza ziara yake Mkoa wa Arusha ambapo alitembelea Wilaya zote akiangalia utendaji kazi wa Taasisi zake pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa mara baada ya kuteuliwa kuwa Waziri, mwezi Julai mwaka jana.

Maagizo aliyoyatoa mara baada ya kuteuliwa, dhamana zitolewe saa 24, wananchi kutokubambikizwa kesi, pikipiki kuondolewa vituo vya polisi ambazo hazina sifa kuwepo katika vituo hivyo..
View attachment 1027633

MY TAKE;

Ninja Kaanza vizuri. Tutegemee tume pia kuundwa kwa swala la Lissu, Mawazo, Gwanda na Ben Saanane. Miili ya kwenye Viroba coco beach, watu waliopotea Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) nk.

Kangi Lugola asionee Dagaaa bali aonee Kambale. Dagaa wamejifunza kwa Kambale kupiga watu risasi.
Huyu waziri sio mzalendo katumwa na mabepari na anakiuka amri ya raisi
 
Uonevu wa polisi dhidi ya raia utakoma tu pale rais atakapotengua kauli yake ya kwamba 'askari lolote walifanyalo yuko nyuma yao' jingine aliwahi kuwaambia polisi 'hakuna urafiki na raia' kauli hizi za mkulu haya ndio matokea yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom