Kangi Lugola aagiza kuswekwa ndani mratibu wa mradi wa ufugaji samaki kwa ubadhirifu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Ukerewe. Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola ameagiza kuwekwa mahabusu mratibu wa mradi wa ufugaji samaki wilayani Ukerewe, Jackson Ndobeji kwa mahojiano kuhusu ubadhirifu na utekelezaji mradi chini ya kiwango.

Lugola ametoa agizo hilo leo Jumatano Januari 24,2018 baada ya kukagua mradi huo unaotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa gharama ya Sh317.4 milioni.

UNDP inafadhili miradi ya ufugaji samaki katika Kijiji cha Namagondo wilayani Ukerewe tangu mwaka 2014.

“Pamoja na mratibu kukamatwa, naagiza uchunguzi na hatua za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu katika mradi huu,” amesema Lugola.

Amesema ziara kwenye miradi mingine ya aina hiyo katika wilaya za Bahi na Kongwa mkoani Dodoma imebaini imetekelezwa chini ya kiwango licha ya kugharimu mamilioni ya fedha.

Awali, katibu wa kikundi cha Pambazuka chenye wanachama 13, Athanas Musiba alimweleza Lugola kuwa baadhi ya waliostahili kupokea fedha hawajapatiwa chochote kutoka timu ya uratibu.

Akizungumza kabla ya kushikiliwa na polisi, Ndobeji alidai ofisi yake imepokea Sh240 milioni zilizotumika kujenga mabwawa, nyumba ya mlinzi na matangi ya maji kwenye eneo la mradi.

Bila kutaja kiasi, alisema fedha zingine zimetumika kununua vifaa vya umeme jua kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya mradi.

Ndobeji amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuwasili Ukerewe wakati wowote na kwamba, wameomba fedha ili kukamilisha kazi iliyosalia.

Chanzo: Mwananchi
 
Kangi amekuwa OCD sasa hana jipya zaidi kamata kamata tu kweli jasiri haachi asili!!!
 
UKEREWE: Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola ameagiza kuwekwa mahabusu mratibu wa mradi wa ufugaji samaki wilayani Ukerewe, Jackson Ndobeji kwa mahojiano kuhusu ubadhirifu na utekelezaji mradi chini ya kiwango.

Lugola ametoa agizo hilo leo Jumatano Januari 24,2018 baada ya kukagua mradi huo unaotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa gharama ya Sh317.4 milioni.

UNDP inafadhili miradi ya ufugaji samaki katika Kijiji cha Namagondo wilayani Ukerewe tangu mwaka 2014.

“Pamoja na mratibu kukamatwa, naagiza uchunguzi na hatua za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu katika mradi huu,” amesema Lugola.

Amesema ziara kwenye miradi mingine ya aina hiyo katika wilaya za Bahi na Kongwa mkoani Dodoma imebaini imetekelezwa chini ya kiwango licha ya kugharimu mamilioni ya fedha.

Awali, katibu wa kikundi cha Pambazuka chenye wanachama 13, Athanas Musiba alimweleza Lugola kuwa baadhi ya waliostahili kupokea fedha hawajapatiwa chochote kutoka timu ya uratibu.

Akizungumza kabla ya kushikiliwa na polisi, Ndobeji alidai ofisi yake imepokea Sh240 milioni zilizotumika kujenga mabwawa, nyumba ya mlinzi na matangi ya maji kwenye eneo la mradi.

Bila kutaja kiasi, alisema fedha zingine zimetumika kununua vifaa vya umeme jua kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya mradi.

Ndobeji amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuwasili Ukerewe wakati wowote na kwamba, wameomba fedha ili kukamilisha kazi iliyosalia.

Mwananchi
 
Huko ndipo walipoambiwa marufuku kuvua samaki na kama hawaelewi watapambanishwa na mamba wa kwenye hifadhi?Sijui hii habari ni ya kweli?
 
Huyu mzee hana moral authority yoyote ya kumshika mla rushwa,maana yeye alishashikwa live kabisa!!

Hii serikali ya double standards!
 
Back
Top Bottom