Kangi angalau alijaribu kuwadhibiti ST, huyu Simbachawene hamna kitu labda mengine!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,785
Kama wewe ni mtumiaji na msafiri utakubaliana na mimi kwamba wavunjaji wakubwa wa Sheria za barabarani ni Serikali, magari ya ST hayafwati Sheria zozote, hayasimami kwenye taa, yanatanua, huko kwenye kibao cha 50 km/saa wanakwenda wanavyotaka, angalau Waziri aliyepita alikuwa anadili nao lakini huyu wa sasa hivi labda anafanya vizuri kwenye mambo mengine hilo silijui kjn kwenye kudhibiti magari ya ST barabarani hakuna kitu anafanya, sijui kwa nini Raisi Magufuli huwa Mawaziri wazuri anawapotezea, I mean huyu wa sasa anafanya nini sasa hapo Wizarani.

MH. KANGI LUGOLA "NINJA"

"Madereva wa viongozi wa serikali watakao sababisha ajali kwa kisingizio cha kuambiwa kuongeza speed na viongozi wa serikali kipindi wanawaendesha kuchukuliwa hatua kali za kisheria"

Ni kauli ya waziri wa mambo ya ndani mh.kangi lugola NINJA
 
Kwako mleta mada.

Salaamu.

Rejea post yako ambayo ni ya kwanza ya uzi huu.

Mkuu, umejaribu kuwasiliana na Mheshimiwa Waziri Simbachawene kwa mawasiliano yake binafsi juu ya dukuduku lako hili kabla ya kupandisha uzi wako huu!? Jibu kama ni ndiyo, tupe mrejesho wa alichokisema Mheshimiwa Waziri.

Natanguliza shukrani kwa majibu yako.
 
hiyo siyo kazi ya waziri bana.

mbali na kwamba huyu wa sasa battery low,ila bado hapo utakuwa unamuonea.

ST mziache tu jamani,kama una nafasi nzuri ya kuzipisha zipishe tu maisha yaendelee,usiziige,usizivimbie,wala usizichomekee.
 
Tuchape Kazi Tu
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Alisema Wakati Anawaapisha Mawaziri
Nendeni Mkafanye Kazi, Kaamueni Hata Kama Unakosea Ni Bora Kuliko Kutokuamua Lolote

Mkuu Akishauri Ni Amri, Yaani Tanzania Yote
Hao Nao Wanafanya Kama Maagizo
 
hiyo siyo kazi ya waziri bana.

mbali na kwamba huyu wa sasa battery low,ila bado hapo utakuwa unamuonea.

ST mziache tu jamani,kama una nafasi nzuri ya kuzipisha zipishe tu maisha yaendelee,usiziige,usizivimbie,wala usizichomekee.

Hizo ST kwa sasa ziko kwenye serikali yenye kiburi cha madaraka?
 
Kangi lugola alikuwa mzuri sana
Lugola alikuwa na mapungufu yake kiasi lakini kwenye kero za barabarani alikuwa smart sana na hasa hilo la magari STK, PT, UT, SU ,JW, MT na wenzao Namba za ubalozi, UN nk hutanua hovyo hovyo barabarani hupita kwenye barabara ya mwendo kasi kihuni huni kuyabuguzi mabasi ya mwendo kasi, kutengeneza foleni kubwa baada ya kutanua barabarani hovyo hovyo, mkuu wa Trafiki mpya bado muoga muoga kashindwa kukaa na waziri simbachawene wapange mpango mkakati kupiga marufuku Magari ya Serikali kutanua barabarani
 
hiyo siyo kazi ya waziri bana.

mbali na kwamba huyu wa sasa battery low,ila bado hapo utakuwa unamuonea.

ST mziache tu jamani,kama una nafasi nzuri ya kuzipisha zipishe tu maisha yaendelee,usiziige,usizivimbie,wala usizichomekee.
naunga mkono hoja.zile ni mashine za kazi.wakuu unakuta wanawah vikao muhim na alipotoka pia katoka katika majukumu muhimu.ndio mana dereva anakamua mashine kuwahi.ndio mana ni profeshno.acheni zipige kiatu. Ili mradi suka anakua makin sasa mashine hujuiiuliz kwa nini ni v8? mana yake ipo.kikaz zaid.acheni gari ziende kikaz zaidi
 
Gari za ubalozi hutanua huvunja Sheria wakati mwingine Balozi yupo ndani ya hiyo Gari, ndipo ushangae sasa mwakilishi wa ubalozi anavunja Sheria makusudi na hachukuliwi hatua yeyote, Sheria za barabarani za Tanzania ni za kibaguzi zinamtesa Dereva wa magari ya kawaida kuliko Dereva wa Gari la Serikali
 
Back
Top Bottom