Kanga ya mwanafunzi sebuleni imezua balaa kwenye ndoa

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Salaam kwenu

Jana jioni nilitembelewa na mabinti wawili ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.

Ujio wa mabinti hawa ulitokana na kuagizwa na Kaka wa mmoja wabinti hawa waniletee bahasha iliyokuwa na documents flani ndani.Tuseme binti mmoja alikuwa kamsindikiza mwenzake.

Walipokuja nilikuwa nje nafanya shughuli flani hvy nikawasihi waingie sebuleni wanisubiri kwani nilitakiwa kuzikagua hizo nyaraka kabla hawajaondoka.
Kwenye TV nilikuwa nimeweka movie ambayo waliipenda hivyo wakazama Kwenye kuitazama.

Mimi nilipoingia nikawakuta wanaangalia movie sikutaka kuwasumbua badala yake nikachukua Ile bahasha iliyokuwa mezani nakujiridhisha.

Muda ulienda kagiza kakaanza kuingia so ikabidi watoto wale waage nakuondoka.Nilifunga mlango nikawasindikiza kdg ambapo nilipoachan nao niliamua kupitia mahali kubadilishana mawazo na jamaa zangu.
Niliporudi nilienda zangu kulala bila kukaa pale sebuleni.

Eebhanaeee, kumbe pale sebuleni binti mmoja alisahau kanga yake sehemu alipokuwa amekaa.Hili nimeligundua asubhi baada ya kutembelewa na mke wangu bila taarifa.Alikuwa kasafiri.

Hapa kimewaka kweli kweli, wife anadai nilikuwa namchepuko ndo umesahau kanga.Nimejaribu kumwelezea lakini haelewi kabisa. Njia pekee tuliyokubaliana nikuwaita wale watoto waje watoe ushahidi.Yule binti naye sijui imekuwaje kwani hadi saivi hajarudi kubeba kanga yake.

Nataman binti huyo atokee hata saivi japo lazima ajieleze vizuri kuwa ilikuaje akasahau kanga(nguo) sebuleni kwa watu.

Hili nalo mkaliangalie
Wasalaam!
 
Ameshatuma ujumbe huku
 
Attachments

  • IMG-20220812-WA0034.jpg
    IMG-20220812-WA0034.jpg
    75.4 KB · Views: 15
  • IMG-20220812-WA0035.jpg
    IMG-20220812-WA0035.jpg
    36.8 KB · Views: 20
Mambo mengi ya msingi hususani ndoa huharibika kwa dhana mbaya.......watu wengi huwaziana mabaya hivyo hupelekea kudhaniana mambo mabaya watu wengi hutoa hukumu kwa kudhania ubaya....... dhana mbaya ikikithiri hutengeneza uadui na chuki baina ya watu hao........lakini jambo ni kwamba tunaweza kuzifuta dhana mbaya kwenye mioyo ya wapendwa wetu kwa kukithiri kwa kutendeana mema kwani wema hufuta ubaya...........

Mkeo ana dhana mbaya juu yako ni jambo baya sana.....hatujui imetoa wapi ila wewe ndio unajua......safisha nafsi ya mkeo juu yako kwa kujirekebisha kile ambacho wewe unadhani kilimjengea kuwa na dhana mbaya juu yako.......
 
Sawa mkuu
 
Mwalimu umeletewa documents na wanafunzi wako wa kike, baada ya kuzihakiki unawasindika...

Kulikuwa na ulazima gani wa wewe kuwasindikiza??

Hili la khanga litaisha lenyewe baada ya huyo mwanafunzi kuirudia khanga yake.

Au huyo kaka (japo hujabainisha kama ni mwalimu mwenzio au rafiki yako) ndiye wa kumaliza tatizo
 
Hivi kumbe nimesema Mimi nimwalimu? Au kuwatambulisha hawa watoto kuwa niwanafunzi tayar naingia moja kw moja kama mwalimu? Au pengine bahasha na documents zake ni mwalimu tu anaeza kuwa nazo.
Kuhusu kuwasindikiza nilifanya hvy kwa kuwa namimi nilikuwa natoka.
Kingine nikwamba hadi wanatumwa kwangu muda huo means naaminika kuwa siwez kufany chcht kibaya kwao.
 
Back
Top Bottom