Kandoro ataka Sh 2 bilioni zilizochakachuliwa zirudishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kandoro ataka Sh 2 bilioni zilizochakachuliwa zirudishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 24, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na Pendo Fundisha, Mbeya MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ametoa miezi miwili kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kurudisha zaidi ya Sh bilioni mbili zilizotakiwa kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Fedha hizo zilipaswa kutumika katika idara ya elimu, afya, maji na kilimo, lakini hazikutumika, licha ya uongozi kueleza kuwa matumizi yake yalibadilishwa kutokana na sababu mbalimbali.

  Agizo hilo alilitoa mjini hapa jana, katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kinapitia majibu na hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi kinachomalizika.

  Alisema katika michanganuo ya matumizi hayo, inaonyesha zaidi ya Sh bilioni moja zilizotakiwa kutumika katika miradi hiyo hazikutumika na hazieleweki zilipo.

  Alisema kitendo cha halmashauri hiyo kudai fedha hizo zilikopwa na kutumika katika utawala pasipo kuomba ridhaa kutoka hazina ni makosa, kwa kuwa fedha yoyote ile ya Serikali inapaswa kufuata taratibu na misingi iliyojiwekea.

  “Mnadai kubadilisha matumizi ya fedha hizo, lakini mbona hata kwenye matumizi ya upande wa pili mliyotumia hayana viambatanisho, kwa kweli suala hili haliniingii akilini,” alisema Kandoro.

  Alisema hapo inaonyesha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha hizo ambazo malengo yake makubwa yalilenga kumkomboa mwananchi kwa kutekeleza miradi iliyokusudiwa kutumika.

  “Naomba fedha hizo zirudishwe ndani ya miezi miwili kama mlivyonieleza ili fedha hizi ziingizwe katika matumizi halisi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi,” alisema Kandoro.

  Aidha, aliwataka wakuu hao wa idara kutambua kuwa wakati wa kufuja fedha za Serikali haupo kwa kuwa Serikali haiwezi kukaa na kuangalia jinsi wananchi wanavyoteseka kwa kukosa mahitaji muhimu kama elimu, maji na afya.

  “Mimi sijui fedha hizo mtazitolea wapi, ila ninataka zirudishwe na kwa hili siwezi kukubali kwa kuwa siwezi kuwajibishwa kutokana na uzembe na tamaa za watendaji wachache ambao kazi yao kubwa ni kuangalia matumbo, huku jamii ikiendelea kuteseka,” alisema Kandoro.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mh hivi ile kashfa yake ya kujiuzia gari bei chee ili ishia wapi vile, huyu mteule Kandoro
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Kiinimacho....bilioni 1 zirudi ndani ya mwezi mmoja hapa Bongo?
   
 4. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Dah!!! anachokiongea mh. Kandolo ni ukweli, ila wasiwasi wangu ni kama ana kimaanisha hicho anachokiongea. Kawaida ya ccm, ni kuongea kile ambacho hakipo moyoni. UKIWA MBELE YA WANANCHI UNAJIFANYA HATA KUTOA MACHOZI, KUMBE MOYONI UNAWAAMBIA "WAJINGA NDO CHAKULA CHA WAJANJA" haya, ngoja tuone, tuombe Mwenyezi Mungu atujaalie uzima tuwepo hiyo miezi miwili ijayo kushuhudia kwa mara ya kwanza wezi wa ccm wanarudisha pesa walizoiba. katika kumbukumbu zangu, sikumbuki kama kuna pesa zilizowahi kurudishwa. ila nazikumbuka nyingi mno zilizoibwa, tena mchana kweupe huku VIYOYOZI VIKIWAPEPEA HAO WEZI. Duh!!! magamba bhana!!!
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Nafikiri anaropoka Kama mnywa wanzuki
   
 6. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Halo mbona unamsingizia Ustaadhi! Mwambieni Vule vichochoro alivyovifungua Dar alipokuwa Mkuu wa Mkoa Vimefungwa Tena
   
 7. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bilioni 2 ni nyingi kwa viongozi wa wilaya tu bila kuhusisha mamlaka za juu kama vile TAMISEMI - si ajabu TAMISEMI ilishafanya hamisha2 hapo kuvuruga mtirirko wa ushahidi.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Na hapo ni mbeya.. Fikiria halmashauri ngapi nchi hii zinachakachua fedha za walipa kodi??!!
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huko kwenye halmashauri ndiko wanakoibia hela za wananchi; mnakumbuka ile kesi ya watendaji wa halmashsuri ya wilaya ya Bagamoyo ambayo iliwagusa vigogo wa serikali akiwemo Celina Kombani? Mpaka hivi leo hakuna chochote kinachoendelea na wahusika wamepewa uhamisho akiwemo waziri wao!!
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inaelekea hawakumkumbuka kwenye mgao...
   
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  kabla ya bilioni 2 za mbarali kwanza tunataka bilioni 300 ziliko uswiss. Hatutaki maigizo.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Usanii mtupu unaendelea. Nani atamfunga nani hapa? Kitu cha kuangalia ni wewe na mimi tusivinje sheria maana watatufunga kweli. Hao wana siasa wao project yao ni kuitafuna nchi na kulindana kwa gharama yoyote ile.
   
Loading...