Kandarasi ya kulinda legacy, wafadhili wamechemsha?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,630
697,597
Hakuna pesa inayotosha ndio maana maisha yetu ni ya kutafuta pesa mpaka tunakufa.

Leo ni siku ya 53 tangu hayati mwendazake atwaliwe kutoka maisha haya... Wafaidikaji wa utawala wake wakajipa kandarasi ya kulinda 'mazuri' yake huku wakipambana mitandaoni na kila aliyejaribu kukosoa utawala wa hayati mwendazake. Hii si kandarasi ndogo hata kidogo.

Kuweza kuiendesha kwa mafanikio mpaka ufikie lengo kunahitaji oganaizesheni kubwa ya pamoja, rasilimali watu, na vyanzo vya uhakika vya mapato.

Vikundi tarajiwa kwa maana ya rasilimali watu vilivyotegemewa kuifanya hii kandarasi ni LMB7, MATAGA na kikundi kidogo cha SKM GANG! Lakini kwa bahati mbaya kabisa watatu hawa wakakosa ushirikiano na kuanza kuhitilafiana na kutuhumiana wao kwa wao
Ili uweze kuendesha kampeni ya mafanikio .. Ukiachana na mpango kazi wa mradi wako ... Pesa za kuwezesha na watu wa kufanya kazi ni muhimu sana.

Na hizo pesa lazima zipatikane toka chanzo cha uhakika na endelevu

Mwanzoni baada tu ya kifo mradi ulienda vizuri sana, wafanya kampeni za kulinda legacy walilipwa bila kigugumizi na walipaji walitoa bila kusita....lakini kadiri muda ulivyosogea ukweli mchungu na wa kuogofya sana ulianza kujifunua. Kwamba malipo yanayotoka hayana monitoring ya kueleweka

Kwamba kila sent itokayo hakuna replacement yake tena kwakuwa mfadhili mkuu hayupo tena.

Kwamba malipo yanatofautiana kwa watu wanaofanya kazi moja..kuna wanaopata zaidi na kuna wanaopata kiduchu. Kwamba uhitaji wa cash ni mkubwa sana kuliko matarajio na hakuna vyanzo vya mapato.

Chini ya siku 100 tayari wanapumulia mashine. Kilichobaki sasa hakuna umoja wala kandarasi ya kulinda legacy tena.. Kila mtu na lwake! Wanachoangalia sasa ni maslahi binafsi.. Kuliko kushupaa kulinda legacy ya mfu Yenye gharama kubwa ni heri kulinda chochote alichovuna toka utawala wa hayati mwendazake.

Ni wazi kuna baadhi yao ni wafaidikaji wakubwa wa miradi binafsi ya marehemu waliopewa kuisimamia, ambayo kimsingi ni ya familia ya mwendazake! Si ajabu kati yao kuna walio busy kutaka kuitaifisha na kuigeuza ya kwao.. Na hapa ndio wanachimbana na kutofautiana.

Joto la kulinda legacy linapoa kwa kasi ya aina yake na ikigonga siku ya 100 litakuwa tayari baridi kabisa... Tena ile YABISI... Halafu tutaenda kuizika legacy kwenye makaburi ya sahau.
 
Ipo siku mtanikumbuka ndugu zangu---- JPM.


Ukiona unashangiliwa na Chadema nenda ukapime uwezo wako wa kufikiri utakuwa umeshuka sana.
Kabla hata ya miezi miwili haijaisha ni wizi kila kona.


Screenshot_20210508-121100_WhatsApp.jpg
20210508_120538.jpg
 
Mama aliwaneutralize kwa kuwaambia kwa maneno matupu kuwa yeye na hayati ni kitu kimoja. Wakawa disarmed, wakakosa sababu ya kuwa confronrational, wakakosa wa kumlinganisha naye ili kuzilinganisha legacy.

Wakaona wamshambulie Kikwete ili kujaribu kuonyesha kuwa hayati eti alikuwa bora, Lakini hiyo haiwezi kuzaa matunda maana Mzee Jakata yuko kwenye mioyo ya watu, anapendwa kweli.

Wanaona Wakimshambulia mama basi ana nguvu za kuwazingua kwelikweli, kwa hiyo wameamua kujing'tang'ata tu!
 
Mama aliwaneutralize kwa kuwaambia kwa maneno matupu kuwa yeye na hayati ni kitu kimoja. Wakawa disarmed, wakakosa sababu ya kuwa confronrational, wakakosa wa kumlinganisha naye ili kuzulinganisha legacy. Wakajikuta wambulie Kikwete ili kujaribu kuonyesha kuwa hayati alikuwa bora, Lakini hiyo haiwezi kuzaa matubda maana Mzee Jakata yuko kwenye mioyo ya watu, anapendwa kweli.
Wanaona Wakimshambulia mama basi ana nguvu za kuwazingua kwelikweli, kwa hiyo wameamua kujing'tang'ata tu!

Ikigonga siku mia tutakuwa tumewasahau wote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom