ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Date::12/5/2009Kanali mstaafu atangaza kugombea ubunge Tarime kupitia CCM
Na Samson Chacha, Tarime
KANALI Mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mahende Kichonge (65)ametangaza kugombea Ubunge katika Jimbo la Tarime mwakani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Kichonge alitangaza nia hiyo wakati wa mazishi ya kaka yake aliyewahi kuwa Ofisa Utumishi Tawala wa Kwanza katika Wilaya ya Tarime na Mkaguzi wa Mahakama za Mwanzo nchini, Kichonge Mahende aliyefariki Novemba 30, mwaka huu na kuzikwa Desemba 4, mwaka huu kijijini kwake Kemakorere Kata ya Nyarero.
Katika mazishi hayo, alikuwepo kanali Raphael Isarra Chacha na kijana mkubwa wa marehemu Kichonge Luteni Kanali David Kichonge,na mamia ya waombolezaji, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ryoba Kangoye Masero ambaye ni ndugu wa marehemu.
Akitoa kauli hiyo katika umati mkubwa wa waombolezaji waliofika katika mazishi hayo, Kanali Mahende alisema kuwa
"Mimi kama mwana Tarime ninayo haki ya kugombea Ubunge katika Jimbo langu hili la Tarime mwakani kupitia chama changu ambacho sitakihama daima cha CCM na ninazo sababu za kuwania kiti hicho, kwanza kuwaunganisha Jamii ya Kabila la Wakurya na kuwa kitu kimoja na kuondoa dhana potofu za mila zilizopitwa na wakati za kubaguana, kuwashirikisha wazee wa mila wa koo zote za kabila la Wakurya na kukomesha wizi wa mifugo kwa kushirikiana na Sungusungu,†alisema.
Kanali Mahende alisema endapo atachaguliwa atahakikisha barabara zote ambazo hazipitiki kwa urahisi zinafanyiwa matengenezo, kukamilisha madarasa na nyumba za walimu na kwamba ataiomba serikali kuongeza walimu katika shule za Sekondari za kata kutokana na kuwepo kwa tatizo la walimu.
HIVI HAWA MAKANALI HUWA NI MAKADA WA CCM HUKO JESHINI????

Pia alisema ataanzisha vikundi vya vijana na Wazee kwa lego la kuwapatia mikopo ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Christopher Kangoye na Kanali David Gichonge waliwashukuru wananchi na marafiki waliofika katika shughuli za kumzika kaka yao Gichonge Mahende.