Kanali Mjengwa alia na demokrasia

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
80,683
93,423
mwananchi.PNG

Mbarali. Mkuu wa wilaya mstaafu, Kanali Edmund Mjengwa amesikitishwa kuminywa demokrasia nchini.

Kanali Mjengwa amesema hafurahishwi na namna upinzani unavyominywa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

Amesema mfumo wa demokrasia ya vyama vingi nchini uliridhiwa na Serikali ya CCM yenyewe miaka ya 1990, hivyo haiwezekani Serikali hiyohiyo inayoongozwa na CCM ikasema siasa hadi mwaka 2020.

“Mimi ni mwanaCCM haswa, niliyelelewa na kukulia ndani ya CCM tangu tunapata uhuru mwaka 1961, hivyo ninakifahamu vyema kabisa chama changu na hapa najiuliza hivi chama changu ndicho kilichoiamuru Serikali iminye upinzani au ni Serikali yenyewe? Nasema hivi, upinzani hautendewi haki kabisa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu hawawezi kula democrasia.

Mnawashindisha juani watoto wa watu kuwahubiria upuuzi na mabadiliko hewa alafu nyie baada ya hapo mnajilipa posho nono kwa kuhutubia mkutano wa hadhara!!!

Siyo vyama vya upinzani tu hata ccm wenyewe wamezuiwa kufanya hayo.

Hata hivyo mmiliki wa chadema Lowasa amempongeza rais kwa kuruhusu mikutano ya ndani tu.
 
Aisee ilitakiwa akiwa jeshini ausaidie upinzani,lkn sasa naona haina effects
 
CCM ina watu makini CCM ina watu wenye uthubutu wa kuhoji sioni nani mwenye uwezo wa kujibu hoja nzito kama hizi.
 
Watu hawawezi kula democrasia.

Mnawashindisha juani watoto wa watu kuwahubiria upuuzi na mabadiliko hewa alafu nyie baada ya hapo mnajilipa posho nono kwa kuhutubia mkutano wa hadhara!!!

Siyo vyama vya upinzani tu hata ccm wenyewe wamezuiwa kufanya hayo.

Hata hivyo mmiliki wa chadema Lowasa amempongeza rais kwa kuruhusu mikutano ya ndani tu.
unaweza ukaweka Mikataba ya kuuziana chama kati ya Mbowe na Lowassa?

Chama cha mapinduzi kama kitaendelea kuwa na wanachama sampuli yenu basi ni janga kwa taifa hili.
 
Mzee ameona mbali tukiacha ushabiki wa kisiasa.

Kanali yupo sahihi

Kama taratibu za kufanya siasa zinabadilishwa ingekuwa vyema wadau wangeshirikishwa kabla.

tume ya uchaguzi, msajiri wa vyama, polisi na wanasiasa wangejadili utaratibu wa utendaji wa vikao vya ndani, mikutano ya nje, umuhimu wa kalenda ya mwaka, matumizi ya ruzuku nk... hapo demokrasia ingefana.
 
Umewaza vizuri
 
Back
Top Bottom