Kanali Haruni Kondo "Nimetumwa na Rais Magufuli kugombea"

usinijibu hivyo

JF-Expert Member
Nov 7, 2017
248
327
Mzee huyu Miaka 71 anazunguka Wilaya ya Kilombero akiutaka Ubunge, akitoa Rushwa ya Shilingi Elfu tano tano na elfu kumi kumi na wapambe wake wakubwa anawapa laki tatu tatu.

Ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta na juzi ameongezewa Mkataba na pia anajinasibu kuwa Ni mjumbe mzito katika vikao vya juu vya wadhamini wa CCM.

Tunapenda sana kazi nzuri afanyayo Mhe Rais JPM lakini kuliko kumchagua babu huyu anaetoa Rushwa wazi wazi na kusema ametumwa na Rais agombee ili awe Waziri Mara mia tuendelee na Mbunge wetu Lijualikali.

Mnaomsaidia Mhe Rais Mfatilieni huyu mtu anachafua jina la Rais kujinathibisha nalo huku akitoa Rushwa.

Tumemsikia Katibu Mkuu Dkt Bashiru akilaani na kukemea watu wa hivi na kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa hana Mgombea.

Mama yangu amenambia Leo alipita kwenye kata yao akawaita wajumbe nakuwaambia
"..miaka mingi sana hatujapata Waziri kwakuwa hamtaki kunichagua Mimi,safari hii hakuna wakunizuia ata iweje, mmeona Jinsi Mhe Rais ameniteua vyeo vingi,ameniambia nije kumgombea na Mimi Ni Waziri...msifanye Makosa..."

Mama anasema amechukua elfu kumi yake akaweka vocha akanipigia
"...Mwanangu Gwakashina
Neema imeanza Mwanangu,agu Mwaka gwa mavuno agu..amepita huko vijijini anatoa 5000 mjini 10000 ..."
akaendelea kunisimulia kama.nilivyoeleza hapo juu..

Kuwa amezunguka Kata zote.

Kama Kweli viongozi wa CCM wanasema watendayo nasubiri kuona wakikamata watu hawa wandani ya chama chao na kuwatoa mfano

Vinginevyo
PolePole unakazi ngumu sana,nilikusikia siku ile ukiwaambia TAKUKURU wakamate ata wateuliwa wa Rais ama WanaCCM,Nazi bado sana,Rushwa Ni Kansa.
IMG-20200127-WA0001.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi JPM ni nani?
Kwa nini wanatuma vila walaze akili za vilaza wapigakura??
Mzee anazingua
 
Mbona hana nuru? mkimchagua kweli ataweza kasi ya JPM au ndio mtakuwa mmemsogeza karibu na kaburi?
 
Ushindi wa kisiasa hutokana na mbinu, mikakati, na uwezo. Ukipungukiwa kimoja umeisha.

Ni mzee lkn dhahabu
 
Mzee huyu Miaka 71 anazunguka Wilaya ya Kilombero akiutaka Ubunge, akitoa Rushwa ya Shilingi Elfu tano tano na elfu kumi kumi na wapambe wake wakubwa anawapa laki tatu tatu.

Ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta na juzi ameongezewa Mkataba na pia anajinasibu kuwa Ni mjumbe mzito katika vikao vya juu vya wadhamini wa CCM.

Tunapenda sana kazi nzuri afanyayo Mhe Rais JPM lakini kuliko kumchagua babu huyu anaetoa Rushwa wazi wazi na kusema ametumwa na Rais agombee ili awe Waziri Mara mia tuendelee na Mbunge wetu Lijualikali.

Mnaomsaidia Mhe Rais Mfatilieni huyu mtu anachafua jina la Rais kujinathibisha nalo huku akitoa Rushwa.

Tumemsikia Katibu Mkuu Dkt Bashiru akilaani na kukemea watu wa hivi na kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa hana Mgombea.

Mama yangu amenambia Leo alipita kwenye kata yao akawaita wajumbe nakuwaambia
"..miaka mingi sana hatujapata Waziri kwakuwa hamtaki kunichagua Mimi,safari hii hakuna wakunizuia ata iweje, mmeona Jinsi Mhe Rais ameniteua vyeo vingi,ameniambia nije kumgombea na Mimi Ni Waziri...msifanye Makosa..."

Mama anasema amechukua elfu kumi yake akaweka vocha akanipigia
"...Mwanangu Gwakashina
Neema imeanza Mwanangu,agu Mwaka gwa mavuno agu..amepita huko vijijini anatoa 5000 mjini 10000 ..."
akaendelea kunisimulia kama.nilivyoeleza hapo juu..

Kuwa amezunguka Kata zote.

Kama Kweli viongozi wa CCM wanasema watendayo nasubiri kuona wakikamata watu hawa wandani ya chama chao na kuwatoa mfano

Vinginevyo
PolePole unakazi ngumu sana,nilikusikia siku ile ukiwaambia TAKUKURU wakamate ata wateuliwa wa Rais ama WanaCCM,Nazi bado sana,Rushwa Ni Kansa.View attachment 1336507

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Aboubakary Assenga hagombei tena?
 
Back
Top Bottom