Kamusi ya Matusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamusi ya Matusi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by klf, Oct 7, 2010.

 1. k

  klf Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Msomaji mwenzangu: Naomba unitegee sikio. Hapa Ulaya kamusi za matusi na maneno yenye sifa mbaya ziko madukani. Niwie radhi kama maoni yangu hapa yanazua karaha hata iwe kidogo miongoni mwenu lakini sina nia mbaya hata kidogo. Lazima tutambue kwamba lugha mchafu ndio sehemu muhimu sana isiyotengeka ya lugha yoyote duniani. Ni kiambato cha utamaduni wa lugha. Mimi nia yangu ni kutunga kamusi ya kiswahili yenye kujumlisha maneno mabaya/machafu kama matusi, laana, apizo na vingine vingi vya aina hiyo (yaana misemo ya kutukana, kukebehi, kukemea, kuaibisha, kufedhehesha na hali kadhaika) ambayo siku hizi hutumiwa katika jamii ya kisasa. Mara nyingi vijenzi hivi vya kilugha huboresha uelewa wetu kiroho na kiakili na kihisia wa wanadamu wenzetu tena huangaza sehemu zenye kina sana ubongoni mwa mtu.
  Ikiwa mradi huu muhimu unakuvutia tafadhali niandikie kupitia anwani ya pepe yangu klf100@iolfree.ie. Afadhali toa maana ya msemo pia ili tusidanganyike kuhusu kusudi linalofichika humo ndani. Michango yote yanakaribishwa na yatakiriwa … Natanguliza shukrani za dhati
   
 2. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa unaandika matusi ili nini!?
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa kamusi ya maneno ya kisayansi, tungechangia. Kwa kuwa ni matusi, hiyo ni dhidi ya maadili ya kiAfrika.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  gOOOOSH!
  Tunanukuu na kubandika mambo yote ya Ulaya na kutaka kuyaleta Bongo....Kuna manufaa gani hapa?...Kamusi ya matusi?...for what....yamsaidie nani....umuuzie nani...upate faida ya udhalimu?
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Changia JF kwanza........!
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  wewe unaiga mambo ya ulaya? Iga na ushoga basi nikuone kidume.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  HAhahahahahahaha mkuu wewe ni kiboko, unataka mshikaji aanze kushika ukutani lol!
   
 8. Muacici

  Muacici JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama unafanya utafiti kwa ajili ya shule naona hapo ushafeli, nakushauri utafute topic nyingine yakufanyia utafiti. Kwa utamaduni wetu kamwe hatutakuelewa.
   
 9. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe jamaa vipi huono haya wala hujui vibaya
   
 10. Madikizela

  Madikizela JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 4, 2009
  Messages: 320
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mie nakupongeza kwani bila matusi usingezaliwa, ni muhimu ku mind ulikotokea
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Aliye kwambia kuwa watu wanazaliwa kutokana na matusi ni nani?
   
 12. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu watu wanazaliwa kutokana na mapenzi kamwe sio matusi- Labda (sina uhakika mtanirekebisha kama siko sahihi) mimba iwe imetokana na kubakwa
   
 13. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Vipi kamusi yako ya matusi, ulifanikiwa?
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu anataka kutuharibia Lugha yetu ili Wazungu waione ni Lugha yetu ya Kiswahili ni kuwa Lugha ya Matusi? Mbona sisi tuko huku

  Ughaibuni lakini hatuigi mambo ya huku? Ustaarabu wa Kizungu mimi ninauita ni Ustaraabu wa kishetani inakuwaje Baba wa kizungu analala na

  mwanawe wa kike kitanda kimoja? Je Usiku hawawezi kufanya Nanihii?Au Mama wa Kizungu kulala kitanda kimoja na Mwanawe wa kiume?Je huyo

  mama hawezi kufanya Nanihi na mwanawe wa kiume usiku wakiwa kitanda kimoja na mtoto wake wa kiume tena mkubwa? Tafadhali

  musimfundishe Lugha yetu tukufu, huyu asije akaharibu huko ulaya kumesha mharibu natanguliza asanteni.
   
 15. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hivi hayo maneno ya matusi unayotaka kutunga yatatusaiadia nini sisi kutukwamua katika hali ngumu hii tulionayo, tafadhali usiharibu muda wako kutunga kamusi kama hiyo, tusaidie kutukwamua katika ukata huu tulionao.
   
 16. k

  klf Member

  #16
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanatovuti washariki: Ni dhahiri kwamba mradi huu haukuchochea watu wengi kuichangia. Pai hakuna ubishi kwamba wakati wake haujafika. Ingawa nakubali maamuzi yaliofanywa lakini niruhusu kuwaambiena kwamba siku moja wakati ujao kamuzi ndogo ya aina hii itachapishwa ......hakika. Si vizuri kwa watu fulani kujisingizia kwamba maneno hayo hayamo kwenye lugha. Duniani kote hakuna lugha isiyo na misemo na maneno ya aina hiyo. Kuyaangazia ndiko kuyachukulia kama istilahi ya kiufundi kama tuavyofanya kwa fani nyingine k.m mambo ya kitarakirishi au tuseme fani ya kiseremala. Matusi - yawe mabaya sana au yasiyoumiza sana - ndiyo vifaa vya k.m kujieleza kihisia kuhusu mwenendo fulani fulani n.k.Si jambo la aibu hata kidogo kutambua kuwepo kwake.
   
 17. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Ningekuunga mkono kama ungekuwa na mpango wa kuanziasha kamusi ya maneno ambayo yatasaidia watu kupunguza kutumia maneno ya kuudhi katika kiswahili. Hili halitupeleki popote kimaadili ya kiafrika na hata kukuza upanuzi wa matumizi ya kiswahili ulimwenguni.
   
Loading...