MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,296
KAMUSI MPYA YA KISWAHILI YA CCM
Toleo la Kwanza
©LUMUMBA Street Publishing House 2013
Nukuu chache:
mzalendo: mwananchi anayeona watawala wakiiba mali ya umma huku akiwapigia makofi na kuwalamba miguu.
uchochezi: tabia ya kuwaelimisha wananchi kulinda ama kunufaika na rasilimali za nchi yao na kutetea haki zao za msingi -kikatiba na kibinadamu.
wivu (tena wa kike): hali au tabia ya mwananchi kumyoonshea kidole fisadi.
maandamano: mfuatano au msururu haramu wa wananchi ambao wanatembea kuelekea mahali fulani ili kulaani ufisadi na udhalimu wa chama tawala, aghalabu hulazimika kutawanywa na vyombo vya usalama vya dola.
matembezi ya mshikamano: mfuatano au msururu halali wa wananchi ambao wanatembea kuelekea mahali fulani ili kupongeza au kuunga mkono ajenda za mafisadi, aghalabu husindikizwa na vyombo vya usalama vya dola.
Spika: mtu anayeongoza majadiliano katika bunge kwa kuhakikisha hoja mbadala za upinzani hazitiliwi maanani.
bunge: baraza la taifa lenye wajumbe waliochaguliwa na wananchi ili watetee madudu yanayofanywa na serikali.
mhuni: mtu anayejitokeza mbele ya kadamnasi kudai haki zake za kikatiba na kibinadamu.
ukweli: uchochezi
amani: hali ya wananchi kukaa kimya ilhali wakiona mali zao za umma zikiibiwa na mafisadi au wakifanyiwa dhuluma na watawala.
ufisadi: hali ya wanaume vigogo wanaorubuni wake za vigogo wenzao ili kufanya nao ngono.