Kamusi Mpya ya Kiswahili ya CCM

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
KAMUSI MPYA YA KISWAHILI YA CCM
Toleo la Kwanza
©LUMUMBA Street Publishing House 2013

Nukuu chache:

mzalendo: mwananchi anayeona watawala wakiiba mali ya umma huku akiwapigia makofi na kuwalamba miguu.

uchochezi: tabia ya kuwaelimisha wananchi kulinda ama kunufaika na rasilimali za nchi yao na kutetea haki zao za msingi -kikatiba na kibinadamu.

wivu (tena wa kike): hali au tabia ya mwananchi kumyoonshea kidole fisadi.

maandamano: mfuatano au msururu haramu wa wananchi ambao wanatembea kuelekea mahali fulani ili kulaani ufisadi na udhalimu wa chama tawala, aghalabu hulazimika kutawanywa na vyombo vya usalama vya dola.

matembezi ya mshikamano: mfuatano au msururu halali wa wananchi ambao wanatembea kuelekea mahali fulani ili kupongeza au kuunga mkono ajenda za mafisadi, aghalabu husindikizwa na vyombo vya usalama vya dola.

Spika: mtu anayeongoza majadiliano katika bunge kwa kuhakikisha hoja mbadala za upinzani hazitiliwi maanani.

bunge: baraza la taifa lenye wajumbe waliochaguliwa na wananchi ili watetee madudu yanayofanywa na serikali.

mhuni: mtu anayejitokeza mbele ya kadamnasi kudai haki zake za kikatiba na kibinadamu.

ukweli: uchochezi
amani: hali ya wananchi kukaa kimya ilhali wakiona mali zao za umma zikiibiwa na mafisadi au wakifanyiwa dhuluma na watawala.
ufisadi: hali ya wanaume vigogo wanaorubuni wake za vigogo wenzao ili kufanya nao ngono.
 
Maendeleo: Kuwa na hali duni ya kimaisha kwa walio wengi huku wachache wakinufaika

Elimu: Kuwa na wahitimu wa shule za msingi wasiojua kusoma na kuandika
 
ugaidi: (kt), kuusema ukweli, na kuelekeza watu namna ya kudai haki yao.

maendeleo; (n) wachache kulipwa kikubwa ili hali wengine wakiambiwa kasungura ni kadogo
 
wezi;ni vibaka wanaoiba kuku na simu.
rushwa;ni ile inayochukuliwa na watu kuanzia hakimu wa mahakama ya mwanzo kurudi chini.
maisha bora kwa kila mtanzania;wimbo mtamu wa kuwaimbia walala hoi kipindi cha kampeni ili wapate usingizi mwanana wa kulala miaka mi5;
mahakama ya kadhi;ndoano ya kuwanasa waislamu kipindi cha kampeni.
udini; ni kitu kisichokuwepo lakini kitaliangamiza nchi.
ikulu;ni fursa au zali.
 
Usalama wa taifa: chombo cha kuakikisha mafisadi wanalindwa, mfano-kuimalishwa ulinzi wa spika kwa maamuzi ya kulinda bunge ndioooo...

Dola: muhunganiko wa jeshi, mahakama, bunge ktk maamuzi ya ya kuakikisha tanzania inabaki salama kwa wawekezaji kuamisha rasirimali za taifa. mfano twiga, mchanga wa dhahabu, gesi....

Katiba mpya: chombo chenye maamuzi makuu yakulinda utawala wa magamba
 
Tbccm: television ya taifa ya kueneza habari za magamba.
Policcm: jeshi la polisi kwa ajili ya kukisaidia chama magamba na kuwanyanyasa wapinzani hasa cdm.
Dokta: mwana magamba yeyote mwenye elimu ya magumashi. Kama nchimbi,kamara,jk etc
 
Kamusi hii itatupeleka mbali na Utukufu wa MUNGU.Kila Mtanzania anayependa kuiona PEPO, popote alipo afanye jitihada za kuhakikisha Waandika Kausi wa CCM wanatoa tafsiri sahihi ya Maneno hayo au tutafute Wataalamu wengine wa Kiswahili ili tupate tafsiri sahihi.
 
Mchakato: utaratibu wa ucheleweshwaji kwa makusudi jambo muhimu lenye masilah kwa Taifa ili kulinda mtu wa kundi fulani.
 
Tume: kikundi cha watu kilichoundwa kupoteza muda na ukweli wa jambo mpaka lififie na mwisho kulipwa kodi za wananchi bila kutoa ripoti ya jambo lenyewe likiwa lina wagusa watawala.
 
Back
Top Bottom