Kamundu Class 102: Hatuwezi kuendelea bila kuchagua mfumo wa kufuata! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamundu Class 102: Hatuwezi kuendelea bila kuchagua mfumo wa kufuata!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamundu, Aug 22, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Naona hii topic ni muhimu sana kuliko watu wanavyofikiria naomba nitoe some tena!

  Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?


  1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu

  2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la

  3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.

  Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  mwanakijiji upo!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  dawa ni kuliondoa hili dubwana ccm...sisi wote ni wamoja tatizo ni hili dubwana ccm...
   
 4. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Hoja yako ni nzuri. Sisi ni Waswanglish bwana - mix, mixi, mix kwa kwenda mbele. hakuna anayecome close kwetu: iwe lugha, iwe siasa, iwe mavazi, iwe muziki, uchumi ni ujapari, fikiria ni kitu gani sisi ambapo hatuswanglishagi?
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Narudia Katiba ikikosa hili hatutakuwa na Focus nzuri kwenye maendeleo ni lazima tuongeze uwezo wa Watanzania waweze kuonyesha vipaji vyao vya biashara bila serikali kuingilia kila kitu. Hii Topic imeona mbele sana lakini nafikiri ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.
   
 6. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kamundu, kwanza nikushukuru kwa kuona umuhimu wa kuirudia uzi huu, mimi pia ni muhanga wa mifumo (system's). Kuna mambo mengi sana nimekwama kwasababu ya mifumo. Ni ngumu sana kwenda kinyume na mfumo na hata ukifanikiwa utakua sio mtu wa kawaida tena. Miaka ya hivi karibuni nimeona mfumo mkubwa sana duniani ukishindwa kumudu mapigo, nao sio mwingine ni WORLD ECONOMIC CRISIS, wengi wanajaribu kutafuta ni nini chanzo ila ukweli ni mfumo umeshindwa. Nakubaliana na ww kua mfumo huu tulio nao umefika mwisho, na tunahitaji mfumo mpya wenye vipaumbele, kwani ninachokiona saa hizi ni mabehewa yanaongoza kichwa cha gari moshi, hii ni kwenda kinyume na mfumo.
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Mwanahisa nimekupa na hii ni tatizo kubwa sana Tanzania. Wanasiasa wengi sio watu wenye vipaji vya kutengeneza na kurekebisha mifumo hivyo hata hawaelewi kitu gani tunaongea sana. Tanzania haijulikani inafuata mfumo gani hivyo hakuna kipengele kinachosema serikali inatakiwa kufanya nini. Hii inasababisha kila kiongozi akija kuanzisha miradi ambayo haitafutwa kiongozi huyo akiondoka hivyo inaongeza ukubwa wa serikali bila kurekebisha System. System inasaidia kujua jinsi ya kurekebisha kama mambo hayaendi vizuri.
   
 8. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2016
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  somo miaka minne sasa
   
Loading...