~ Kamtumbwi alikokataa Kikwete ~

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929

boatman_phixr.jpg

SIPENDI tena sitaki kusikia eti Rais wetu Jakaya Kikwete, alitakiwa aingie kwenye mtumbwi kuvuka Mto Ruvuma kwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa Msumbiji.

Tena mtumbwi wenyewe uwe wa kusukumwa na upepo. Zaidi ya yote, sitaki kusikia chaguo lake jingine siku hiyo lilikuwa ni ngalawa ya kasia!

Katika ziara yake mkoani Ruvuma, iliyomalizika siku chache zilizopita, Rais Kikwete alitakiwa kwenda kufungua daraja la Mkenda na hatimaye avuke kuelekea Msumbiji kushiriki sherehe za uhuru wa nchi hiyo.

Alipofika hapo darajani kumbe ni asilimia 35 tu ya daraja ilikuwa imekamilika na hakukuwa na dalili yoyote ya daraja hilo kukamilika ndani ya dakika chache za msafara wa rais.

Matokeo yake, Rais Kikwete, akalazimika kuuruka utepe wa ufunguzi na kwenda kung’aza macho bila kufungua daraja hilo au kuvuka ng’ambo kwenda kwa watani zetu Msumbiji.

Baadaye alipohutubia wananchi alielezea jinsi alivyojisikia kuhusu suala la kuvuka mto kwa mtumbwi, alinukuliwa akisema: “Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea, afadhali Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbamba Bay ataogelea.”

Ni kutokana na hisia zake hizo leo nimejikuta nazungumzia hili ambalo limetokana na maneno hayo. Rais Kikwete aliona mara moja kuwa yeye kwa hakika si mtu wa ‘majini’, licha ya kukaa karibu na Bahari ya Hindi, pamoja na ujanja wake wote, lakini si mwogeleaji.

Kilichonikera mwenzenu si rais kushindwa kutumia mtumbwi au kukiri kuwa hawezi kuogelea, bali ni ule uwezekano kuwa hadi leo karibu wiki mbili baadaye, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, anapigiwa saluti! Kinachonikera, mkuu wa Itifaki bado ni yule yule!

Hivi hawa wawili peke yao walikuwa wanafikiria nini hata kutoa wazo kuwa rais atumie mtumbwi wa kusukumwa na upepo wakati tuna dege letu la sh bilioni 50 lililogongwa na gari la watu wa Usalama wa Taifa na hatuna hata kaboti ka umeme ka kumvusha rais?

Hivi wale watendaji waliohusika na maandalizi ya safari hiyo kwa nini wanaendelea kutesa na kulipwa mishahara kwa fedha za walipakodi wa taifa letu?

Hivi kama Rais Kikwete angeamua kujikaza kisabuni na kuingia kwenye mtumbwi halafu mtumbwi ungepinduka (mitumbwi ina kawaida ya kupinduka ikibeba marais na walinzi wao!) na rais wetu maskini wa Mungu hajui kuogelea na yule mpambe wake anayemfuata kila anakokwenda, angefanya nini, kumpigia saluti? Hivi, walikuwa na maboya ya kuogelea kweli?

Ningekuwa mimi “fulani” kabla sijaondoka pale kuna watu wangefungasha mizigo yao kurudi kijijini na kusahauliwa na mfumo wetu. Huu ni uzembe uliotukuka, ambao tuzo yake ni lupango kwa kuhatarisha maisha ya rais! Lakini, hii ni Tanzania, uzembe unazawadiwa na kutowajibika kunatukuzwa!

Lakini kilichotokea Mto Ruvuma ni mfano wa hali halisi ya uongozi wa taifa letu. Tanzania ipo upande mmoja wa maisha na inataka kuvuka kuelekea mafanikio, neema na heri.

Lakini viongozi wetu wanaogopa kuingia kwenye mtumbwi uitwao ‘uongozi.’ Wanaogopa kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kuharibu sifa zao na hata kuhatarisha maisha yao katika sanduku la kura.

Wote kama Kikwete wanabakia upande na kuishia kusema: “Nikaangalia uamuzi wa kuchukua, nikaona eh, mimi mzembe, nitaweza vipi kuwaambia hawa ukweli na kuwatimua kazi? Nitawaacha kina Mwanakijiji wapige kelele kwa maana wapo kijijini!”

Taifa letu linahitaji uongozi wa dhati, kwani sasa uongozi huo hauonekani. Leo hii tunaambiwa kuna mpango wa Canada kuja na mapendekezo ya kulinda makampuni yao kama Barrick Gold, ili yasikumbane na mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya madini yanayoletwa na Kamati ya Jaji Mark Bomani. Waziri mkuu aliulizwa wiki moja iliyopita na hakujua kinachoendelea!

Leo hii watu wanasubiri ripoti ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, wakati hakuna aliyempa maagizo ya kuandika ripoti ya kuiwasilisha kwa rais!

Leo hii tunajivunia ‘vimaendeleo’ vya simu za mkononi na ‘internet’, wakati maisha ya watu wetu katika takwimu mbalimbali hayajanyanyuka sana. Leo watawala wetu wanataka tuimbe sifa za maendeleo wakati walioendelea ni wao na vizazi vyao.

Lakini tukikosoa tunaambiwa tumezidi kukosoa, ukweli wao wanaufahamu. Wanataka waandishi wasomee fani hiyo wakati wao hawajajiamulia kusomea uongozi. Hivi wamesahau kuwa waliotufikisha hapa kama taifa si waandishi na wasiosoma? Waliotufikisha hapa, wamerundikana serikalini, bungeni na kwenye taasisi kibao, ni wale walio na BA, MA, PhD na kila aina ya vyeti vya sifa?

Hivi Tanzania imefikia hapa kwa sababu haina waandishi wasomi au viongozi wasiosoma? Hivi aliyesaini mkataba wa Buzwagi ana shahada gani? Je, yule aliyesimamia wizi wa Benki Kuu na watu walio chini yake wameishia darasa la nne?

Hivi waliotunga sheria ya Usalama wa Taifa na wale waliopitisha muswada wa sheria ya madini kule bungeni hakuna hata mmoja ambaye ni profesa humo?

Kujaribu kuona kuwa tatizo la Tanzania ni la waandishi ni kutafuta kisingizio. Mzigo huu mnaubeba wenyewe viongozi na kama woga wa Rais Kikwete kupanda mtumbwi wa upepo ni mfano, ni kweli kuwa viongozi wetu mna matatizo. Mnaogopa kupanda mitumbwi ya uongozi ambao unaendana na maamuzi magumu.

Mmebakia kusakizia kina ‘Membe’ wenu na kuwaacha wengine wafanye yale ambayo ninyi wenyewe yamewashinda, siyo kwa sababu hamuwezi bali mnaogopa kujaribu, kwa kuwa mnaweza kupinduka!

Tanzania, nchi yetu inahitaji uongozi wa kweli; kuna kila dalili kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa kama wengine, na tunu ya uongozi hana. Nimefuatilia na sijaona dalili yoyote ya kuonyesha maono kwa taifa na kuliamsha kufikia linapotakiwa.

Jukumu la kuliongoza taifa linamuangukia rais kwa namna ya pekee kuliko waziri mkuu, waziri au mbunge yeyote. Baba wa Taifa alisema hivi katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania: “Na katika makosa makubwa ya maadili na utendaji, mwenye jukumu la wazi wazi la kuwadhibiti wahusika ni rais, na mawaziri wake wanapofanya makosa makubwa, badala ya kujiuzulu, wanaanza kufanya hila na kutafuta visingizio vya kutofanya hivyo.”

Aliongezea na kusema: “Ni kazi yake rais mwenyewe, asiyoweza kusaidiwa na mtu mwingine. Mtu anaweza kumsaidia rais kumnong’oneza waziri wake kujiuzulu; lakini hawezi kumsaidia kumfukuza waziri wake. Hiyo ni kazi ya rais peke yake. Asipoifanya, kosa ni lake peke yake.”

Ni wazi kuwa Rais Kikwete hataki kuingia kwenye mtumbwi wa uongozi na maamuzi magumu. Katiba (Ibara 36) inasema wazi kuwa watumishi wa serikali wanafanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya rais na zaidi ya yote bado ana uwezo wa kusimamia nidhamu ya watumishi wa serikali yetu.

Sasa inapotokea kuna watu kama Mama Mbega kule Ruvuma, ambao wanamuandalia rais mtumbwi wa kusukumwa na upepo kwenda Msumbiji, bado wapo madarakani. Wakulaumiwa si Mbega, bali ni rais mwenyewe, kwani ni yeye aliyetoa baraka kwa mama huyo kuendelea kuwapo hapo.

Kuna watu wanasema na kurudia mara nyingi kuwa: “Rais ana nia nzuri ya kwenda ng’ambo lakini ni hawa aliowatuma kukodisha mtumbwi ndio wana matatizo.” Kuna watu wanaamini kabisa kuwa Rais Kikwete anaangushwa na ‘watendaji.’

Watu hawa wanashindwa kuelewa kuwa mwenye jukumu na uwezo wa mwisho wa kuajiri watu hawa ni rais! Wakati umefika tuite kijiko, kijiko; rais wetu pamoja na sura yake nzuri na tabasamu lake la nguvu lililotufanya tumpigie kura, kwa hakika kwenye suala la uongozi si kiongozi.

Yawezekana ana kipaji cha kuvutia watu lakini kwenye kutuongoza kuelekea mafanikio na neema, kwa hakika tukubali kuwa tumeliwa, tusubiri mwaka 2010.

Tumshukuru kwa jitihada zake zote, lakini kwa hakika kwenye mtumbwi hataingia, kwani ‘yeye ni Mkwere’, hajui kuogelea! Tuwaache wengine wakate mawimbi, naye abaki kuangalia kutoka ng’ambo.

Na kwa kadiri ambavyo watuhumiwa wa ubadhirifu uliofanyika kwenye akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), wanaendelea kunata, ndivyo anavyoonekana asiyeingia kwenye mtumbwi wa uongozi; kwa kadiri serikali yake ilivyoshindwa kuitisha uchunguzi huru na kukaribisha taasisi ya kimataifa ya Scotland Yard kuchunguza mazingira ya safari, ajali na kifo cha Mbunge wa Jamhuri ya Muungano na kutegemea polisi ambao wenyewe nao wanatakiwa kuwa mashahidi, ndivyo mtumbwi wa taifa letu utakavyoendelea kuwabeba kina Membe!

Ndiyo, ukweli na usemwe. Mtumbi alioukataa Kikwete kwa hakika unapelekwa na upepo; unasukumwa na nguvu nje yake! Hakuna nguvu ndani yake isipokuwa kelele za wananchi na taasisi za nje ya nchi.

Ni mpaka pale Rais Kikwete atakapoamua kwa makusudi kabisa kukataa mtumbwi na kutaka meli ambayo yeye ni nahodha na yuko tayari kuyakata mawimbi na kuipeleka ‘mv Mafanikio’ kulekelea kwenye neema.

Vinginevyo, kama nilivyowahi kusema huko nyuma, kwa mtindo huu wa kukaa ng’ambo na kukodolea wengine kwenye mitumbwi, kwa hakika asishangae kama atakuwa ni rais wa mhula mmoja katika historia yetu. Kwa nini?

Jibu alilitoa Baba wa Taifa na ninanukuu (kutoka kitabu kile kile): “Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa masilahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi.

‘‘Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na nzi.” Na kama Mwalimu (nikiwa mwanafunzi wake), niseme kuwa: “Ole wake Tanzania, Tusipoisaidia, niwezalo nimefanya, kushauri na kuonya”.

Kama nahodha anaogopa kushika usukani wa mtumbwi wetu, tuangalie nahodha mwingine mwaka 2010 na kama hatumuoni, bora tutafute mtumbwi mwingine na nadhodha mpya, kwani safari bado ipo.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com au
nipigie simu: 1 248 686 2010
 
Last edited by a moderator:
Hakika, ikiwa kutakuwa na pengo la uongozi kuna watu watakuja na watalijaza. TZ sasa inakosa mwelekeo wa kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kile alichokipigania Mwalimu JK Nyerere sasa kimebaki kuwa ni njozi miongoni mwa WaTZ na kwa hakika tunamuhitaji Nyerere mwingine ili kuweza kurekibisha hii hali.

Tunawahitaji watu wanaothubutu, wataokathubutu kuwaambia viongozi wahujumu uchumi na mafisadi wapishe katika uongozi na kuwachukulia hatua za kinidhamu ili wafuasi wao wasithubutu kurudia makosa ya mabwana zao.

Nahodha legelege ni hatari kwa meli yetu, Hakika atagongesha kwenye miamba na itasambaratika
 
Naliaaaa... pole naliaaa pole sana uwiiii

Jamani hivi kweli ni wapi tunaelekea? Viongozi wenye uthubutu wako wapi?
 
Wanashindwa kupanda mtumbwi au hawataki kupanda mtumbwi? Unasahau kuwa walishapanda kwenye ndege ambayp imeshapaa? sasa wapandeje tena kwenye mtumbwi wakati walishapaa na ndege yao!
 
Angalau waliwahi kwenye ndege, sasa hata mtumbwi hawataki wanataka twende kwa miguu kwa kasi, ari, na nguvu mpya!
 
Jamani huyu Kikwete wetu anatakiwa aombewe sana, kwa wale watu wa dini. Mtumbwi umemshinda, na wenzake nao wanatapatpa. Lakini solution ni moja tu wadanganyika 2010 ni lazima tutafute mtumbwi mwingine na nahodha anayeweza kuthubutu. Kama kuna wakati ambapo wadanganyika wanatakiwa kusimama kidete na kusema imetosha ni sasa na si kesho. Tutiane shime kuanzia sasa kwamba 2010 basi imetosha. Khanga, kofia za 2005 zimekwisha chakaa, tusizichukue tena 2010. Hata hivyo chama cha mafisadi sasa hakina ujanja, fedha za EPA hawatazipata tena kwani wadanganyika sasa wameamka kila kona. Hatutakubali tena fdha zetu ziende kwenye kampeni ya kumweka kiongozi mwoga asiyeweza kuendesha kamtumbwi anapoona kanayumba.
 
Mavanza, unajuaje kuwa hizo fedha zetu hazijaanza kuchukuliwa kwa ajili ya kampeni zijazo? kwani zilizotumika 2005 si tulishagundua wakati zimeshatumika! We subiri, tayari zimeshachotwa, tutashangaa tu zitakavyomwagwa
 
boatman_phixr.jpg

SIPENDI tena sitaki kusikia eti Rais wetu Jakaya Kikwete, alitakiwa aingie kwenye mtumbwi kuvuka Mto Ruvuma kwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa Msumbiji.

Tena mtumbwi wenyewe uwe wa kusukumwa na upepo. Zaidi ya yote, sitaki kusikia chaguo lake jingine siku hiyo lilikuwa ni ngalawa ya kasia!

Katika ziara yake mkoani Ruvuma, iliyomalizika siku chache zilizopita, Rais Kikwete alitakiwa kwenda kufungua daraja la Mkenda na hatimaye avuke kuelekea Msumbiji kushiriki sherehe za uhuru wa nchi hiyo.

Alipofika hapo darajani kumbe ni asilimia 35 tu ya daraja ilikuwa imekamilika na hakukuwa na dalili yoyote ya daraja hilo kukamilika ndani ya dakika chache za msafara wa rais.

Matokeo yake, Rais Kikwete, akalazimika kuuruka utepe wa ufunguzi na kwenda kung’aza macho bila kufungua daraja hilo au kuvuka ng’ambo kwenda kwa watani zetu Msumbiji.

Baadaye alipohutubia wananchi alielezea jinsi alivyojisikia kuhusu suala la kuvuka mto kwa mtumbwi, alinukuliwa akisema: “Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea, afadhali Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbamba Bay ataogelea.”

Ni kutokana na hisia zake hizo leo nimejikuta nazungumzia hili ambalo limetokana na maneno hayo. Rais Kikwete aliona mara moja kuwa yeye kwa hakika si mtu wa ‘majini’, licha ya kukaa karibu na Bahari ya Hindi, pamoja na ujanja wake wote, lakini si mwogeleaji.

Kilichonikera mwenzenu si rais kushindwa kutumia mtumbwi au kukiri kuwa hawezi kuogelea, bali ni ule uwezekano kuwa hadi leo karibu wiki mbili baadaye, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, anapigiwa saluti! Kinachonikera, mkuu wa Itifaki bado ni yule yule!

Hivi hawa wawili peke yao walikuwa wanafikiria nini hata kutoa wazo kuwa rais atumie mtumbwi wa kusukumwa na upepo wakati tuna dege letu la sh bilioni 50 lililogongwa na gari la watu wa Usalama wa Taifa na hatuna hata kaboti ka umeme ka kumvusha rais?

Hivi wale watendaji waliohusika na maandalizi ya safari hiyo kwa nini wanaendelea kutesa na kulipwa mishahara kwa fedha za walipakodi wa taifa letu?

Hivi kama Rais Kikwete angeamua kujikaza kisabuni na kuingia kwenye mtumbwi halafu mtumbwi ungepinduka (mitumbwi ina kawaida ya kupinduka ikibeba marais na walinzi wao!) na rais wetu maskini wa Mungu hajui kuogelea na yule mpambe wake anayemfuata kila anakokwenda, angefanya nini, kumpigia saluti? Hivi, walikuwa na maboya ya kuogelea kweli?

Ningekuwa mimi “fulani” kabla sijaondoka pale kuna watu wangefungasha mizigo yao kurudi kijijini na kusahauliwa na mfumo wetu. Huu ni uzembe uliotukuka, ambao tuzo yake ni lupango kwa kuhatarisha maisha ya rais! Lakini, hii ni Tanzania, uzembe unazawadiwa na kutowajibika kunatukuzwa!

Lakini kilichotokea Mto Ruvuma ni mfano wa hali halisi ya uongozi wa taifa letu. Tanzania ipo upande mmoja wa maisha na inataka kuvuka kuelekea mafanikio, neema na heri.

Lakini viongozi wetu wanaogopa kuingia kwenye mtumbwi uitwao ‘uongozi.’ Wanaogopa kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kuharibu sifa zao na hata kuhatarisha maisha yao katika sanduku la kura.

Wote kama Kikwete wanabakia upande na kuishia kusema: “Nikaangalia uamuzi wa kuchukua, nikaona eh, mimi mzembe, nitaweza vipi kuwaambia hawa ukweli na kuwatimua kazi? Nitawaacha kina Mwanakijiji wapige kelele kwa maana wapo kijijini!”

Taifa letu linahitaji uongozi wa dhati, kwani sasa uongozi huo hauonekani. Leo hii tunaambiwa kuna mpango wa Canada kuja na mapendekezo ya kulinda makampuni yao kama Barrick Gold, ili yasikumbane na mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya madini yanayoletwa na Kamati ya Jaji Mark Bomani. Waziri mkuu aliulizwa wiki moja iliyopita na hakujua kinachoendelea!

Leo hii watu wanasubiri ripoti ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, wakati hakuna aliyempa maagizo ya kuandika ripoti ya kuiwasilisha kwa rais!

Leo hii tunajivunia ‘vimaendeleo’ vya simu za mkononi na ‘internet’, wakati maisha ya watu wetu katika takwimu mbalimbali hayajanyanyuka sana. Leo watawala wetu wanataka tuimbe sifa za maendeleo wakati walioendelea ni wao na vizazi vyao.

Lakini tukikosoa tunaambiwa tumezidi kukosoa, ukweli wao wanaufahamu. Wanataka waandishi wasomee fani hiyo wakati wao hawajajiamulia kusomea uongozi. Hivi wamesahau kuwa waliotufikisha hapa kama taifa si waandishi na wasiosoma? Waliotufikisha hapa, wamerundikana serikalini, bungeni na kwenye taasisi kibao, ni wale walio na BA, MA, PhD na kila aina ya vyeti vya sifa?

Hivi Tanzania imefikia hapa kwa sababu haina waandishi wasomi au viongozi wasiosoma? Hivi aliyesaini mkataba wa Buzwagi ana shahada gani? Je, yule aliyesimamia wizi wa Benki Kuu na watu walio chini yake wameishia darasa la nne?

Hivi waliotunga sheria ya Usalama wa Taifa na wale waliopitisha muswada wa sheria ya madini kule bungeni hakuna hata mmoja ambaye ni profesa humo?

Kujaribu kuona kuwa tatizo la Tanzania ni la waandishi ni kutafuta kisingizio. Mzigo huu mnaubeba wenyewe viongozi na kama woga wa Rais Kikwete kupanda mtumbwi wa upepo ni mfano, ni kweli kuwa viongozi wetu mna matatizo. Mnaogopa kupanda mitumbwi ya uongozi ambao unaendana na maamuzi magumu.

Mmebakia kusakizia kina ‘Membe’ wenu na kuwaacha wengine wafanye yale ambayo ninyi wenyewe yamewashinda, siyo kwa sababu hamuwezi bali mnaogopa kujaribu, kwa kuwa mnaweza kupinduka!

Tanzania, nchi yetu inahitaji uongozi wa kweli; kuna kila dalili kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa kama wengine, na tunu ya uongozi hana. Nimefuatilia na sijaona dalili yoyote ya kuonyesha maono kwa taifa na kuliamsha kufikia linapotakiwa.

Jukumu la kuliongoza taifa linamuangukia rais kwa namna ya pekee kuliko waziri mkuu, waziri au mbunge yeyote. Baba wa Taifa alisema hivi katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania: “Na katika makosa makubwa ya maadili na utendaji, mwenye jukumu la wazi wazi la kuwadhibiti wahusika ni rais, na mawaziri wake wanapofanya makosa makubwa, badala ya kujiuzulu, wanaanza kufanya hila na kutafuta visingizio vya kutofanya hivyo.”

Aliongezea na kusema: “Ni kazi yake rais mwenyewe, asiyoweza kusaidiwa na mtu mwingine. Mtu anaweza kumsaidia rais kumnong’oneza waziri wake kujiuzulu; lakini hawezi kumsaidia kumfukuza waziri wake. Hiyo ni kazi ya rais peke yake. Asipoifanya, kosa ni lake peke yake.”

Ni wazi kuwa Rais Kikwete hataki kuingia kwenye mtumbwi wa uongozi na maamuzi magumu. Katiba (Ibara 36) inasema wazi kuwa watumishi wa serikali wanafanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya rais na zaidi ya yote bado ana uwezo wa kusimamia nidhamu ya watumishi wa serikali yetu.

Sasa inapotokea kuna watu kama Mama Mbega kule Ruvuma, ambao wanamuandalia rais mtumbwi wa kusukumwa na upepo kwenda Msumbiji, bado wapo madarakani. Wakulaumiwa si Mbega, bali ni rais mwenyewe, kwani ni yeye aliyetoa baraka kwa mama huyo kuendelea kuwapo hapo.

Kuna watu wanasema na kurudia mara nyingi kuwa: “Rais ana nia nzuri ya kwenda ng’ambo lakini ni hawa aliowatuma kukodisha mtumbwi ndio wana matatizo.” Kuna watu wanaamini kabisa kuwa Rais Kikwete anaangushwa na ‘watendaji.’

Watu hawa wanashindwa kuelewa kuwa mwenye jukumu na uwezo wa mwisho wa kuajiri watu hawa ni rais! Wakati umefika tuite kijiko, kijiko; rais wetu pamoja na sura yake nzuri na tabasamu lake la nguvu lililotufanya tumpigie kura, kwa hakika kwenye suala la uongozi si kiongozi.

Yawezekana ana kipaji cha kuvutia watu lakini kwenye kutuongoza kuelekea mafanikio na neema, kwa hakika tukubali kuwa tumeliwa, tusubiri mwaka 2010.

Tumshukuru kwa jitihada zake zote, lakini kwa hakika kwenye mtumbwi hataingia, kwani ‘yeye ni Mkwere’, hajui kuogelea! Tuwaache wengine wakate mawimbi, naye abaki kuangalia kutoka ng’ambo.

Na kwa kadiri ambavyo watuhumiwa wa ubadhirifu uliofanyika kwenye akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), wanaendelea kunata, ndivyo anavyoonekana asiyeingia kwenye mtumbwi wa uongozi; kwa kadiri serikali yake ilivyoshindwa kuitisha uchunguzi huru na kukaribisha taasisi ya kimataifa ya Scotland Yard kuchunguza mazingira ya safari, ajali na kifo cha Mbunge wa Jamhuri ya Muungano na kutegemea polisi ambao wenyewe nao wanatakiwa kuwa mashahidi, ndivyo mtumbwi wa taifa letu utakavyoendelea kuwabeba kina Membe!

Ndiyo, ukweli na usemwe. Mtumbi alioukataa Kikwete kwa hakika unapelekwa na upepo; unasukumwa na nguvu nje yake! Hakuna nguvu ndani yake isipokuwa kelele za wananchi na taasisi za nje ya nchi.

Ni mpaka pale Rais Kikwete atakapoamua kwa makusudi kabisa kukataa mtumbwi na kutaka meli ambayo yeye ni nahodha na yuko tayari kuyakata mawimbi na kuipeleka ‘mv Mafanikio’ kulekelea kwenye neema.

Vinginevyo, kama nilivyowahi kusema huko nyuma, kwa mtindo huu wa kukaa ng’ambo na kukodolea wengine kwenye mitumbwi, kwa hakika asishangae kama atakuwa ni rais wa mhula mmoja katika historia yetu. Kwa nini?

Jibu alilitoa Baba wa Taifa na ninanukuu (kutoka kitabu kile kile): “Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa masilahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi.

‘‘Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na nzi.” Na kama Mwalimu (nikiwa mwanafunzi wake), niseme kuwa: “Ole wake Tanzania, Tusipoisaidia, niwezalo nimefanya, kushauri na kuonya”.

Kama nahodha anaogopa kushika usukani wa mtumbwi wetu, tuangalie nahodha mwingine mwaka 2010 na kama hatumuoni, bora tutafute mtumbwi mwingine na nadhodha mpya, kwani safari bado ipo.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com au
nipigie simu: 1 248 686 2010

Mzee Mwanakijiji,

I salute your writing mkuu. The "Mtumbwi-Uongozi" Metaphor you have used neatly shows the lack and failure in leadership that has besieged Tanzania. Tuendelee kuweka mambo wazi, na sisi tufanye kila tunaloweza.
 
sasa hapo watayajuaje na kushare machungu ya wananchi wao, wapiga kura wao? Nakumbuka lile daraja la Mbeya alilojaribu kuvika Mh. H. Mwakyembe....... for how long watu wamelitumia? na bado wakati wa uchaguzi watakuja rufiji kuomba kura zetu.... Mr. Politician
 
Mwkjj,
Ndugu yetu tanzania bado kuna kigugumizi cha utawala, jamaa wameng'ang'ania kama ruba ktk uongozi sijui wanawezaje kutoka pale
 
Nakubali kwa uandishi wako mkuu
 
If anything, this entire saga demonstrates a few things and betrays some facts that even a die hard Kikweteite cannot ignore.

1.Kikwete will sacrifice you in a minute for his own interest.Kitendo cha kukataa kupanda mtumbwi kwa sababu za usalama lakini kumtuma Membe aende kupanda kinaonyesha kuwa Kikwete amefikiri kuwa maisha yake ni muhimu kuliko ya Membe. Waziri mkuu wa zamani hayati Edward Moringe Sokoine alifariki kwa ajali ya gari akitoka bungeni Dodoma kuja Dar. Kabla ya kupanda gari aliombwa kutumia ndege lakini akakataa kwa kusema kuwa alikuja na msafara wa watu wake kwa gari na angependa arudi nao vile vile, hakupenda special treatment. This is in sharp contrast with Kikwete.While the other extreme may also be disdainfully naive, it is at least chivalrous and admirably gallant.Kikwete cannot calaim this gallantry.

2.As I pointed out before, this demonstrates that our Ikulu is run like some medieval chieftain, perhaps less than a court of the majestic chiefs of old.I mean what does it take to send an investigative team ahead of time, all the secret service "detail" people, what are they for? Why are they paid? Couldn't they have gone to do an investigation of the place and brief the president ahead of time about the conditions on the ground?

All I can say is, I predicted this shyt, niliwaambia watu in 95 na tena 2005 kwamba Kikwete ataiabisha nchi, sasa tumeona huko Ruvuma, tumeona tena Mexico City.Na Frankly my surprise is not that this is happenning, but why we did not see this much earlier and more often.Ukimsikiliza alivyojitetea ndiyo kabisa, unakuwa unamsikiliza muhuza kahawa wa mtaani (no offense) ambaye siyo tu hatakiwi kuwa presidential, bali hajapitia hata jeshini!
 
MKJJ,

Kiongozi husema ameshindwa na siyo watu wangu wameshindwa. Kazi ya msingi ya kiongozi wa kweli ni kuhakikishwa tumaini la wananchi wake halipotei. Huyo siyo tu ajue matatizo lakini ajue pia namna na njia bora ya kuyatatua. Lazima ahakikishe kunakuwapo tofauti kati yake na marafiki zake kwa sababu asipofanya hivyo hawezi kuwawajibisha na kuchukua maamuzi mazito. Awe kama mwewe na katu asikubali mkusanyiko kwani atafanana nao. Hazina anayotakiwa kuwa nayo kiongozi bora si pesa wala mali bali tumaini na mapenzi ya wananchi wake.

Hakuna kitu kigumu, cha kijasiri, hatari na kinacholeta wasiwasi kama kuchukua maamuzi mazito dhidi ya makomredi. Huwezi kumtaka mtu afanye kitu ambacho wewe una hofu kukifanya unless wewe ni dhaifu, mwoga na usiyestahili kuwa kingozi. Raisi kama kiongozi hutafuta watu wanaoweza kupewa uongozi na siyo watu wa kuongozwa kwa sababu sifa zake zatosha kufanya hiyo kazi. Kama jitihada zake zinakuwa za kutafuta wanachama zaidi ni vyema akakaa pembeni na kuwapisha wengine.

Raisi huwatoa wananchi wake mahali walipo na kuwavusha kwenye neema zaidi kama jemadari wao. Awe tayari kuwajibika hata pale ambapo anatambua hatari ya kufanya hivyo. Akifanya hivyo si ajabu akakuta wananchi wanakubaliana na kusimama pamoja naye. Kiongozi anayefikiria hana maadui kabisa ajue anajidanganya na hata wafuasi alionao ni feki. Kama unataka raha tafuta kazi rahisi lakini kama unataka kwenda ikulu uwe tayari kuyakabili matatizo ya nchi - ikulu si pa mchezo wala mzaha.

Kwa Mkapa tulitoka kapa na kwa Kikwete tumeula chuya. Kiongozi aliye bora huacha madaraka akijua fika kuwa kazi aliyoiacha itaendelea kwa sababu watu aliowaachia kazi wana uwezo wa kuiendeleza. Tumewaona waliomrithi Mkapa na sasa tujiulize, Kikwete atatuachia uozo gani zaidi.

Lets keep up the fight..........
 
boatman_phixr.jpg

SIPENDI tena sitaki kusikia eti Rais wetu Jakaya Kikwete, alitakiwa aingie kwenye mtumbwi kuvuka Mto Ruvuma kwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa Msumbiji.

Tena mtumbwi wenyewe uwe wa kusukumwa na upepo. Zaidi ya yote, sitaki kusikia chaguo lake jingine siku hiyo lilikuwa ni ngalawa ya kasia!

Katika ziara yake mkoani Ruvuma, iliyomalizika siku chache zilizopita, Rais Kikwete alitakiwa kwenda kufungua daraja la Mkenda na hatimaye avuke kuelekea Msumbiji kushiriki sherehe za uhuru wa nchi hiyo.

Alipofika hapo darajani kumbe ni asilimia 35 tu ya daraja ilikuwa imekamilika na hakukuwa na dalili yoyote ya daraja hilo kukamilika ndani ya dakika chache za msafara wa rais.

Matokeo yake, Rais Kikwete, akalazimika kuuruka utepe wa ufunguzi na kwenda kung'aza macho bila kufungua daraja hilo au kuvuka ng'ambo kwenda kwa watani zetu Msumbiji.

Baadaye alipohutubia wananchi alielezea jinsi alivyojisikia kuhusu suala la kuvuka mto kwa mtumbwi, alinukuliwa akisema: "Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea, afadhali Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbamba Bay ataogelea."

Ni kutokana na hisia zake hizo leo nimejikuta nazungumzia hili ambalo limetokana na maneno hayo. Rais Kikwete aliona mara moja kuwa yeye kwa hakika si mtu wa ‘majini', licha ya kukaa karibu na Bahari ya Hindi, pamoja na ujanja wake wote, lakini si mwogeleaji.

Kilichonikera mwenzenu si rais kushindwa kutumia mtumbwi au kukiri kuwa hawezi kuogelea, bali ni ule uwezekano kuwa hadi leo karibu wiki mbili baadaye, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, anapigiwa saluti! Kinachonikera, mkuu wa Itifaki bado ni yule yule!

Hivi hawa wawili peke yao walikuwa wanafikiria nini hata kutoa wazo kuwa rais atumie mtumbwi wa kusukumwa na upepo wakati tuna dege letu la sh bilioni 50 lililogongwa na gari la watu wa Usalama wa Taifa na hatuna hata kaboti ka umeme ka kumvusha rais?

Hivi wale watendaji waliohusika na maandalizi ya safari hiyo kwa nini wanaendelea kutesa na kulipwa mishahara kwa fedha za walipakodi wa taifa letu?

Hivi kama Rais Kikwete angeamua kujikaza kisabuni na kuingia kwenye mtumbwi halafu mtumbwi ungepinduka (mitumbwi ina kawaida ya kupinduka ikibeba marais na walinzi wao!) na rais wetu maskini wa Mungu hajui kuogelea na yule mpambe wake anayemfuata kila anakokwenda, angefanya nini, kumpigia saluti? Hivi, walikuwa na maboya ya kuogelea kweli?

Ningekuwa mimi "fulani" kabla sijaondoka pale kuna watu wangefungasha mizigo yao kurudi kijijini na kusahauliwa na mfumo wetu. Huu ni uzembe uliotukuka, ambao tuzo yake ni lupango kwa kuhatarisha maisha ya rais! Lakini, hii ni Tanzania, uzembe unazawadiwa na kutowajibika kunatukuzwa!

Lakini kilichotokea Mto Ruvuma ni mfano wa hali halisi ya uongozi wa taifa letu. Tanzania ipo upande mmoja wa maisha na inataka kuvuka kuelekea mafanikio, neema na heri.

Lakini viongozi wetu wanaogopa kuingia kwenye mtumbwi uitwao ‘uongozi.' Wanaogopa kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kuharibu sifa zao na hata kuhatarisha maisha yao katika sanduku la kura.

Wote kama Kikwete wanabakia upande na kuishia kusema: "Nikaangalia uamuzi wa kuchukua, nikaona eh, mimi mzembe, nitaweza vipi kuwaambia hawa ukweli na kuwatimua kazi? Nitawaacha kina Mwanakijiji wapige kelele kwa maana wapo kijijini!"

Taifa letu linahitaji uongozi wa dhati, kwani sasa uongozi huo hauonekani. Leo hii tunaambiwa kuna mpango wa Canada kuja na mapendekezo ya kulinda makampuni yao kama Barrick Gold, ili yasikumbane na mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya madini yanayoletwa na Kamati ya Jaji Mark Bomani. Waziri mkuu aliulizwa wiki moja iliyopita na hakujua kinachoendelea!

Leo hii watu wanasubiri ripoti ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, wakati hakuna aliyempa maagizo ya kuandika ripoti ya kuiwasilisha kwa rais!

Leo hii tunajivunia ‘vimaendeleo' vya simu za mkononi na ‘internet', wakati maisha ya watu wetu katika takwimu mbalimbali hayajanyanyuka sana. Leo watawala wetu wanataka tuimbe sifa za maendeleo wakati walioendelea ni wao na vizazi vyao.

Lakini tukikosoa tunaambiwa tumezidi kukosoa, ukweli wao wanaufahamu. Wanataka waandishi wasomee fani hiyo wakati wao hawajajiamulia kusomea uongozi. Hivi wamesahau kuwa waliotufikisha hapa kama taifa si waandishi na wasiosoma? Waliotufikisha hapa, wamerundikana serikalini, bungeni na kwenye taasisi kibao, ni wale walio na BA, MA, PhD na kila aina ya vyeti vya sifa?

Hivi Tanzania imefikia hapa kwa sababu haina waandishi wasomi au viongozi wasiosoma? Hivi aliyesaini mkataba wa Buzwagi ana shahada gani? Je, yule aliyesimamia wizi wa Benki Kuu na watu walio chini yake wameishia darasa la nne?

Hivi waliotunga sheria ya Usalama wa Taifa na wale waliopitisha muswada wa sheria ya madini kule bungeni hakuna hata mmoja ambaye ni profesa humo?

Kujaribu kuona kuwa tatizo la Tanzania ni la waandishi ni kutafuta kisingizio. Mzigo huu mnaubeba wenyewe viongozi na kama woga wa Rais Kikwete kupanda mtumbwi wa upepo ni mfano, ni kweli kuwa viongozi wetu mna matatizo. Mnaogopa kupanda mitumbwi ya uongozi ambao unaendana na maamuzi magumu.

Mmebakia kusakizia kina ‘Membe' wenu na kuwaacha wengine wafanye yale ambayo ninyi wenyewe yamewashinda, siyo kwa sababu hamuwezi bali mnaogopa kujaribu, kwa kuwa mnaweza kupinduka!

Tanzania, nchi yetu inahitaji uongozi wa kweli; kuna kila dalili kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa kama wengine, na tunu ya uongozi hana. Nimefuatilia na sijaona dalili yoyote ya kuonyesha maono kwa taifa na kuliamsha kufikia linapotakiwa.

Jukumu la kuliongoza taifa linamuangukia rais kwa namna ya pekee kuliko waziri mkuu, waziri au mbunge yeyote. Baba wa Taifa alisema hivi katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania: "Na katika makosa makubwa ya maadili na utendaji, mwenye jukumu la wazi wazi la kuwadhibiti wahusika ni rais, na mawaziri wake wanapofanya makosa makubwa, badala ya kujiuzulu, wanaanza kufanya hila na kutafuta visingizio vya kutofanya hivyo."

Aliongezea na kusema: "Ni kazi yake rais mwenyewe, asiyoweza kusaidiwa na mtu mwingine. Mtu anaweza kumsaidia rais kumnong'oneza waziri wake kujiuzulu; lakini hawezi kumsaidia kumfukuza waziri wake. Hiyo ni kazi ya rais peke yake. Asipoifanya, kosa ni lake peke yake."

Ni wazi kuwa Rais Kikwete hataki kuingia kwenye mtumbwi wa uongozi na maamuzi magumu. Katiba (Ibara 36) inasema wazi kuwa watumishi wa serikali wanafanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya rais na zaidi ya yote bado ana uwezo wa kusimamia nidhamu ya watumishi wa serikali yetu.

Sasa inapotokea kuna watu kama Mama Mbega kule Ruvuma, ambao wanamuandalia rais mtumbwi wa kusukumwa na upepo kwenda Msumbiji, bado wapo madarakani. Wakulaumiwa si Mbega, bali ni rais mwenyewe, kwani ni yeye aliyetoa baraka kwa mama huyo kuendelea kuwapo hapo.

Kuna watu wanasema na kurudia mara nyingi kuwa: "Rais ana nia nzuri ya kwenda ng'ambo lakini ni hawa aliowatuma kukodisha mtumbwi ndio wana matatizo." Kuna watu wanaamini kabisa kuwa Rais Kikwete anaangushwa na ‘watendaji.'

Watu hawa wanashindwa kuelewa kuwa mwenye jukumu na uwezo wa mwisho wa kuajiri watu hawa ni rais! Wakati umefika tuite kijiko, kijiko; rais wetu pamoja na sura yake nzuri na tabasamu lake la nguvu lililotufanya tumpigie kura, kwa hakika kwenye suala la uongozi si kiongozi.

Yawezekana ana kipaji cha kuvutia watu lakini kwenye kutuongoza kuelekea mafanikio na neema, kwa hakika tukubali kuwa tumeliwa, tusubiri mwaka 2010.

Tumshukuru kwa jitihada zake zote, lakini kwa hakika kwenye mtumbwi hataingia, kwani ‘yeye ni Mkwere', hajui kuogelea! Tuwaache wengine wakate mawimbi, naye abaki kuangalia kutoka ng'ambo.

Na kwa kadiri ambavyo watuhumiwa wa ubadhirifu uliofanyika kwenye akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), wanaendelea kunata, ndivyo anavyoonekana asiyeingia kwenye mtumbwi wa uongozi; kwa kadiri serikali yake ilivyoshindwa kuitisha uchunguzi huru na kukaribisha taasisi ya kimataifa ya Scotland Yard kuchunguza mazingira ya safari, ajali na kifo cha Mbunge wa Jamhuri ya Muungano na kutegemea polisi ambao wenyewe nao wanatakiwa kuwa mashahidi, ndivyo mtumbwi wa taifa letu utakavyoendelea kuwabeba kina Membe!

Ndiyo, ukweli na usemwe. Mtumbi alioukataa Kikwete kwa hakika unapelekwa na upepo; unasukumwa na nguvu nje yake! Hakuna nguvu ndani yake isipokuwa kelele za wananchi na taasisi za nje ya nchi.

Ni mpaka pale Rais Kikwete atakapoamua kwa makusudi kabisa kukataa mtumbwi na kutaka meli ambayo yeye ni nahodha na yuko tayari kuyakata mawimbi na kuipeleka ‘mv Mafanikio' kulekelea kwenye neema.

Vinginevyo, kama nilivyowahi kusema huko nyuma, kwa mtindo huu wa kukaa ng'ambo na kukodolea wengine kwenye mitumbwi, kwa hakika asishangae kama atakuwa ni rais wa mhula mmoja katika historia yetu. Kwa nini?

Jibu alilitoa Baba wa Taifa na ninanukuu (kutoka kitabu kile kile): "Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa masilahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi.

'‘Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na nzi." Na kama Mwalimu (nikiwa mwanafunzi wake), niseme kuwa: "Ole wake Tanzania, Tusipoisaidia, niwezalo nimefanya, kushauri na kuonya".

Kama nahodha anaogopa kushika usukani wa mtumbwi wetu, tuangalie nahodha mwingine mwaka 2010 na kama hatumuoni, bora tutafute mtumbwi mwingine na nadhodha mpya, kwani safari bado ipo.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com au
nipigie simu: 1 248 686 2010

Mzee Mwanakijiji

Bravo BRAVO ..... .... huku ndiko kumkoma nyani giladi haswa hadi golan. Unafahamu hawa punguani wanafikiri kuna mchezo wa upatu ambao unachezwa lakini wewe subiri moto wake utakapowaka hakuna atakayeweza kuuzima. Huyu ni one term president tena aache kwa ridhaa yake mwenyewe asigombee maana patakuwa hapatoshi.
 
boatman_phixr.jpg

... "Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea, afadhali Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbamba Bay ataogelea."

Hivi hawa wawili peke yao walikuwa wanafikiria nini hata kutoa wazo kuwa rais atumie mtumbwi wa kusukumwa na upepo wakati tuna dege letu la sh bilioni 50 lililogongwa na gari la watu wa Usalama wa Taifa na hatuna hata kaboti ka umeme ka kumvusha rais?

...Huu ni uzembe uliotukuka, ambao tuzo yake ni lupango kwa kuhatarisha maisha ya rais! Lakini, hii ni Tanzania, uzembe unazawadiwa na kutowajibika kunatukuzwa!

Sasa inapotokea kuna watu kama Mama Mbega kule Ruvuma, ambao wanamuandalia rais mtumbwi wa kusukumwa na upepo kwenda Msumbiji,bado wapo madarakani.

Tunajuaje kama Kikwete aliandaliwa mtumbwi na Mkuu wa Itifaki na Mkoa wa Ruvuma au yeye ndio alitoa tu ki joke kwamba ali consider mtumbwi kivyake ?

Siku ile na chache za mbeleni sikuona ripoti yeyote ya press kuiliza Ikulu au serikali ya Ruvuma, je, Rais aliandaliwa mtumbwi, au ni yeye ali consider mtumbwi ?

Na kama hili liliulizwa, mimi sikuona lilipoandikwa. Tunarudi pale pale, kwamba tunaweza kuwa tunajadili maswala ya Kitaifa wakati, kwa kweli, hakuna anaejua kinachoendelea. The media hapa ndio the weakest link. Kwa kuwa hatujui kinachoendelea, hatuwezi kujua kinachotakiwa kieendelee. Kwa hiyo hatuwezi kuendelea.
 
Makosa yote ni ya Kikwete mwenyewe kwa vile ndiye aliyewaweka jamaa hao pale na ndiye anayeendela kuwaweka hapo. Siku nyingine atakuta hakuna hata hako kamtumbwi, watamwambia mzee vua nguo uoegelee.
 
Kile alichokipigania Mwalimu JK Nyerere sasa kimebaki kuwa ni njozi miongoni mwa WaTZ na kwa hakika tunamuhitaji Nyerere mwingine ili kuweza kurekibisha hii hali.

No, tunachohitaji sio another Nyerere, tunachohitaji ni dictatorship. And I mean it. Seriously. You know, couple of years ago, niliwahi kuona watu wanasukuma ndege ya jeshi (huko mkoa) ati iwake ili waendelee na safari. Think of it people: wanasukuma ndege ya jeshi ili iwake?

Seriously, tunahitaji dictator mmoja atucharaze bakora kwanza kisha ndo tupate akili.

I rest my case.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom