Kampuni zataka kuinunua Zain | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni zataka kuinunua Zain

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Aug 17, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kampuni kadhaa zinataka kuinunua kampuni ya simu za mkononi, Zain Afrika.

  Bodi ya Wakurugenzi ya Zain inajadiliana kuhusu suala hilo na watayatathimini maombi yatakayowasilishwa.

  “Taarifa zaidi itatolewa baadaye,” imesema taarifa iliyotolewa leo na kampuni hiyo.

  Zain imetangaza hesabu ya nusu mwaka zikionesha kuwa wateja wameongezeka na mapato pia yameongezeka kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na mwaka uliopita.

  Kampuni hiyo inatathimini upya mtaji wake wa Afrika kwa lengo la kuongeza thamani kwa ajili ya wadau.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi Juni 30 mwaka huu, mapato yameongezeka kufikia dola za Marekani milioni 4.014 sawa na asilimia 24.1 ya mapato ya mwaka jana.

  Mapato ya kampuni pia kabla ya kutoa faida na kodi pia yameongezeka kwa asilimia 46.3 na kufikia dola za Marekani bilioni 1.77.

  Baada ya kodi, mapato yamefika dola za Marekani milioni 533.5 ikiwa ni nyongeza ya asilimia 4.4 ikilinganisha na hesabu za kipindi kama hicho mwaka jana.

  Faida kwa kila hisa kwa ajili ya kipindi cha miezi sita pia ilifika dola za Marekani 0.14.

  Taarifa hiyo imebainisha kuwa, hadi juni 30, 2009 idadi ya wateja wa Mashariki ya Kati na Afrika yenye mtandao wa Zain pia imeongezeka kwa asilimia 37 na kufikia wateja hadi milioni 69.5.

  "Licha ya mazingira yenye changamoto inayotokana na misukosuko ya kiuchumi duniani, mabadiliko katika thamani za fedha za kigeni na ushindani katika soko, pamoja na uwekezaji katika kupanua mtandao wetu, Zain bado iliweza kupata matokeo mazuri na kupata faida nzuri katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2009.” amesema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain, Dk Saad Al Barrak.

  Dk. Al Barrak amesema, huo ni ushuhuda wa uongozi madhubuti na ufanisi wa biashara za kampuni hiyo Mashariki ya Kati na Afrika.

  Katika miaka ya karibuni, Zain imewekeza katika kupanua mtandao wake na huduma inazotoa kama huduma ya One Network katika mabara yote na kuwezesha ongezeko la wateja wapya na mapato.

  "Tunatarajia kuvuna mengi zaidi kutokana na uwekezaji katika mtandao, na sio tu katika kipindi cha nusu mwaka wa 2009, lakini hata katika miaka inayokuja na huduma yetu ya One Network ikichochea kukua kwetu,’’ amesema Dk Al Barrak.

  Hivi karibuni kampuni imezindua programu ya ‘Drive11’, inayofanya Zain iweke mkazo katika huduma zinazoikutanisha kampuni na wateja wake ana kwa ana pamoja na mambo ya kibiashara.

  Programu hiyo inatarajia kuongeza tija na kuiwezesha Zain kufanya kazi kwa gharama ndogo za kiutawala.
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3144&cat=kitaifa
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Nothing is surprising; acquisitions and mergers are part and parcel of capitalist survival strategies.
  TTCL karagabaho!
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hapo wanacheza na sera ya uwekezaji ya Tanzania inayowapa miaka 3 kuangalia biashara bila kulipa kodi. Hii ipo tanzania tu!!. Hivi Tanzania tumerogwa?? Watu wana pata faida wanaondoka, kibaya zaidi wanaacha wameua kampuni zetu (TTCL) halafu wapumbavu TIC wapo tu!!!

  Bora hata ya Vodacom, ingawa nazo ni hela zetu (RA), Zain/Celtel hawakujenga hata mnara mmoja wa gharama, wanatumia ya TTCL halafu wanatuambia wamepata faida mara dufu!! CCM PUMbafu tu!!!
   
  Last edited: Aug 17, 2009
 4. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160

  Hujui kuwa tanzania ni shamba la BIBI,Chukua Chako Mapema(CCM)
   
Loading...