Kampuni za simu zinawaibia wananchi. TCRA wanajua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni za simu zinawaibia wananchi. TCRA wanajua hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mutambukamalogo, Jun 20, 2011.

 1. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mi ni mteja wa Airtel, nakumbuka kuna member alichangia humu jamvini kwamba kampuni za simu zinawaibia wateja. Aidha kwa kufahamu au kutofahamu. Nimefuatilia mara kadhaa, leo nime prove alicholalamika yule Bwana. Airtel wana promotion ya kutuma sms 5 ambazo utakatwa pesa kisha unapewa sms 100 za bure kutuma ndani ya masaa 12.

  Leo nime chagua watu wangu 18 kisha nikawatumia sms, cha ajabu mtandao ulikuwa unanitaarifu kila sms inayotumwa. Ilianza umeshatuma sms 10 za bure, Salio sms 90. Kisha umeshatuma sms 20... Salio sms 80.., Mwisho ikaniambia umeshatuma sms 30 za bure.

  Salio la sms za bure ni 70. Jamani! Nilituma sms 18 tu hizi 30 zilitokea wapi?. Kingine,ni kwamba kama ukim beep mtu, hata kama hajapokea, angalia salio utakuta limepungua.

  Nilimpigia mtu leo, Simu ili beep kwa sekunde 3 haikupokelewa. Nilitumiwa ujumbe kwamba umetumia sh 11.05. Zimetumika wapi hizi? Wanajamvi tufatilie. Kampuni za simu zinatuibia.
   
Loading...