Kampuni za simu zaweza kusaidia kumjua mgoni wako?

Ampigie huyo tax driver aje amchukue nyumbani kwenda mahali wakati mkewe akiwepo nyumbani na asimpe nafasi ya kuwasiliana naye. Ikiwezekana atumie namba ambayo mkewe hajui. Atapata majibu yenye kuelekea ukweli.

mkuu, mshikaji anatonya kuwa kishafanya hivyo, ndio maana aligundua kuwa yule jamaa wala si tax diver wala nini bali hawara tu kwani alisema kila alipompigia alizuga kuwa yuko mbali na ajaribu axi nyingine!!!

ni kwamba kwa vile hawana mipaka ya simu na wife ndio wife akamseve kma taxi driver ili mzee akikutana na no hiyo asishtukie dili.
 
Ashamaliza mzizi wa Fitina hapo; amconfornt mkewew na alazimishwe simu ipigwe mbele yake; na pengine hata yeye ampigie huyo jamaa kumtafadhalisha aachane na mkewe!:D
Ashaupata ukweli sasa anataka kufumania? Anaweza kuhimili matokeo ya fumanizi?

ninavyomfahamu jamaa yangu kwa hasia, akifumania ataua mtu siku hiyo!!!
 
ninavyomfahamu jamaa yangu kwa hasia, akifumania ataua mtu siku hiyo!!!

Ok nimekuapata; alonge na mkewe na kumwambia wazi kuwa he knows what going on na kama mke akibisha athibitishe vinginevyo hapo hapo! Na amuase mkewe aache utoto; la basi atamke wazi kuwa hapo ndoa haipo na mwambie kuwa aonyeshe dhamira ya kweli kuwa asipojulishwa kinachoendelea basi amchukulie hatua; aidha kuhakikisha huo ufirauni haundelei ama kummwaga; basi!

Hakuna kitu kizuri na kibaya kama instincts; na hujatuamabia hapa mkewe alitoa maelezo agami kuhusu wasiwasi wa mwenzie akiwa a ushahidi wote huo?

hayo mambo yapo; Grace wa saloon; fundi wa kushona nk
 
hajamwambia mkewe hadi sasa............... ndio maana anataka kufumania pachimbike!!!!!!!!!!11
 
Mmmh ndoa hizi siku hizi mara number za simu ohh hanitoshelezi unyumba mwingine anaombwa Tigo, ahh wacha wengine tusubirie kwanza.
 
Very Simple.

1. Mwite Mkanye juu ya mawasiliano na mtu huyo na mweleze unavyohisi. Akikubali msamehe na mkanye asirudie, kisha endeleeni na maisha.

2. Akikataa mwambie wife ampigie simu huyo Tax-Driver na kisha yeye aongee naye na muonye huyo bwana kuwa hutaki awasiliane na wife wako. Mwonye mkeo pia.

3. Ukiona bado wanaendelea, Kodi jamaa wa pikipiki wa kufuatilia mwenendo wa mkeo for 1 week huku ukijenga mazingira ya yeye kuwa huru zaidi na kufanya atakalo huku ukiwa huna noma kabisa. Mpatie details zote mtu wa piki piki with Cameras za picha za mnato na video etc etc. Ukipata ushahidi . . . . basi utaamua utakalo.
 
Manabii wa kale walisema, unaweza kutaka kuifunika dunia nzima kwa zulia ili mguu wako usikanyage ardhi, lakini njia rahisi zaidi ni kuvaa kiatu kitakachofunika mguu wako.

Utaenda makampuni yote ya simu, watu watatumiana barua, au hata salamu kwenye redio na magazeti, utafanya nini?

Kama ni mke wako anaye misbehave mtight mke wako. By the way privacy principles zina apply mpaka kwa mke wako, kama anaweza kukukatalia unyumba kisheria unategemea kampuni ya simu iwe na haki ya kukupa rekodi za mtu baki ambaye unadai ana uhusiano na mkeo?

Ukipata jina na kwenda kumpiga risasi halafu ikajulikana kampuni ya simu imetoa jina? Unafikiri kampuni ya simu haitapata matatizo? Vipi kuhusu wateja wake wakisikia hivyo watajiona wako secure kiasi gani? Vipi ndugu za huyu bwana wakiamua kui sue kampuni ya simu?

Nenda mahakamani katafute subpoena, au ajiri private detective wa kukusaidia kum nail mkeo, lakini hili la kwenda kampuni ya simu bila subpoena ni lame.
 
Advice - It takes 2 to Tango, kupewa jina ya jamaa mpaka Court Injunction, na utafanya kwa wangapi kama mwanamke ana tabia hiyo? baada ya taxi 3, itakuwa lone ranger, smooth operator n.k Talk to your wifey hamna short cut. (labda maskini ya Mungu kamwambia hata jamaa I am single and available?)

Hivi kuna wanawake sasa hivi very agressive wao ndo wanafanya the chase...
 
Hiyo ni issue personal!ila ukienda mahakamani ufungue kesi...itaitishwa....ila uwe na ushahidi...la sivyo litatupwa huko kuwa ni wivu wa mapenzi
 
Kama upo maeneo ya huku kwetu, milimani Mwanza hiyo kampuni ya simu piga ua hawawezi kukupa hizo info vinginevyo watamtajirisha huyo Taxi 3. atawa-sue mpaka wakome ubishi, wewe tumia ujanja wako wa porini kumjua huyo mtu na ukimpata wewe mvunjie yai tu makalioni halafu unamwacha!.
 
Hajajibu swali langu!

KIFUA ANACHO YAKHE?!

Maana asije dondoka kwa mshtuko!

We kama vipi akubali matokeo tu! Ya nini kujifia kwa presha?

Du! Nawe umeshanoti kitu? Kufumania sio lazima uwakute wakipandana! Hii kazi ngumu jamani, unahangaika kutafuta ukweli utakaokumaliza kwa presha! Hivyo, anapaswa ajiandae na matokeo ya aina yoyote. Kama anaona hataweza kuhimili ukweli, basi akubali tu.
 
mkuu, mshikaji anatonya kuwa kishafanya hivyo, ndio maana aligundua kuwa yule jamaa wala si tax diver wala nini bali hawara tu kwani alisema kila alipompigia alizuga kuwa yuko mbali na ajaribu axi nyingine!!!

ni kwamba kwa vile hawana mipaka ya simu na wife ndio wife akamseve kma taxi driver ili mzee akikutana na no hiyo asishtukie dili.

Achukue hizo namba, kisha amshauri mkewe kubadili stail ya kusave majina kwenye simu kwa kuandika majina full badala ya abreviations, ataona jina litakalojitokeza badala ya "tax driver", na afuatilie taratibu kama hilo jina ni la kweli.Kama jina halitaonekana au jina hilo sio la kweli, basi kufumania si lazima uwakute wakicheza game, na hivyo kazi kwake...
 
sijapendezwa na jinsi mnavyolichukulkia hili suala. kama vile rahisi sana. nyie wote mnaosema aache upuuzi mna matatizo, tena si madogo. i can tell from what you have written. hamna uwezo wa kujibainisha (empathy) kujua huyu jamaa anahisi nini. mkeo kuliwa au mumeo kuiba nje kwenu. muelekezeni ni vipi anaweza kutatua tatizo lake na si kukejeli. hao wa makampuni ya simu mbona huwa wanatoa hhizp taarifa? be wise
 
mkuu,

dark city akikusoma hapo kwenye bold, ataingilia kati sasa hivi!!!!!!!!!!!

AK wewe mchokozi sana. Unataka kuniingiza kwenye suala lenye utata kama hili. Hata hivyo umeshindwa kuona kuwa Babaa alishadokeza mapema kwamba huenda wote wawili wanacheza rafu. Kwa hiyo ajiangalie kwanza. Hata hivyo jaribu kumpa ushauri tu kuwa hakuna formula ya ku-handle issue ngumu kama hizi. To handle an emergency is an emergency as well.
 
sijapendezwa na jinsi mnavyolichukulkia hili suala. kama vile rahisi sana. nyie wote mnaosema aache upuuzi mna matatizo, tena si madogo. i can tell from what you have written. hamna uwezo wa kujibainisha (empathy) kujua huyu jamaa anahisi nini. mkeo kuliwa au mumeo kuiba nje kwenu. muelekezeni ni vipi anaweza kutatua tatizo lake na si kukejeli. hao wa makampuni ya simu mbona huwa wanatoa hhizp taarifa? be wise

Usijali mkuu, kila mtu ana yake kichwani. Kwa hiyo jaribu kumchukulia kila mtu kivyake vyake. Huyu jamaa hajakosea kwenda kwenye kampuni za simu kwa sababu hivyo ndivyo akili zake zilivyomwelekeza. Kwa upande wa kampuni za simu, hawawezi kumsaidia kwa sababu ni kinyume cha sheria.

Jamaa inabid aelewe kuwa hata kama angeongea na watu 100 ili wamshauri, si ajabu kila mtu angekuja na lake. Hakuna mtu mwenye uzoefu wa kushughulikia matatizo ya ugoni kwa sababu si suala ambalo linawatokea watu wengi na hata kujirudia rudia kwa mtu yule yule ili apate uzoefu. Kwa maana hiyo wengi wanaongea kwa mtazamo wa jinsi ambavyo wangeshughulikia suala hilo. Ni mtazamo wao na hawana kosa lolote.

Mimi ningeanzia jipu lilipo. Ningeshughulika na my wife wangu mpaka kieleweke. Ataruka, lakini tutakubaliana dili kwamba endapo nitawakamata ama zangu au zao. Baada ya hapo ndio ningeanza kufuatilia. Sidhani kama ningehangaika kufumania kwa sababu ni suala la hatari na matakeo yake huwezi kuyatabiri. Mie nikishagundua kuwa mke wangu ana-cheat basi ndoa imelala kwenye 50-50. No simple answer.
 
:D na haya makampuni ya simu yakianza kutoa siri za wateja basi itabidi watu warudi kwenye zama za kati za mawe sijui walikuwa wanawasiliana kwa njia gani?
 
:D na haya makampuni ya simu yakianza kutoa siri za wateja basi itabidi watu warudi kwenye zama za kati za mawe sijui walikuwa wanawasiliana kwa njia gani?

Hawatakiwi kutoa ila zinatoka tu kama unaijua vizuri bongo! Jamaa yangu alishapewa within minutes!
 
Back
Top Bottom