#COVID19 Kampuni za Silaha Duniani zazidi kutengeneza faida licha ya Coronavirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
1638864437322.png

Ripoti mpya ya taasisi ya kimataifa inayohusika na amani SIPRI inasema watengenezaji wakubwa wa silaha duniani kwa kiasi kikubwa waliepuka anguko la kiuchumi lililosababishwa na janga la Covid-19.

Ripoti ya SIPRI iliyotolewa leo Jumatatu inasema serikali ulimwenguni zimeendelea kununua silaha wakati wa janga la Covid-19, huku baadhi yake zikipitisha hatua za kuyasaidia makampuni ya silaha.

Kwa ujumla makampuni 100 ya juu yameshuhudia ongezeko la faida kwa asilimia 1.3 licha ya uchumi wa dunia kushuka kwa zaidi ya asilimia tatu.

Taasisi ya SIPRI yenye makao yake makuu nchini Sweden, imeongeza kuwa kampuni hizo zimenufaika kutokana na kuingiza fedha taslimu katika uchumi, pamoja na hatua mahususi zilizoundwa kuzisaidia kampuni kama vile malipo ya haraka au mchakato wa kuagiza.

Marekani iliendelea kuongoza katika utengenezaji na mauzo ya silaha duniani, huku watengenezaji wa silaha wa Marekani wakichukua makampuni ya silaha 41 miongoni mwa 100 ya juu duniani. Kati yao, mauzo ya silaha zao ilifikia dola bilioni 285 mnamo 2020 sawa na asilimia 1.9 ya ongezeko ya mwaka hadi mwaka.
 
Hivi chanjo ya COVID -19 inayopigiwa chapuo na Mama Samiah &co ni ya version Gani ya virus?

Manake Kuna virus version 1 waliotokea Wuhan China,baadae ikaja version ya pili, baadae ya 3 sijui ndio Delta.Sasa hivi Kuna version ya 4, Omicron.

Sasa hizi chanjo za bongo zinapambana na virus Gani?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom