Kampuni za mafuta KUGOMA sasa na hawa sijui wamehongwa wagome?

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,337
Baadhi ya kampuni za mafuta zimetishia kugoma iwapo hatua hazitachukuliwa kurekebisha mpango wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja ambao umebainika kukumbwa na dosari ya kuwa na mafuta yaliyochakachuliwa.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kampuni hizo kuona hakuna hatua zilizochukuliwa ili kurekebisha dosari ya kuingizwa nchini mafuta yaliyochakachuliwa na ambayo yalisababisha kuyumba kwa biashara hiyo.

Mapema mwezi huu, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), ilikiri kuwa shehena ya mafuta yaliyoingizwa nchini mwanzoni mwa mwaka huu ilikuwa imechakachuliwa.

Juni 5, mwaka huu Ewura ilimwandikia Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kutaribu Uagizaji Mafuta, PIC (T) Ltd, kueleza kuwa mafuta yaliyoingizwa nchini katika kipindi cha Januari na Machi, mwaka huu yalikuwa yamechakachukuliwa kutokana na kuwa na ethanol kwa wingi.

Barua hiyo ambayo NIPASHE inayo nakala yake inaonyesha kwamba baada ya mafuta hayo kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ilibainika kwamba katika sampuli 11 zilizopelekwa, 10 zilikutwa mafuta yana ethanol nyingi kwa kiwango ambacho hakikubaliki hata katika vigezo vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

"Kutokana na unyeti na umuhimu wa biashara ya mafuta, mamlaka inataka kupata mipango yako na jinsi ya kushughulikia suala hilo," ilifafanua barua hiyo ya Ewura.

Uamuzi huo wa Ewura ndiyo umefanya baadhi ya wafanyabiashara kuona kuwa suala hilo linaendeshwa kisiasa bila kujali maslahi yao, hivyo kutishia uhai wao.

"Mamlaka imekiri kuwa mafuta yaliyoingizwa nchini kipindi hicho yalikuwa yamechakachuliwa, kwa nini hatua zisichukuliwe na badala yake wahusika wanalindwa na kuombwa watoe maoni...tunakwenda wapi katika biashara ya mafuta," alisema.


CHANZO: NIPASHE

 
Maisha yanazidi kupanda serikali inahusika 99.9% tunaelekea wapi
 
are you sure jamaa wanataka kugoma?

unataka nikujibu....? Kaulize ewura wanavyohaha.....hivi hujui kua ccm imechemsha na inachefua sana sasa hivi......wanakazana kuua watu na kunyanyasa wananchi...............
 
Baadhi ya kampuni za mafuta zimetishia kugoma iwapo hatua hazitachukuliwa kurekebisha mpango wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja ambao umebainika kukumbwa na dosari ya kuwa na mafuta yaliyochakachuliwa.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kampuni hizo kuona hakuna hatua zilizochukuliwa ili kurekebisha dosari ya kuingizwa nchini mafuta yaliyochakachuliwa na ambayo yalisababisha kuyumba kwa biashara hiyo...


Tatizo watazungukana mbele ya safari..
 
Kwa mtondo huu wa kugomagoma kila kukicha tutafika mahala tutawagomea wake zetu kwa mambo ya ndani tu.
 
comprar nolvadex espana es un contra-estrogeno no-esteroida que inhibe eficazmente los receptors de estrogeno en los organos tratados y los tumores que estos incorporan.

nolvadex comprar comprar es un contra-estrogeno no-esteroida que inhibe eficazmente los receptors de estrogeno en los organos tratados y los tumores que estos incorporan.

El mecanismo de su accion no ha sido completamente investigado aunque se sabe que la combinacion del Nolvadex con el receptor y el cofactor si tiene lugar y que se transfiere al nucleo celular previniendo la hipertrofia de las celulas que dependen de la regulacion por lado del estrogeno.
 
Back
Top Bottom